Mambo mengine utata mtupu.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Kuna mwalimu mmoja hapa Tunduma-Mbeya alioa mke ambaye tayari alikwisha zaa watoto wawili na mwanaume mwingine.Asubuhi tulivu,wameamka salama,mke kapokea simu,mara ghafla akadondoka chini,akapoteza fahamu.Alipozinduka,aliangua bonge la kilio cha kinyakyusa.Alipoulizwa kunani,akajibu kuna ndugu wa karibu kafariki nyumbani kyela.Alipoulizwa ni nani kafariki,akajibu,'nitakwambia nikifika'.Kwa kuwe mume hali ya kifedha haikuwa nzuri,akaamua kuuza ng'ombe mmoja wa kisasa,akamkabidhi mkewe nauli na pesa ya matumizi.Baada ya kufika kule kyela,mke akapiga simu kumtaarifu mumewe kwamba mtu aliyefariki ni baba aliyezaa naye wale watoto wawili.Mume aka-panic vibaya na kumwambia aishie huko huko kyela na asirudi tena tunduma.Sijui wakuu mnalionaje hili.
 
Mhhh mambo mengine ngumu aise kuwa na la kusema
Ana familia na huyu mume mpya au hakuwahi kupata nae mtoto
Kama hakuna kinachowaunganisha hapo akubalia hasara ya ng'ombe wake aanze upya maisha ajipange upya
 
Ukweli haubadiliki, angesema tu ex- kafariki.
Ukweli hukuweka huru.

Swali: Huyo mwalimu alijua au hakujua au hakutaka kujua kama ex- wa huyo my waifu wake alikuwa hai?
 
Si lazima kuwa huyo mama alilia kwa kuumizwa na kifo cha mzazi mwenzie....inawezekana pia amelizwa na sababu ya kifo cha mzazi mwenzie huyo, especially sababu yenyewe ya kifo inaambukiza!
 
Mhhh mambo mengine ngumu aise kuwa na la kusema
Ana familia na huyu mume mpya au hakuwahi kupata nae mtoto
Kama hakuna kinachowaunganisha hapo akubalia hasara ya ng'ombe wake aanze upya maisha ajipange upya
Kazaa naye watoto wengine wawili!
 
Kazaa naye watoto wengine wawili!

Duh hapo pagumu
Ajihakikishie tu kuwa yuko salama alee watoto wake
Ila bado ana nafasi ya kumuuliza mtu wake kuhusu upendo baina yao na kilichomfanya ashindwe kumwambia wazi kuwa mtu wake wa zamani amefariki
 
ah kawaida mbona...sasa yeye alitegemea kuwa kwa kuwa amemchukua basi ndio kafita kabisa baba watoto...chizi huyo. ni natural response jamani sii mtu kafaa na walishare life mpaka kuzaa
 
uyu mama alikuwa anauzimikia bado mzigo wa zamani.Usikute friendly match zilikuwa zaendelea kama kawa
Kwa kuwa ndo ushavuta jamaa sasa ashangilie na kumwambia mamaa arudi
 
Kuna mwalimu mmoja hapa Tunduma-Mbeya alioa mke ambaye tayari alikwisha zaa watoto wawili na mwanaume mwingine.Asubuhi tulivu,wameamka salama,mke kapokea simu,mara ghafla akadondoka chini,akapoteza fahamu.Alipozinduka,aliangua bonge la kilio cha kinyakyusa.Alipoulizwa kunani,akajibu kuna ndugu wa karibu kafariki nyumbani kyela.Alipoulizwa ni nani kafariki,akajibu,'nitakwambia nikifika'.Kwa kuwe mume hali ya kifedha haikuwa nzuri,akaamua kuuza ng'ombe mmoja wa kisasa,akamkabidhi mkewe nauli na pesa ya matumizi.Baada ya kufika kule kyela,mke akapiga simu kumtaarifu mumewe kwamba mtu aliyefariki ni baba aliyezaa naye wale watoto wawili.Mume aka-panic vibaya na kumwambia aishie huko huko kyela na asirudi tena tunduma.Sijui wakuu mnalionaje hili.

"Truth shall set you Free"
 
Mhhh mambo mengine ngumu aise kuwa na la kusema
Ana familia na huyu mume mpya au hakuwahi kupata nae mtoto
Kama hakuna kinachowaunganisha hapo akubalia hasara ya ng'ombe wake aanze upya maisha ajipange upya[/Q

Sawa akaanze maisha upya lakini iwe baada ya kupima UKIMWI, kwani hatujaambiwa chanzo cha kifo cha yule bwana; isije ikawa ngoma!!
 
Hii info ni incomplete kwa kutoa ushauri wa maana wachangiaji watabaki wana assume. More info tafadhali.
 
Duh, kuna watu wanaoana kama vile wanaigiza.

Maswali Mme: hakujua kama kuna watoto? Hakufanya due diligence hata kidogo? Watoto wawili unaweza waficha?
Maswali Mke: Kwa nini alificha msiba? Kwa nini alisema baada ya kufika huko.

Hii story ya kutunga, ila ya kwenye magazeti ya 'ungekuwa ww ungefanyaje?'
 
Kuna mwalimu mmoja hapa Tunduma-Mbeya alioa mke ambaye tayari alikwisha zaa watoto wawili na mwanaume mwingine.Asubuhi tulivu,wameamka salama,mke kapokea simu,mara ghafla akadondoka chini,akapoteza fahamu.Alipozinduka,aliangua bonge la kilio cha kinyakyusa.Alipoulizwa kunani,akajibu kuna ndugu wa karibu kafariki nyumbani kyela.Alipoulizwa ni nani kafariki,akajibu,'nitakwambia nikifika'.Kwa kuwe mume hali ya kifedha haikuwa nzuri,akaamua kuuza ng'ombe mmoja wa kisasa,akamkabidhi mkewe nauli na pesa ya matumizi.Baada ya kufika kule kyela,mke akapiga simu kumtaarifu mumewe kwamba mtu aliyefariki ni baba aliyezaa naye wale watoto wawili.Mume aka-panic vibaya na kumwambia aishie huko huko kyela na asirudi tena tunduma.Sijui wakuu mnalionaje hili.

Mh!!!!!!!! huyo mwanaume wivu mpaka msibani inahusu
 
sasa hapo hasira ni kwa sababu
au
mkewe kwenda msibani?
au
ng'ombe aliyeuzwa?

Nafikiri ticha aligundua kuwa marehemu alikua bado anapiga moja moja na akifikira kwamba visafari vya hapa na pale vilikua vya kutosha inakua ni ngumu kumeza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom