Mambo makubwa Matano kutokea baada ya 25th Oct

Mambo makubwa Matano kutokea baada ya 25th Oct

mongoya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2014
Posts
298
Reaction score
120
Wana Jf
Yafuatayo ni mambo makubwa matano kutokea baada ya 25 Oct;
-Kambi imara ya upinzani chini ya ZZK,SLAA NA LIPUMBA Kuasisiwa
-Historia ya Mwanasiasa mashuhuri ENL kufananishwa na AUGUSTINO E MREMA
-Chama cha CUF ndio basi tena.
-Mikakati kabambe ya kuimarisha CCM kuongezeka.
-Mpasuko mkubwa kutokea na kuiangamiza CHADEMA

Haya ni maoni yangu tu kama unachakuongeza Karibu!
 
Nasikia Redet wamesita kutoa matokeo ya utafiti wao wa Karibuni!! BTW kesho una hela ya kuanzia siku from lumumba.
 
Bahati mbaya ccm wamemtuma tena mkapa awaite watz mbumbu....
Hapo patamu kwa jinsi nilivo na hasira
 
Endeleeni kuota mkiwa mmesimama maana siku hizi ata usingizi hampati
VIVA UKAWA
 
Mbona hayo mambo ni madogo...

Mambo makubwa ni pale tu CCM itakapoaga...
 
Yule mtabiri wenye maccm kishajifilia. Kama hakuweza hata kutabiri kifo chake sembuse nyiye msojua hata kuangalia tu nyota ya kijani??
Mmejichimbia choo mtatumbukia wenyewe. Alipokuwa anazitoa zile ahadi elfu elfu hamkujua kuwa msipozitimiza nd kifo chenu?? Hamtoki nasema. Ati hapa kazi tu, hilo nalo ni neno kuweza kuwadanganya tena nalo Watz?? Akikuchagua mtu, jua ni taahira.
Elezeni mlilolitenda sio mangonjera ati tuliingia madarakani tutaaaa kwani nyiye ni upinzani?? Ati, nikiwa rais, nitahakikisha mnakuta dawa hospitalini, Ajiulize, huyo Magofuli anakuja nazo mfukoni??
Mmekwisha mmefilisika, sasa mmebaki kuota ndoto tuuuuu
 
KWA HAYA CCM ITAINGIA KATIKA KUMBUKUMBU ZA MSAJILI WA HAZINA
“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,malofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Wana Jf
Yafuatayo ni mambo makubwa matano kutokea baada ya 25 Oct;
-Kambi imara ya upinzani chini ya ZZK,SLAA NA LIPUMBA Kuasisiwa
-Historia ya Mwanasiasa mashuhuri ENL kufananishwa na AUGUSTINO E MREMA
-Chama cha CUF ndio basi tena.
-Mikakati kabambe ya kuimarisha CCM kuongezeka.
-Mpasuko mkubwa kutokea na kuiangamiza CHADEMA

Haya ni maoni yangu tu kama unachakuongeza Karibu!

Sheheee giuza basii na nyuma yake .kama samaki au wewe unakula samaki upande
 
NCCR mageuzi kupasuka na kupotea kabisa katika ramani
 
Wana Jf
Yafuatayo ni mambo makubwa matano kutokea baada ya 25 Oct;
-Kambi imara ya upinzani chini ya ZZK,SLAA NA LIPUMBA Kuasisiwa
-Historia ya Mwanasiasa mashuhuri ENL kufananishwa na AUGUSTINO E MREMA
-Chama cha CUF ndio basi tena.
-Mikakati kabambe ya kuimarisha CCM kuongezeka.
-Mpasuko mkubwa kutokea na kuiangamiza CHADEMA

Haya ni maoni yangu tu kama unachakuongeza Karibu!


Wee jipe nafuu tu!
 
Back
Top Bottom