Mambo 5 yatakayowapa UKAWA ushindi katika uchaguzi 2015

Mambo 5 yatakayowapa UKAWA ushindi katika uchaguzi 2015

maaka

Senior Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
109
Reaction score
44
MAMBO 5 YANAYONIPA AMANI YA KUWAWAPA DHAMANA UKAWA FOR 2015-2020

i. Elimu
ii. Katiba mpya
iii. Usimamizi wa utawala wa sheria na uwajibikaji
iv. Ulinzi wa rasilimali hasa gesi na mafuta
v. Chachu ya vijana/ushirikishaji wa vijana
vi. Dhana ya mabadiliko/changes:

A. Elimu, Elimu, Elimu
Tushabikie kitu chenye uhalisia kwa fahari bila kuogopa, tusiwakosoe kuwa serikali yao itawezaje kuitekeleza sera hii muhimu, bali tutafakari umuhimu wake ili tuone namna ya ku support iweze kutimia

Mataifa mengi yamepata mapinduzi makubwa kiuchumi kupitia elimu, mfano UK and US elimu yao ni bure bure bure na ni elimu bora, wata compromise kwenye maeneo mengine but they dont mess up with education....kama unaona mbali utakubaliana na mimi kuwa hata Jamhiri ya Uchina, Malasia, Singapore, South Korea, Japan ni Elimu kwa vijana wao iliwekwa kuwa kipaumbele na hapo vijana hawa wakaja kuikoa nchi

2014 Marekeni walitumia $3.5trilion kwenye education ambayo ni sawa na 20% ya budget katika mwaka wa fedha

Faida za elimu
1. Huondoa ujinga
2. Huongeza ujaziri, confidence
3.Hujenga ubunifu
4.Huimarisha ushindani.

Elimu tunayoitaka:
1.Free education: Elimu bora/quality, waalimu bora, mazingira bora maslahi....tangu elimu ya awali mpaka university, tufike mahali mtu akitaka kumsomesha mwanae private schools iwe ni hiari tu ila siyo kwa sababu elimu ya Umma siyo BORA
2. COMPETITIVE EDUCATION KWA HIGHER LEARNING: ELIMU YENYE UBORA NA USHINDANI
3. Capacity and infrastuctures za kutosha ili watu wote wanaotaka kusoma wapate nafasi.
4.Maarifa ya kazi/home craft iwe ni sehemu ya lazima katika elimu
5.National service ni compusory kwa wahitimu wa form six
6.Uwekezaji katika sayansi na technology upewe kupaumbele
7. Kusomesha vijana wetu vyuo vya nje kwa wingi pale inapokuwa hakuna nyenzo hizo hapa nyumbani
8.Tafiti endelevu/vyuo vya tafiti nk

B. KATIBA MPYA:

KATIBA YA WANANCHI ITEKELEZWE KWA DHATI: RASIMU YA WARIOBA

C. RASILIMALI/GAS + MAFUTA:
1.sera nzuri ya uwekezaji, wizara pekee ya kushughulikia eneo hili
2. Ulinzi wa rasilimali zetu.

D. UTAWALA WA KISHERIA:
Sheria nzuri isiyokandamiza na inayofuatwa:

E. CHACHU YA VIJANA:
Sehemu nyingi duniani ukiona vijana wanaingia kwenye jambo ujue mapinduzi ya kweli yanaendakutokea, hili ni jambo liko hivyo kihistoria.
Inasemekana asilimia kubwa ya wapiga kura wa mwaka huu ni vijana, hili ni jambo la heri pia kwa kuwa zaidi ya 60% ya Tz ni vijana, hivyo
wakiamua wanaamua sawasawa na matakwa yanayowahusu zaidi. Jambo hili linatiwa chachu na ukweli kwamba hata wagombea waliowengi ni vijana.

F. DHANA YA MABADILIKO:
Changes are inevitable: Falsafa ya mabadiliko ilimpa OBAMA ushindi mwaka 2008: ni dhana kubwa yenye maana kubwa pia:
"Big changes in your life may be to move to a new city, state, or country, or a change in jobs. You can even try really hard to change who runs the government. In fact, that last type of change is probably one of the biggest a group of people can experience. When there is a significant disruption in a government that leads to new or modified leadership or policies, we call this type of change political change"

Kimsingi tuache ushabiki, tuhurumie vizazi vijavyo, Nigeria waliona hilo na kuamua kwa pamoja hata wanachama wa PDP wakamnyima kura rais G. Jonathan na Kumchagua Gen. Muhammadu Buhari wa APC kwa 53.96% Huku chama tawala wakiabulia 44.96% ya kura zote:

Nguvu ya umma hutumika kwa maslahi ya umma, kuziondoa tofauti zetu za kivyama na kuamua kubadilisha serikali, bila kujali upo chama gani..mambo kama haya hufanyika hata Marekani...bila kujali uchama watu huamua kupiga kura kiuzalendo zaidi

KARIBU TZ MPYA YA UKAWA:
MUNGU IBARIKI TZ
 
Lowasa! Mabadilikoooooo! Mabadiliko! Lowasaaaaaaa! Yan bana hapo na mimi amepata kura yangu. Hayo ndiyo mambo tunayoyataka watz sio porojo za ccm.
 
kwenye swala la elimu, ushiriki wa vijana, na dhana ya mabadiliko nakubaliana na wewe.. lakin ishu ya katiba mpya, kusimmia uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma nakataa. huu ni ulaghai wa mchana kweupe. huwez mkabidhi majukumu hayo kubwa la mafisadi alaf utegemee matokeo chanya.. hell no
 
Lowassa Indie Rais piga au....Tafiti zote kwa Magufuli Hazisomi Kabisa; Wapiga ramli Hazisomi, Karumanzila Anaona chenga tu name Wasoma Ngota ndio hata Helufi za Jina la Pombe..
 
maaka

Bila kusahau ajenda ya kuvifanya vivuko vyote kutoa huduma bure nchi nzoma.
Kumbuka vivuko ni madaraja yanayotembea (Locomotive bridges)
hivo sio haki raia kulipia huduma za daraja.
Hii ya kuondoa vivuko katika miradi ya uzalishaji ya serikali
na kuvifanya kuwa huduma za wananchi itaipaisha UKAWA.
 
Last edited by a moderator:
kwenye swala la elimu, ushiriki wa vijana, na dhana ya mabadiliko nakubaliana na wewe.. lakin ishu ya katiba mpya, kusimmia uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma nakataa. huu ni ulaghai wa mchana kweupe. huwez mkabidhi majukumu hayo kubwa la mafisadi alaf utegemee matokeo chanya.. hell no
Mkuu, alikuwa kubwa la Mafisadi huko alikokuwa kwa sababu ya watu waliokuwa wamemzunguka, huku atazungukwa na watu wenye uchungu na nchi, atawezaje fanya huo ufisadi peke yake ? Kumbuka kuwa Bungeni pia kutakuwa na ushindani mkubwa katika kuisimamia Serikali kama ilivyo Kenya sasa hivi, katika hali kama hiyo hakuna Waziri akayefanya mchezo tena na rasilimali za taifa, vinginevyo, atatakiwa kuachia ngazi, kitu ambacho kinajenga uwajibikaji, tofauti na hali hii iliyokuwepo ambayo Nawaziri wanakuwa Miungu watu na kutoa majibu yenye ukakasi Bungeni na kwa wananchi.
 
This is rubbish and nonsense!

mkuu, alikuwa kubwa la mafisadi huko alikokuwa kwa sababu ya watu waliokuwa wamemzunguka, huku atazungukwa na watu wenye uchungu na nchi, atawezaje fanya huo ufisadi peke yake ? Kumbuka kuwa bungeni pia kutakuwa na ushindani mkubwa katika kuisimamia serikali kama ilivyo kenya sasa hivi, katika hali kama hiyo hakuna waziri akayefanya mchezo tena na rasilimali za taifa, vinginevyo, atatakiwa kuachia ngazi, kitu ambacho kinajenga uwajibikaji, tofauti na hali hii iliyokuwepo ambayo nawaziri wanakuwa miungu watu na kutoa majibu yenye ukakasi bungeni na kwa wananchi.
 
maaka

ukawa bananeni hapo hapo...
 
Last edited by a moderator:
Hii ndo kampeni ya kunishawishi nipige kura ukawa? Thubutuuuuuuu
 
kwenye swala la elimu, ushiriki wa vijana, na dhana ya mabadiliko nakubaliana na wewe.. lakin ishu ya katiba mpya, kusimmia uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma nakataa. huu ni ulaghai wa mchana kweupe. huwez mkabidhi majukumu hayo kubwa la mafisadi alaf utegemee matokeo chanya.. hell no

nakushauri umpe kura yako Lowassa kwani hvyo ulivyovitaja akiviweza tz tutakua mbali sana achana na hao wasioeleweka.
VIVA UKAWA
 
Uloi nga mâché68;14062628 said:
This is rubbish and nonsense!
Yes, it may be. But sir/Madam from your point of view, can you elaborate what is sensible to the nation give its current situation. Mapovu ya nini badala ya kujenga hoja ? Mapovu hawezi leta maendeleo, shawishi kwa hoja na mifano.
 
Mkuu, alikuwa kubwa la Mafisadi huko alikokuwa kwa sababu ya watu waliokuwa wamemzunguka, huku atazungukwa na watu wenye uchungu na nchi, atawezaje fanya huo ufisadi peke yake ? Kumbuka kuwa Bungeni pia kutakuwa na ushindani mkubwa katika kuisimamia Serikali kama ilivyo Kenya sasa hivi, katika hali kama hiyo hakuna Waziri akayefanya mchezo tena na rasilimali za taifa, vinginevyo, atatakiwa kuachia ngazi, kitu ambacho kinajenga uwajibikaji, tofauti na hali hii iliyokuwepo ambayo Nawaziri wanakuwa Miungu watu na kutoa majibu yenye ukakasi Bungeni na kwa wananchi.
mkuu hapo utanifanya nicheke.. nani mwenye uchungu na inchi hii katika hao wanaomzunguka. mbowe, sumaye, lema, msigwa sugu.... kweli hao ndo unasema wana uchungu.... acha masihara ndugu. au tuanze kumwaga mambo yao hadharaini.. moja tu ni kwamba katika vihela vya ruzuku wanavyopewa wanapata hati chafu ya CAG Alaf unaleta story et kazungukwa na waadilifu....
 
mbowe, lema, msigwa, sugu, Mnyika, Mdee, Lisu na wengine zaidi ukijumuisha na wale wataoingia katika uchaguzi huu. Hata hivyo, Mkuu kama kweli uko fair utakuwa umegundua kuwa wanashabikia UKAWA sio kwamba wanaipenda ila wanapenda mabadiliko, hivyo, wanatapa tapa kuona nani anaweza kuyaleta. Wanaweza kuwa tayari kuchagua hata jiwe ili mradi tu kuwa wamechoka na mambo ya chama fulani.
 
Kabisaaa kabisaaa...✌✌✌✌

Sera za UKAWA ziko open, clear, understandable and can be easily IMPLEMENTED...!!!

Ndio ushindi wao...!!!

Mungu fanya maajabu, wenzetu Kenya wameweza... wako mbali sana sanaaa sasa hivi... sisi bado tuko tunapandisha twiga ndege... !!!
 
Back
Top Bottom