Mambo 6 yakuzingatia katika mahusiano ya kimapenzi

malisak

Platinum Member
Joined
Mar 16, 2006
Posts
739
Reaction score
853
Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limetetereka na kiwango kimeshuka baina yao.​
Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za kukusaidia

1. kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo. Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua na sisi pia.

3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala. Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?
Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa katika mahusiano yenu.

4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.

5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.

6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano wetu lazima ume halisi na sio feki. Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu. Ukianza kupata ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote mpenzi wako alivyonavyo ambavyo hukuza ukaribu wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.
 
Dah, kwa mtu ambae ameoa na ana watoto kuanzia wawili na anaipenda familia yake naona hausiki kwa uzi huu.
Binafsi before hatujawa na watoto nilikuwa nikitoka kazini nikifika home nafikia ktk mikono na kifua cha wife, mabusu,kupapaswa na pole ningi ilikuwa ada, nikipumzika kidogo naambiwa maji ya kuoga tayari kaondoe uchovu nimekumis, nikishaoga nakutana na juice au maziwa fresh mezani kabla ya chakula japo na chenyewe kimeshaiva na mwenyewe kashaoga katulia. Tunakula na kulishana vizuri, tunaangalia tv na mbwembwe nyingine kibao kabla ya kwenda kitandani.

Baada ya watoto wawili sasa. Nikirudi napokelewa na watoto na kazi zao za shule, niwasimamie mmoja mmoja na kufanya nao marudio. Mama yupo jikoni ndio anapambana kupika maana tangu asubuhi alipoamka alianza na kuwaanda watoto na kuwaandalia kifungua kinywa baada ya hapo ni anafua nguo zetu watu wanne, usafi wa mazingira, amewapeleka na kuwachukua shule, amewapikia na kuwaogesha maji vuguvugu, kaenda gengeni kuhemea cha siku hiyo, kachoka hata kuoga bado.
Baada ya mimi kumaliza kuwasaidia kazi zao nikimcheki wife alivyo na harakati nyingi maji ya kuoga nijiwekea mwenyewe na baada ya hapo nakuja kutulia na watoto ili wasisinzie japo walilala mchana. Mama anatutengea chakula nakula na watoto ili wasilale na yeye anaelekea kuoga. Akija kula akiingia kitandani sekunde 59 keshalala kwa uchovu.

Yale niliyoyaeleza mwanzo yenye bashasha na mbwembwe nyingi yametoweka yenyewe automatically, sio sisi ni hali. Kuna siku nilijaribu kumlisha chakula mbele ya watoto, dah, walicheka balaa halafu yakafuata maswali kama nipo ktk interview.
Kila jambo lina mwanzo na mwisho, maisha ya kuishi kwa mazoea hayaepukiki ktk maisha ya ndoa.
 
Kilichotokea hapo mkuu ni kupotea kwa mwemko kat yenu na kuanza kuishi kwa, azoea kitu ambacho ni hatar ktk uhai wa furaha OG ya ndoa yenu...... Kama unafuatlia mafunzo ya DR. ELIE clouds Chomoza...... Utajfunza namna ya kutoka ktk hyo hal.......... Inaonesha kuwa mkeo na ww mmekubali kubebwa na upepo wa hali..... Jiulze mbona wenzetu wazungu au hata waafrika wejijengea utamaduni unaowafanya wawe active kwny mapenz/ndoa zao kila wakat!??......

Ni kawaida hata ukinunua gar leo utakuwa na ham nayo sana kwa kipnd flan then after unaiona ya kawaida........ Hata kwa mke ni hvyo cha msingi jenga utamaduni wa kuji update
 
Dah, kwa mtu ambae ameoa na ana watoto kuanzia wawili na anaipenda familia yake naona hausiki kwa uzi huu.
Binafsi before hatujawa na watoto nilikuwa nikitoka kazini nikifika home nafikia ktk mikono na kifua cha wife, mabusu,kupapaswa na pole ningi ilikuwa ada, nikipumzika kidogo naambiwa maji ya kuoga tayari kaondoe uchovu nimekumis, nikishaoga nakutana na juice au maziwa fresh mezani kabla ya chakula japo na chenyewe kimeshaiva na mwenyewe kashaoga katulia. Tunakula na kulishana vizuri, tunaangalia tv na mbwembwe nyingine kibao kabla ya kwenda kitandani.
Baada ya watoto wawili sasa. Nikirudi napokelewa na watoto na kazi zao za shule, niwasimamie mmoja mmoja na kufanya nao marudio. Mama yupo jikoni ndio anapambana kupika maana tangu asubuhi alipoamka alianza na kuwaanda watoto na kuwaandalia kifungua kinywa baada ya hapo ni anafua nguo zetu watu wanne, usafi wa mazingira, amewapeleka na kuwachukua shule, amewapikia na kuwaogesha maji vuguvugu, kaenda gengeni kuhemea cha siku hiyo, kachoka hata kuoga bado.
Baada ya mimi kumaliza kuwasaidia kazi zao nikimcheki wife alivyo na harakati nyingi maji ya kuoga nijiwekea mwenyewe na baada ya hapo nakuja kutulia na watoto ili wasisinzie japo walilala mchana. Mama anatutengea chakula nakula na watoto ili wasilale na yeye anaelekea kuoga. Akija kula akiingia kitandani sekunde 59 keshalala kwa uchovu.
Yale niliyoyaeleza mwanzo yenye bashasha na mbwembwe nyingi yametoweka yenyewe automatically, sio sisi ni hali. Kuna siku nilijaribu kumlisha chakula mbele ya watoto, dah, walicheka balaa halafu yakafuata maswali kama nipo ktk interview.
Kila jambo lina mwanzo na mwisho, maisha ya kuishi kwa mazoea hayaepukiki ktk maisha ya ndoa.
Hali ya mwenza wangu kuchoka ndio inayonitokea siku hizi,natamani hata kumtafutia mwenza sema magonjwa nayo ni mengi...naishia kujichua tuu
 
Akiingia kulala hiyo mida ya saa nne mvungie mpaka usiku wa manane akikurupuka kukojoa tu unae hapohapo, maisha ya ndoa yana changamoto zingine hazisemeki watu wengi wanakufanazo.
 
Sasa hapo vipi akisema hataki ana usingizi bana utamfosi?
 
Hapo ndio ubakaji wa kwnye ndoa unapoanzia
Hahahah na kwa wenzetu kule sheria zilipokomaa ukimfosi mke kwa design hio anaweza file charges dhidi yako ukaishia jela! Aheri ya kwetu huku unaweza lazimisha gemu mwanamke akatoa hata kwa mikiki ila ukafanikiwa kumwaga, but haibadili maana kuwa hamna raha ya ku sex mtu kwa kumlazimisha!
 
Dah, kwa mtu ambae ameoa na ana watoto kuanzia wawili na anaipenda familia yake naona hausiki kwa uzi huu.
Binafsi before hatujawa na watoto nilikuwa nikitoka kazini nikifika home nafikia ktk mikono na kifua cha wife, mabusu,kupapaswa na pole ningi ilikuwa ada, nikipumzika kidogo naambiwa maji ya kuoga tayari kaondoe uchovu nimekumis, nikishaoga nakutana na juice au maziwa fresh mezani kabla ya chakula japo na chenyewe kimeshaiva na mwenyewe kashaoga katulia. Tunakula na kulishana vizuri, tunaangalia tv na mbwembwe nyingine kibao kabla ya kwenda kitandani.

Baada ya watoto wawili sasa. Nikirudi napokelewa na watoto na kazi zao za shule, niwasimamie mmoja mmoja na kufanya nao marudio. Mama yupo jikoni ndio anapambana kupika maana tangu asubuhi alipoamka alianza na kuwaanda watoto na kuwaandalia kifungua kinywa baada ya hapo ni anafua nguo zetu watu wanne, usafi wa mazingira, amewapeleka na kuwachukua shule, amewapikia na kuwaogesha maji vuguvugu, kaenda gengeni kuhemea cha siku hiyo, kachoka hata kuoga bado.
Baada ya mimi kumaliza kuwasaidia kazi zao nikimcheki wife alivyo na harakati nyingi maji ya kuoga nijiwekea mwenyewe na baada ya hapo nakuja kutulia na watoto ili wasisinzie japo walilala mchana. Mama anatutengea chakula nakula na watoto ili wasilale na yeye anaelekea kuoga. Akija kula akiingia kitandani sekunde 59 keshalala kwa uchovu.

Yale niliyoyaeleza mwanzo yenye bashasha na mbwembwe nyingi yametoweka yenyewe automatically, sio sisi ni hali. Kuna siku nilijaribu kumlisha chakula mbele ya watoto, dah, walicheka balaa halafu yakafuata maswali kama nipo ktk interview.
Kila jambo lina mwanzo na mwisho, maisha ya kuishi kwa mazoea hayaepukiki ktk maisha ya ndoa.

Duuuhhh ni kweli ni hali ila inabidi tuseme na hali zenyewe ukizingatia muda mwengine kunakuwa hakuna suluhisho la moja kwa moja
 
Eti walicheka balaaaaa [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom