Mambo Binafsi kuyaweka hadharani

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,165
1,361
Mapema leo nimeona nyuzi mbili ambazo nadhani ni za kibinafsi mno kuwekwa hadharani. Moja ilihusu wosia wa Reginald Mengi ukitaja mali yake igawanywaje akifa. Kitu kama hiki sidhani kama hata ndugu wangependa kiwekwe hadharani namna hii. Kama kitu kinatajwa mahakamani, hapo kinakuwa ni cha umma kwa kuwa mahakama ni chombo cha wazi na mtu yo yote, ahusikaye na asiyehusika, anaruhusiwa kuhudhuria

Uzi mwingine ulimhusu mmiliki wa mjengo wa Kibo, kuwa anaweza kuwa kati ya Weusi kumi matajiri zaidi. Hii nayo naona haina ueledi katika maendeleo ya mwananchi wa kawaida. Kama ni hivyo, au kama sivyo, inamsaidiaje mwananchi wa kawaida katika kujikwamua kutoka kwenye matatizo yake? Badala ya kukaa na kufikiria jinsi gani mtu uboreshe maisha yako, unakaa kujadili mali za wenzako. Hili nalo ni jambo la kibinafsi mno.
 
Acha kuingilia uhuru wa watu kuandika humu, ukishakua public figure kama Reginald Mengi basi ujue hata ukijamba watu lazima wajadili.
 
Mkuu ni viungo vya uzazi tu ndio vya kuficha hivyo vingine sio mbaya vikiwekwa hadharani
 
Back
Top Bottom