Mambo 7 ya kujifunza katika siasa na uongozi

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
MAMBO 7 YA KUJIFUNZA KATIKA SIASA NA UONGOZI

(1) Kwenye siasa Usiabudu watu yatupasa tukumbatie misingi sahihi kwasababu watu huja na kuondoka ila misingi sahihi huendelea kuwepo.

(2) Usithubutu kukurupukia ugomvi/msuguano wawote ambao huuelewi kiini chake, leo wanaogomban/waonasuguana kesho wanapatana utafedheheka. Mzee JK anasema usikubali kurithishwa maadui! Wala tusiwe mabingwa wa kujinafikisha ili kupata mahitaji ya Wakati! Ni heri kubaki peke yako kuliko kutumika ili kufurahisha mtu!

(3) Tujiikite kwenye kuchambua maswala ya msingi(issues) zenye manufaa na yatakayoaacha Alama/athari kwa jamii badala ya kujikita kuchambua watu.

(4) Tutambue kuna maisha nje ya siasa. Hivyo si lazima uwe ktk nafas hizo Muda wote hata pale ambapo inaonekana zama haziko nawe! Tusilazimishe! Uongozi si jambo la kufa na Kupona!

5) Tujifunze kunyamaza. Mungu ametupa maskio mawili na mdomo mmoja ili tusikilize zaidi kuliko kuongea. Japo kuna wakati tunatamani kusikika ili tufafanue, Kujibu au kukosoa mambo kadha wa kadha lakini hekima yatuasa sana tunyamaze! akushindaye kuongea Mshinde kunyamaza. Kimya ni tiba.

(6)Tusiogope kusimama upande ulio sahihi hususani kutetea maslahi ya wengi hususani wananchi wanaotutegemea ama kukutarajia. tuwatetee na kuwapigania. Hata kama kufanya hivyo kutatugharimu! lakini tunu yetu mbinguni ni kubwa.

(7) Tusome alama za nyakati na majira. Mbu hawafanani kati ya masika na Masika! Mzee Kinana anasema mwanasiasa ama kiongozi mzuri ni yule anayejua wakati wa kuingia na wakati wa kutoka! Somo hili lilimpita kushoto Mzee Mugabe, hayati Gadaf na wengine wengi sana!

Kuchibumba Sumbalawinyo
 
Back
Top Bottom