Mambo kumi yanayoweza kufanya mwanaume akuache | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo kumi yanayoweza kufanya mwanaume akuache

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Wa Mjengoni, Feb 1, 2011.

 1. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Binafsi mimi ni mgeni jukwaa hili lakini katika pitapita zangu gp nimeikuta hii ikanikuna, hebu tuijadili:


  Mambo kumi yanayoweza kufanya mwanaume akuache

  Bila shaka u mzima wa afya mpendwa msomaji. Leo nimeandaa mada juu ya mambo
  kumi yanayoweza kukufanya mwanamke ukaachwa na mume/mpenzi wako. Twende pamoja...

  1.KUWA MWIGIZAJI
  Uigizaji unaozungumzwa hapa siyo wa filamu lakini ni ile hali ya kujitengenezea tabia ambazo siyo rasmi. Kwa mfano wewe ni masikini lakini unajifanya ni mtoto wa tajiri au wakati mwingine unaazima nguo za watu kwa lengo la kujiweka juu na tabia za kufanana na hizo. Ukiwa mwanamke uliyependwa, usithubutu kudanganya uhalisia wako kwa kitu chochote. Wanaume hawapendi kabisa tabia hiyo.

  2.KUWA TEGEMEZI
  Katika ulimwengu huu tunaoishi sasa, wanaume wengi hawapendi wanawake tegemezi. Katika hili uchunguzi umeonesha kuwa wanawake wenye kazi ni rahisi kuolewa kuliko wasiokuwa na kazi. Hii ina maana kwamba wanaume hawapendi kutegemewa kwa kila kitu na inapotokea hali hiyo ni rahisi kwao kubwaga manyanga na kutafuta penye unafuu. Kamwe usikubali kuwa mwanamke wa ‘nitumie vocha’, ‘naomba hiki’, ‘naomba kile’ kila siku, utaachwa.

  3. USIKIVU
  Ingawa tafiti zinaonesha kuwa wanawake huzungumza zaidi kuliko wanaume, ukweli unabaki kuwa wanaume hutaka kusikilizwa katika machache wanayosema au kuagiza. Endapo mwanaume atakuwa akisema jambo fulani na mwanamke haoneshi usikivu, ni rahisi kwake kufikiria kuwa anadharauliwa na hivyo kuamua kuachana na mwanamke huyo. Kwa mantiki hiyo, wanawake wanatakiwa kuwa wasikivu kwa wanaume vinginevyo watajiweka katika mazingira ya kuachwa.

  4.MATUMIZI MAKUBWA
  Inawezekana jambo hili linasababishwa na ugumu wa maisha ambao umewafanya wanaume wengi kubana matumizi. Inapotokea mwanamke akawa na matumizi makubwa ya fedha na vitu, humkera mumewe/mpenzi wake. Ewe dada/ mwanamke, katika kulinda uhusiano wako jitahidi kuhakikisha kuwa matumizi yako yanakuwa ya chini kuanzia mnapotoka ‘out’ na mumeo mpaka kwenye fedha za matumizi ya nyumbani unazoachiwa.

  5. UBINAFSI
  Maisha ya mapenzi yanataka umoja. Wanaume wanaamini sana kwenye hili hivyo wanapoona wenza wao wamekuwa wabinafsi katika mafanikio au mipango yao ya kimaisha, huingiwa na wasiwasi na kuhisi kuwa hawapendwi. Ikifikia hatua hii, huamua kujitoa kama njia ya kujihami au kutetea uanaume wao.

  6. KUMTAFSIRI
  Wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kuwatafsiri wanaume kadiri wajuavyo wao bila umakini: “Nilijua uliposema hivyo ulitaka niondoke.”

  Wanaume huamini kuwa wao ni walimu hivyo linapotokea suala la mwanamke kushindwa kuelewa na kutafsiri maneno kinyume na lengo la mhusika, hujiweka kwenye kundi baya la uelewa mdogo na hivyo kujiongezea hatari ya kuachwa. Unapokuwa kwenye mazungumzo na mumeo, usimtafsiri na endapo hilo litatokea basi jitahidi kutafsiri kwa usahihi kile alichokiongea.

  7. KULAZIMISHA VITU
  Uchunguzi unaonesha kuwa, wanaume hawapendi kulazimishwa kufanya mambo na inapotokea mwanamke akaweka msukumo mkubwa wa kuhakikisha mwanaume anatekeleza kitu fulani (bila kujali umuhimu wa jambo lenyewe), ulazima huo hugeuka kuwa kero inayoweza kumfanya apoteze penzi lake. Ushauri kwa wanawake ni kwamba hata kama jambo fulani lina umuhimu, wasiweke lazima yenye kukera.

  8. KUTENDA KINYUME
  “Naomba pesa hii uiweke, ikifika elfu kumi tutanunua unga.” Litakuwa jambo la ajabu na lenye kuvunja moyo kama mwanaume ataagiza hivi halafu akakuta baadaye mwanamke kazitumia zile pesa kununulia nyama kwa hoja kwamba walikuja wageni. Wanaume hupenda wanawake wafanye sawa na walivyoagiza na linapotokea jambo la kubadilisha basi waulizwe kwanza.

  9. KUTOJIAMINI
  Mitindo ya wanawake kuwafuata fuata wanaume kwa kupekua simu zao na mitandao yao kwa lengo la kujihami na usaliti ni jambo linalowaudhi wanaume wengi. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wanapenda kuwa huru na kuheshimiwa siri zao kuanzia mishahara na hata nyendo zao na marafiki zao wakiwemo wa kike.

  Hali ya kuwauliza na kuwabana wanakopita walikuwa na nani huondoa mshawasha wao wa kimapenzi na kujikuta wakiamua kuutafuta uhuru wao kwa kuachana na kero hiyo ya kufuatiliwa kupita kiasi. Ukiwa kama mwanamke, jiamini na uache mumeo ajichunge mwenyewe. Gubu la kujilinda halifai kabisa.

  10. KUMGEUZA KITABIA
  Licha ya kuwa wanawake wana jukumu la kuhakikisha wenza wao wanaishi katika njia sahihi, wanaume hawapendi kubadilishwa tabia kwa nguvu. “Kwa nini umekunywa pombe? Si nilikukataza? Leo utalala chini.” Njia hii ya kumgeuza tabia mwanaume kwa lazima haifai na inaweza kusababisha akuache. Nenda pole pole ukiamini kubadili tabia siyo kitu cha siku moja.
   
 2. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Makungwi na wafundaji wa kwenye kitchen party, mnaonaje hapa si kuna vingi vya kuchukuwa!
   
 3. V

  Vumbi Senior Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii point ya 8 inaumuhimu mkubwa sana ndani ya ndoa. Ukitaka ndoa yako idumu hata siku moja usifanye kinyume cha makubaliano, kama unawazo tofauti kwanza muone mumeo mkubaliane. Hili jambo linasabibisha wanaume wengi kutowahusisha wake zao kwenye mambo ya msingi ya familia then mwamke anakuwa mtu wa kusubiri matokeo. Hakuna kitu kinacho niudhi kama nakubalia na mke afanye jambo falani kwa taratibu flani halafu yeye anafanya anavyotaka.

  8. KUTENDA KINYUME
  "Naomba pesa hii uiweke, ikifika elfu kumi tutanunua unga." Litakuwa jambo la ajabu na lenye kuvunja moyo kama mwanaume ataagiza hivi halafu akakuta baadaye mwanamke kazitumia zile pesa kununulia nyama kwa hoja kwamba walikuja wageni. Wanaume hupenda wanawake wafanye sawa na walivyoagiza na linapotokea jambo la kubadilisha basi waulizwe kwanza.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni nzuri ila nadhani ilitakiwa ziwekwe kama sababu zinazoweza kumfanya mwenzi akuache ME/KE!Kwasababu hata wanawake hatupendi..MWANAUME MWIGIZAJI..TEGEMEZI..ASIYE MSIKIVU..MWENYE MATUMIZI MAKUBWA YA BINAFSI..MBINAFSI..ANAYETAFSIRI VITU TOFAUTI NA MAANA HALISI..KING'ANG'ANIZI..ANAEENDA KINYUME CHA MAKUBALIANO..ASIYEJIAMINI..ANAEHANGAIKA KUMBADILISHA MWANAMKE ASIYEHITAJI MABADILIKO..MBISHI BILA KUSAHAU MJUAJI!
   
 5. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata wanawake hawapendi hayo uliyotaja.

  Nani anapenda tegemezi (marioo), kulazimisha vitu (Specifically ngono), matumizi makubwa, ubinafsi nk.

  Wewe ungesema sababu zinazofanya mke/mume kukuacha si kuwa tu mwanaume mtaacha lini kuonea wanawake nyie aahhhh

  BTW: Im gender sensitive
   
 6. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Samahani dadangu mimi nimenukuu tu toka kwenye source - global publishers - usichukulie kuwa Wa Mjengoni ni wa mfumo dume, la hasha!
   
 7. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mjengoni,

  yaani haya ulioyazungumza yoote ni kweli kabisa. Aisee usiombe ukakutana na Mwanamke wa aina hiyo, halafu mbaya zaidi awe na elimu na ana kazi nzuri...! Mwanaume utakimbia nyumba bila kujijua...! Wanawake wengi sana hujusahau sana, wanasahau kwamba mwanaume ndio kichwa cha nyumba, na yeye ni msaidizi kwa mwanaume.
   
 8. comred

  comred JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 1,392
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  atakaye pinga haya bc nae anatabia mojawapo kati ya hzi...nashkuru kwakufikisha huu ujumbe bcoz mst of thm wako namna hii....shukran tena
   
 9. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwl hayo mambo huvunja mahusiano ati ila kwa pande zote mbili .zaid najua wanaume wanapenda mwanamke mkweli,yaan ukiwa muongo talaka nje nje.ila kuhusu hiyo no 4 jibu la kudumu ni kuoa mpare tu
   
 10. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135  mwe!!!!
   
 11. Atoti

  Atoti Senior Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  I was thnkng of the same thng ya ubahili wkt nasoma pt 4 hahahaha umenivunja mbavu Fl..
   
 12. A

  Aine JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli mambo hayo kumi karibu yote yanawahusu wote iwe mwanamke au mwanaume, so tuchukulie kuwa ni ya wote please
   
 13. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,797
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kuna nyingine mbili ziongezee hapo.
  11. UAMINIFU KATIKA UHUSIANO.
  Endapo mwanaume atagundua mwanamke alishirikiana na Mwanaume mwingine wakati akiwa tayali na uhusiano na yule wa kwanza, hapo ni rahisi sana Mwanamke kuachika hata kama itatokea aliachana na huyo jamaa wa pili. Hili ni donda ndugu kwa Wanaume, akigundua kitu hicho hata kama atasamehe, uhusiano huo huwa umeharibika tayali, utakua unashikiriwa na nyuzi ya pamba na wakati wowote hukatika. Mwanaume makini hupoteza imani kwa Mwanamke wake endepo akigundua au hata kuhisi mpenzi wake alichepuka katika mahusiano yao na kushiriki au hata kutaka kushiriki na mwanaume mwingine.
  12. KUFANYA MAKOSA KWA KIGEZO CHA MSAMAHA
  Wanawake wengi wamekua na tabia ya kurudiarudia makosa na kupenda kuwahi kuomba msamaha, hili ni jambo linalowakera Wanaume na kuhisi huwa wanafanya makusudi wakijua wataomba msamaha, tena Mwanaume hupenda kujua chanzo cha tatizo ili aweze kujua namna ya kusaidia lisitokee tena lakini wanawake wengine wamekua wepesi kukimbilia kwenye msamaha bila kutaka kuelezea kisa na mkasa wa kosa husika. Mbaya zaidi ni pale inapogundulika Mwanamke alitoka nje kisha anaomba msamaha kwa kigezo cha kosa la kwanza, hili ni doa tayali katika mahusiano, Mwanaume anaweza samehe lakini huwa kukubali yaishe ila jambo hilo hupoteza uaminifu kwa asilimia kubwa kwa Mwanaume dhidi ya mpenzi wake na muda wowote anaweza bwaga manyanga. Kwa kigezo cha kosa la kwanza, Mwanaume huvuta subira akisubiri lolote lijitokeze tena na hapo huunganisha na hilo la kwanza kubwaga manyanga hata kama makosa hayafanani.
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Kumbe umetoa Global Publisher nilidhani yako. Ok basi uwe unaedit kidogo ili watu wasikuchukulie we mtu wa mwaka 47
   
 15. M

  Msindima JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  FL umenichekesha mie.
   
 16. e

  emiliana hyera Member

  #16
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 17, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  there ua lizzy
   
Loading...