Mambo niliyoyaona mechi ya Simba FC na JKT Tanzania

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Mambo 10 nilioyaona Simba vs JKT

Na: Ally Kamwe


1: Abdallah Mohammed Baresi Ushindi wa JKT ulianza kwenye kitabu chake cha ufundi. Ile 4-2-2-2 iliimeza kabisa 4-2-1-3 ya Sven. Kipindi cha kwanza walipoikamata Simba, katikati, wakamaliza hesabu zao

2: Sina hakika kama Sven alifanya research ya kutosha kuwajua JKT. Kwa namna yoyote ile, kwa ugumu wa viungo wa JKT, Ibrahim Ajib hakuwa chaguo sahihi kucheza kwenye 'role' ile
.
.
3: Shabani Mgundila What a player Box to Box midfielder aliyefanya majukumu yote uwanjani. Alikaba kibabe, akaanzisha kibabe. Kipindi cha pili alifanya kazi kubwa sana kuziba nafasi za mikimbio ya kina Chama

4: Mechi ilihimuhitaji Kahata tangu dakika ya kwanza. Skills zake, jicho lake la pasi lingeweza kua na madhara makubwa kwa JKT kuliko ilivyokua Ajib

5: Mechi ya pili mfululizo timu pinzani zinatumia dakika 15 za kwanza kuipress Simba. (Dhidi ya Polisi, Simba walifanya attempt ya kwanza golini dakika ya 18. Dhidi ya JKT wamefanya attempt ya kwanza ya maana dakika ya 16) hii si ishara nzuri kiufundi kwa Simba, hasa inapokua nyumbani

6: Uliwaona wale watu wa 4 wa JKT pale katikati. Nurdin Mohammed alikuwa mtulivu, Mgandila akawa mtukutu. Kazimoto akatengeneza space, Hafidh Mussa akapika mashambulizi. JKT wakiwa na mpira, Fraga akajikuta anashambuliwa na watu watatu kwenye zone yake

7: Adam Adam Bao la 6 msimu huu. Bado nasisitiza, akiongeza utulivu, aina yake ya uchezaji ni tishio kwa mabeki wengi VPL. Ana akili kubwa ya kunusa hatari, ni mastraika wachache sana ambao wangeweza kujitega pale kati ya Wawa na Kennedy.

8: Presha ya waamuzi dhidi ya Simba, imewaumiza Simba leo. Bao la Fraga lilikua halali kabisa.

9: Edward Songo Asante sana. Nilichokiona kwako mwanzoni, umekithibisha leo. Perfomance bora sana dhidi ya Simba

10: Kichuya hakua fiti. Luis Muquisone, yes. Kuna kitu ndani yake. Alifanya majukumu yake ya msingi na wakati fulani akaingia kati kufanya jukumu la Ajib

NB: Tukutane Airport

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pdidy,

Ujinga ni kumtukana au kumkashifu mtu usiyemjua kabisa, narudia tena andiko husika nila Ally Kamwe, huyu kaliiba kwenye akaunti husika na bahati mbaya sana ameshindwa kumu acknowledge mwenye andishi lake kinyume kabisa na taratibu za kiuandishi, nitoe tu ushauri kwako, kabla ya kubishania kwenye jambo lolote by your time ufanye research otherwise utaonekana kituko, watu wazima huweka hoja mezani, nothing else but hoja tu.
 
Ujinga ni kumtukana au kumkashifu mtu usiyemjua kabisa, narudia tena andiko husika nila Ally Kamwe, huyu kaliiba kwenye akaunti husika na bahati mbaya sana ameshindwa kumu acknowledge mwenye andishi lake kinyume kabisa na taratibu za kiuandishi, nitoe tu ushauri kwako, kabla ya kubishania kwenye jambo lolote by your time ufanye research otherwise utaonekana kituko, watu wazima huweka hoja mezani, nothing else but hoja tu.
Amekushambulia wakati hajui umemaanisha nini.. Ally Kamwe ndo mwenye kuandika haya kila mechi na hilo amecopy kila kitu na kuja kupest tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwamwala iyunga,

Yanga vichwa vyenu mmevitumbukiza kwenye shimo la kutolea taka.
Mko bize na simba kuliko timu yenu. Inakuaje mnashinda sasa ila bado gepu kubwa?
 
Back
Top Bottom