Mambo 10 yatakayokusaidia kulinda afya yako

Mambo 10 yatakayokusaidia kulinda afya yako

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,491
Reaction score
2,563
Karibu ujifunze.

1: Kula taratibu
Husaidia kuupa muda ubongo wako kukuambia imetosha, na hivyo inaondoa uwezekano wa kula chakula kingi zaidi kisichohitajika mwilini. Pia itakusaidia kupata fursa ya kutafakari juu ya aina ya chakula unachokula na kufanya maamzi sahii ya kiafya.

2: Pata muda wa ku socialize
katika hili si suala la idadi ya marafiki au unaonana nao mara ngapi bali kitu cha msingi ni kuweza kuwa na connection na wengine. itakusaidia kuwa na furaha, kuwa na ufanisi wa kazi, na kuimalisha afya . chukua simu yako wapigie marafiki na tengeni muda wa kwenda dinner au matembezini. siku hizi maisha yapo kiganjani socializa na agemate, school mate, wafanyakazi wenzio thru FB, whats app, Instagram etc

3: Penda kutumia juice au matunda
juice mara nyingi inakuwa na virutubisho sana kama vyote. kadhalika matunda ni chanzo kizuri cha vitamin, fibers, folic acid na pia hayana mafuta na calories nyingi. zingatia usafi unapoandaa juice au matunda.

4: Jipe likizo na mapumziko
Ndiyo-namaanisha. Acha kufanya kazi kama mtumwa. Ata roboti na mashine upumzishwa. tenga muda walikizo, nenda ukawe karibu na watu uwapendao kama familia na marafiki-ili ni zuri kwa afya yako ya akili na kisaikolojia. pata muda wa kupumzika na kulala usingizi mzuri , masaa 7 yanatosha. mapumziko yatakukinga na stress na magonjwa ya moyo. kumbuka ukianza kuw na mawazo na mipango ya kuwa belionea masaa 7 ni mengi mno kuyatumia kitandani-just balance.

5: Punguza vyakula vyenye mafuta sana na wanga
Ukifika umri wa nika 25 kwa wanawake na 35 kwa wanaume anza kuwa makini na ulaji. hata hivyo ukijenga tabia nzuri ya ulaji toka ujanani itakusaidia sana. Idadi ya watu wenye vitambi na miili mikubwa kwa wadada imekua kama fashion hasa kwa maisha ya mjini. pamoja na asili ya miili ya watu issue kubwa ni misosi tunayokula. mafuta na wanga vina calories nyingi sana ambayo ni ngumu kuzitumia kwa maisha yetu haya ya kukaa kwenye ofsi siku nzima. ni hatari kwa afya yako ya moyo na afya kwa ujumla. jizuie kula chips, buggers, vyakula vilivokaangwa kwenye mafuta mengi, chapati, vitumbua n.k

6: Kunywa maji na vinywaji
kwa walokole wenzangu mnisamehe. unywaji sahii wa vimea (alcohol) imeshathibitishwa ni afya kwa mwili wako. chupa mbili kwa mwanaume au moja kwa mwanamke kwa siku inatosha. ukiweza kupata wine itakusaidia sana kwa afya ya moyo, kupunguza stress, na ubora kwenye maisha ya unyumba. hata hivyo kwa non alcohol user-hakikisha unatumia kiasi cha maji safi yasiyo chini ya lita 3 ndani ya masaa 24.

7: Kabiliana na stress

Wote tuna stress katika maisha yetu. stress zinaharibu utulivu, mapigo ya moyo yanaenda kasi, misuli kuuma n.k usipo ikabili stress itakusababishia pressure ya juu, vidonda ya tumbo na maladhi ya moyo. hivyo, jipe muda wa kuvuta pumzi na kutoa-fanya hivyo kwa muda mrefu, fanya kitu ambacho kitakutuliza kama kusikiliza mziki, na pia jaribu kuyakubali mambo amabayo yako nje ya uwezo wako. Akiamua kuondoka mpe muda akajaribu huko njee kama kuna utofauti.....aaah I'm joking

8: Fanya mazoezi
acha kubweteka. tenga muda wa kushugulisha misuli ya mwili wako. tembea, fanya kazi za garden, kimbia, ukiona huwezi fanya mazoezi peke ako tafuta kamapani au nenda gym. mazoezi yamethibitika kuimalisha kinga ya mwili, afya ya moyo na hamu ya tendo la ndoa.

9: Cheza muziki
kwa walokole wenzangu ikifika wakati wa kipindi cha sifa na kuabudu tafadhari usibaki kwenye bench. ruka uwezavyo, shout uwezavyo, na piga steps kama unaweza. yote haya nasisitiza kuwa kucheza mziki imethibitishwa kusaidia kuimalisha afya ya mwili kwa ujumla, afya ya akili na husaidia kupunguza stress. kwani uongo? wanamziki wengi huonekana na afya njema.

10: Tendo la ndoa
Kwa wale waliopewa certificate za uhalali wa kufanya tendo la ndoa tafadhari usipuuze. iko bayana kisayansi tendo husaidia kuimalisha afya ya akili, afya ya ngozi, moyo, kuimalisha mahusiano na kusaidia kuishi maisha marefu. hivyo rafiki acha uzembe, lakini make sure to keep it safe. pima maladhi ya zinaa na UKIMWI, hepuka mimba zisizotarajiwa.

kwa leo tuishie hapo. usiache kunipa mrejesho

Production@2020
 
Back
Top Bottom