Mambo mhimu ya kuzingatia katika siku ya mtoto wa Africa

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Kwa ujumla katika nchi yetu mtoto anatambulika tu kwamba ni mtoto mara baada ya kuzaliwa hadi anapofikia miaka 18, lakini nchi nyingine mtoto mtoto ni kuanzia miaka 0 hadi 16 na kwingine.

Jamii nyingi wananwachukulia watoto kama si kitu, wanawachukulia kama watotk sio sehemu ya jamii, wazazi na walezi wamekuwa wakiwafanyia mambo ya hovyo watoti, wapo wanaowapiga watoto, kuwachoma moto, kuwalawiti na kuwabaka watoto pia wapo wanaofanya biashara za kuwauza watoto kama bidhaa wanasahau kwamba watoto wana haki zao za msingi katika jamii.

Naomba kuwakumbusha mambo muhimu kwa watoto kama yafuatayo:


1.Haki za watoto zizingatiwe kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa na ulimwengu mzima kwa kuzingatia sheria za nchi husika na shirika la watoto duniani.

2.Kwakuwa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo basi wazazi na walezi wote tuwalee watoto wetu katika maadili bora kwa kuzingatia kuwa watoto wa leo pia watakuwa wazazi na viongozi baadaye kama ulivyo mzazi wa leo na kiongozi wa leo.

3.Kwakuwa wahenga walisema samaki mkunje angali mbichi basi tukubali kuwaonya watoto wetu wanapokwenda kinyume na maadili ya jamii husika ili warudi kwenye mstari sahawia tuyafanye haya kwa kujadili nao kirafiki na kuwaelewesha lipi ni jambo jema na lipi ni jambo baya.

4.Tuwajengee watoto hofu ya Mungu maishani mwao angali wadogo ili tusije tengeneza kizazi cha mafisadi, majambazi, wazizi, waongo, wanafiki na walevi n.k

5.Watoto wapewe urithi wao ambao ni elimu bila bugudha ya yoyote kwa kuzingatia mitaala ya elimu ndani ya nchi huska kwa wakati muafaka, urithi uzingatiwe kwa kuzilinda afya zao kwa kuwapa huduma bora za afya tukizingatia pia na lishe bora kwa watoto ili wasipate udumavu wa mwili na akili.

6. Tuache kuwatumikisha watoto katika shughuli zisizofa katika jamii kama vile kuwafanya wafanyakazi wa ndani,kuwatumikisha katika biashara haramu kama vile za madawa ya kulevya na kuuza miili yao.

7.Jamii zetu wawe mabalozi wakuwatetea watoto pale wanapoonelewa na wazazi au walezi wao pia jamii ifichue kama kuna hali ya uonevu na manyanyaso ya kwa watoto wadogo ili kuepusha watoto wasiathirike kisaikolojia.

9.Jamii ijiepushe kutumia lugha zisizo za staha kwa watoto kwani watoto wanaweza kushika mambo kwa haraka sana kichwani na huwa wanakumbukumbu kubwa.

10.Serikali iwe na mfumo mzuri wa kudhibiti familia zinazowafanya watoto watumwa katika nchi yao.

11.Serikali ichukue hatua kali za kisheria kwa walawiti, wanaopiga hovyo watoto, wanaowanyima watoto haki zao za msingi, wanaowaozesha watoto katika umri mdogo.
 
Back
Top Bottom