smarte_r
JF-Expert Member
- Nov 8, 2013
- 4,538
- 11,868
Tahadhari: kama umejiajiri au upo chuo na hufikirii siku moja kuja kuajiriwa, bandiko hili halikufai. "pita hivi".
Kama umeajiriwa au unafikiria kuja kuajiriwa siku sijazo, bandiko hili litakusaudia kukupa mwanga na uzoefu zaidi. karibu.
Moja ya jamii ambayo imebarikiwa katika suala la kumiliki mali hapa duniani, ni waarabu. bisha, kataa ila huo ndio ukweli.
Sihitaji kutaja makampuni makubwa ambayo waarabu wanayamiliki. fanya uchunguzi wako wewe mwenyewe.
Waarabu ni jamii inayoamini katika ujasiriamali na uwekezaji. wamewekeza katika kila sector ikiwemo zile zinazohitaji nguvu kazi kubwa. wapo kwenye sector ya viwanda, transport, hospitality, media nk.
Katika maisha yangu ya utafutaji, niliwahi kufanya kazi katika kampuni moja kubwa nchini inayomilikiwa na tajiri mwarabu. haya ndio niliyojifunza kuhusu jamii hii.
Kampuni zao hazifati mifumo rasmi ya kiutawala(poor management structure)
hawaamini katika supervisor mmoja anayeyeweza kusimamia majukumu yote. idara moja inaweza kuwekewa wakuu watatu au zaidi na wote wanatimiza majukumu yanayofanana. kiutendaji hii inaweza kupelekea ucheleweshaji wa kufanya maamuzi kwasababu ya mgongano wa kimawazo au kimaslahi wa baina ya wakuu wa idara.
Hawazingatii sana kiwango chako cha elimu bali unyenyekevu wako(loyalty).
hiyo degree au masters yako sio kitu kwenye kampuni za waarabu. Usiwaletee kiburi kisa wewe ni msomi sana au una perform vizuri katika eneo lako la kazi . hawababaishwi na hicho cheti chako.
Watakupiga chini faster na kuajiri mwingine. kuwa loyal kwa mkuu wako hata kama umemzidi elimu na efficiency.
Usiweke wazi masuala yako ya starehe hususani unywaji wa pombe.
moja ya kitu haramu kwa waarabu ni pombe. kama unakunywa basi hakikisha unakunywa kwa tahadhali kuepuka machawa wa boss wasijue mienendo yako ya starehe. mwarabu anaweza kukufukuza kazi kisa tu kafikishiwa taarifa kuwa wewe ni mlevi.
Wana entertain sana unafiki.
wanamlolongo mkubwa wa machawa wanaowatumia kuwapa taarifa mbalimbali.
anaweza akakuteua uwe msimamizi mkuu lakini mwisho wa siku akawa anamtumia mfagizi kupata baadhi ya taarifa za kampuni.
Hawazingatii viwango maalumu vya mishahara
katika kampuni za waarabu kila mtu ana kiwango chake cha mshahara kutegemea na vile ameingiaje katika kampuni hiyo. kama uliletwa na mmoja wa senior officers wa kampuni, HR atakuuliza unataka tukulipe shilingi ngapi kwa mwezi au atakujazia kiwango kizuri cha mshahara kwenye mkataba wako. kinyume na hapo itabidi ukubali kiwango chochote hata kama kitakuwa hakikidhi mahitaji yako.
Wanalipa mishahara mizuri na kwa wakati
kwa kiasi fulani jamii hii inajitahidi kuwalipa vizuri wafanyakazi wake. kampuni ambayo nilikuwa nafanyia kazi nilikuwa nalipwa vizuri na kwa wakati. ila ilikuwa ni mara chache sana kulipwa mshahara siku za weekend. mpaka leo sijajua ni kwanini. tarehe ya kulipwa mshahara ikidondokea ijumaa, jumamosi au jumapili hesabu maumivu. mshahara kwenye account yako utawekwa jumatatu.
Kiimani ijumaa ni siku muhimu sana kwa waarabu,iheshimu
kuna msemo unasema "when in rome, do as the romans do". huu usemi una maana kubwa sana unapofanya kazi kwenye kampuni za waarabu. ijumaa ni siku takatifu kwa kwao,vaa mavazi ya staha uwapo eneo lako la kazi. kama wanavaa kanzu na sundals na wewe vaa kama wao.hutopata hasara yoyote kwa kufanya hivyo.
NB: Kuajiriwa kwa mda mrefu ni utumwa, pambana ili mwisho wa siku ujiajiri na utengeneze ajira kwa wengine