Mambo 12 yanayoipasua Tanzania vipande vipande kutoka utawala wa awamu ya 5

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,397
18,004
Kuna mambo mengi sana yanayo isambaratisha Tanzania kutoka utawala wa Magufuri, ila nitataja 12 tu;
1. Ni mropokaji kwa kuwa anapoongea hajali kadamnasi imayomsikia. Matusi ya nguoni ndiyo lugha yake ya kawaida.

2. Hapendi upinzani kwa kuwa akiruhusu atashindwa asubuhi. Ndiyo maana katumia hela ya Serikali kuwanunua wabunge wa Kinondoni, Siha na Bahati.

3. Anapenda rushwa na ufisadi ndiyo maana hataki kufanya kazi na CAG aliye nyooka.

4. Ni mwizi wa mali ya umma ndiyo maana kamuweka Katibu Mkuu Hazina ambaye ni mpwa wake. Kwa miaka 4 tayari Tsh 2.4 Trillion hazijulikani zilipo

5. Ni mpenda ukabila kwa kuwa sehemu nyeti zote amejaza ndugu na watu wa Kanda ya ziwa Angalia IGP, DPP, AG, KM-KM-Hazina, RC DSM, Waziri Nishati, CAG mpya, Waziri Viwanda, Jaji Mkuu nk

6. Ni mtu wa kufuja mali ya umma. Angalia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na uanzishaji wa mbuga ya Burigi -Chato

7. Amezuia shughuli za vyama vya siasa wakati CCM inafanya mkutano kila mahali. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 na Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 zinatambua shughuli za vyama vingi.

8. Hataki watu wajieleze kwa uhuru kadri ya katiba, na amevibana vyombo vya habari. Kwa mfano Eric Kabendera ameanzishiwa shitaka la kutakatisha fedha wakati kiukweli ni maoni yake kwenye gazeti la The Economist

9. Anachukia wenye vyeti feki lakini kamuacha Bashite aendelee kuwa RC DSM wakati naye ana cheti feki. Hata PhD yake yasadikiwa amekopi kwa supervisor wake ambaye kamteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo.

10. Ameruhusu kikundi cha wasiojulikana kiteke watu, kuwatesa na wengine kuwaua kama Ben Saanane, Azory Gwanda. Na majeruhi kwa Tundu Lissu

11. Analitawala Bunge kwa remote control. Bunge haiwezi kuhoji chochote kilichofanywa na Serikali.

12. Mahakama nayo iko mfukoni mwake. Yeye ni Polisi, kuendesha mashtaka na Hakimu

Tuendelee kupaza sauti kukemea uovu na unyama aliouleta huyu Mnyarwanda kwa vile anatuharibia Tanzania yetu
 
4- katibu mkuu Hazina Doto na mwezake kurwa na watoto wake wa DNA alizaa nje, tambua kuanzia leo kuwa Hazina BOT ipo chini ya mtu na Baba yake ndiyo maana wanachukua pesa mda wowote wanaotaka hata pesa za maduka ya kubadili pesa wamechukuchia wao kimya kimya. Hao watu hatari. 5- waziri wa mambo ya ndani, mkuu wa majeshi mpaka wale walinzi wake binafsi wengi ni huko huko
 
Hao wanaomoinga ndio walioiba 2.4T n kuzuia CAG asikague, ni watu wabaya sana.
Kama kulikuwa na ukweli kwa hili.
Na kwa jinsi mnavyomchukia nyinyi mafisadi,mngekywa mnasubiri nini mpaka saa hii kuupeleka kwenye vyombo husika?

Au hata kuuanika hadharani?

Mmeishiwa hoja mmebaki kuwa genge la matusi tu,kuanzia halima mdee,sugu,lema,newton,kigogo,chadema mdude na wengineo wooote.

Shame on you!
 
Moja ya uzi mfu , nawasiwasi na elimu yako ndg!

Tatizo la waafrika ni kula,kunywa,kuongea na hata kutenda kwa kufikirika,ukijifanya kana kwamba unayoyazungumza ni ya ki utopian
 
Wanasiasa ndiyo wamelifikisha taifa hapa,toka pande zote iwe chama tawala au upinzani.........wengi hawana uwezo wa kujenga hoja bali wanatumia lugha zisizo na staha kwa kutukana majukwaani.Uwezo wa kujibu hoja bila lugha ya kukera hamna,wengiwanadhani ukitukana,ukimsema mtu fulani kwa lugha fulani ndiyo unaonekana unauchungu na uzalendo.

Saizi kiongozi wa CCM mfano,akionekana na mtu wa Chadema wapo sehemu wanaongea tayari vyama vinaanza kuleta doubts na usishangae akatimuliwa,sasa wengine wamesoma pamoja,wanatoka kijiji kimoja wasiongee? Hata misiba saizi tunazikana kisiasa jambo ambalo ni hatari sana.

Mungu ibariki Tanzania
 
4- katibu mkuu Hazina Doto na mwezake kurwa na watoto wake wa DNA alizaa nje, tambua kuanzia leo kuwa Hazina BOT ipo chini ya mtu na Baba yake ndiyo maana wanachukua pesa mda wowote wanaotaka hata pesa za maduka ya kubadili pesa wamechukuchia wao kimya kimya. Hao watu hatari. 5- waziri wa mambo ya ndani, mkuu wa majeshi mpaka wale walinzi wake binafsi wengi ni huko huko
Tuendelee kupaza sauti kila Mtanzania aelewe kuwa utawala huu siyo wa wanyonge kama wanvyojinadi bali ni utawala wa kifisadi na kimafia.
 
Inasemekana Boeing 787 - Dreamliner tumepigwa zaidi ya USD 115 Milion sawa na Tsh 2.6 Bilioni
 

Attachments

  • IMG-20191108-WA0018.jpg
    IMG-20191108-WA0018.jpg
    62 KB · Views: 1
Back
Top Bottom