BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Msekwa akosa uvumilivu kwa Warioba
2008-09-30 11:37:50
Na Simon Mhina
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa, ameshangaa madai ya Jaji Joseph Warioba kwamba vikao vya chama hicho vimejaa visasi na kukomoana na kumtaka aache kile alichokiita `usongombwingo`.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka Tarime jana, Msekwa alihoji kwa kusema: ``Wewe Mwandishi unajua maana ya Usongombwingo? Usongombwingo ni umbea uliojaa uzushi na uongo.``
Akifafanua, Msekwa alisema kwa vile vikao anavyolalamikia Warioba vya Umoja wa Wanawake (UWT) vilikuwa vya siri, na wala yeye hakuwa mjumbe, kwa vyovyote alipelekewa taarifa za vikao hivyo na wambea na hivyo kujikuta anajiingiza kwenye usongombwingo bila kujijua.
Msekwa alisema ameshangazwa na kauli ya Warioba kwamba Baraza Kuu la UWT lilitumika kumkomoa mmoja wa wanachama wake aliyeomba kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Halima Mamuya na kumpa alama `E`.
Alisema ameshangaa kuwa Warioba amepata wapi habari za Mamuya kupata alama `E` wakati vikao vya UWT vinahudhuriwa na wanawake watupu.
``Mimi nimeshangaa kama kweli Warioba katoa shutuma hizo kapata wapi taarifa za vikao vya UWT?
Vikao vile ni vya wanawake watupu, yeye alikuwepo? Hata wewe wa Nipashe unaponiuliza pia nakushangaa, mimi ni mwanaume hivyo huko UWT sikuwepo, labda muulize huyo huyo aliyetoa shutuma, labda yeye alikuwepo siwezi kujua mimi niko Tarime,`` alisema Msekwa huku akiangua kicheko.
Kikao cha Baraza Kuu la UWT kilichopitisha majina hayo na kumpa Mamuya alama E kilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Anna Abdallah ambaye ni mke wa Msekwa.
Msekwa pia alisema kisheria mtu anayetoa tuhuma ndiye anayetakiwa athibitishe.
Alisema kwa vile yeye bado hajapata taarifa rasmi juu ya madai hayo, hawezi kuzungumzia `usongombwingo` kwa vile akifanya hivyo atakuwa anajiingiza katika mambo asiyoyajua.
Alisema kimsingi Chama hakiwezi kuingilia maamuzi ya vikao vya jumuiya zake, kabla ya kuletewa taarifa zilizorasmi.
``Tunaziamini jumuiya zetu na taratibu zao, hatuwezi kuwaingilia kwa kutoa maamuzi kabla hawajatuletea taarifa rasmi juu ya vikao vyao na yale waliyojadili na kuamua,`` alisema Msekwa.
Kuhusu Nape Nnauye ambaye naye amepewa alama `E` katika mchujo huo kwenye Jumuiya ya Vijana (UVCCM), Msekwa alisema hata kwenye jumuiya hiyo, taarifa za vikao vya mchujo hazikufika rasmi.
Havi karibuni Warioba alikaririwa na gazeti hili akishutumu tabia iliyoibuka hivi karibuni ya wajumbe wa vikao mbalimbali vya CCM kuvitumia kulipa kisasi na kuwakomoa wanachama wanaoomba kuwania nafasi mbalimbali na kuwapa alama wasizostahili.
Warioba alisema Mamuya na Nape hawakustahili kupata alama `E` inayomaanisha muombaji hajui hata itikadi ya CCM.
SOURCE: Nipashe