Mambo 10 katika Derby ya Leoo

DonMaster

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Messages
258
Points
250

DonMaster

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2017
258 250
Mambo 10 nilioyaona Simba Vs Yanga

Cc @ALIKAMWE

1: WHAT A GAME CLASSIC One of the best perfomance kwenye 'derby' ya Dar es Salaam. Viingilio vimeenda kihalali

2: Yanga walikua bora sana kipindi cha pili, walifanya kile ambacho timu nyingi hua zinaogopa kuwafanyia Simba. Pressing na kuwanyima utulivu wa kuwa na mpira mguuni. Ni ngumu sana kutabiri nyota wa mchezo katika kikosi cha Yanga

3: JUMA ABDUL WHAT A WARRIOR Katika mechi kubwa, ngumu, ameonyesha ukomavu na ukubwa wake. Alikua bora kwenye kukaba, lakini akawa msaada mkubwa kwenye kuisukuma timu mbele

4: Deo Kanda, akili yote ya Simba iliwekwa kwenye mikimbio yake. 'Skills' zake ziliwanyima uhuru sana mabeki wa Yanga. Anguko la kwanza la Simba lilianza alipoumia

5: BALAMA Hakuna kipa angeweza fika pale. Kumlaumu Manula ni kumkosea heshima Balama kwa kile alichokifanya. Bao bora lililowarejesha Yanga mchezoni kibabe

6: Sare ya leo ni somo tosha kwa benchi la ufundi la Simba. Timu inahitaji kua na Plan B inapotokea Plan A inafeli. Haiwezekani Simba ikawa inacheza aina moja ya mpira kwa dakika 90

7: Tairone! Yule Mbrazil ameimarika sana. Ni mabeki wachache sana wenye uwezo wa kusumbuana na Nchimbi uwanjani

8: Makame Nafikiri alikamia sana mechi, utulivu ukapotea. Yanga ikafia kwenye eneo lake. Second Half, Tshishimbi alikuja kumuonyesha jinsi kiungo wa chini anavyotakiwa kucheza kwenye mechi kubwa

9: John Bocco! 'Sub' yake angalau ilisaidia kurejesha hofu kwa mabeki wa Yanga. Alikua bora kwenye mipira ya juu, bahati mbaya akakosa sana huduma ya mipira ya aina hiyo.

10: Jonesia. Jonesia. Jonesia. Historia itakukumbuka

Nb: Hivi mchezaji wa 12 hua ni shabiki au refa
28_manula-20200104-0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ilongailunga

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Messages
1,256
Points
1,500

Ilongailunga

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2012
1,256 1,500
Huyo mama alishawahi kulikubali goli la mkono la striker wa Yanga Mburundi, Simba wakang'oa viti. Siwezi kumlaumu mechi ilikuwa kali sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mama kawabeba Yanga ila watu wasiojua mpira wanadhani Simba ndio walinufaika. Yondani alitakiwa ale umeme na itolewe adhabu ndogo nje ya box. Mama kaona Bora atoe penalty lakini Yanga wabaki 11. Kwa asiyejua sheria za mpira anajua maamuzi yameinufaisha Simba kumbe Yanga ndio mnufaika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

DonMaster

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Messages
258
Points
250

DonMaster

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2017
258 250
Tukiachaaa ushabikii,,, hasiraaa pembeni ki kweliii kajitahidi sana Jonesia kuweza kumudu game kubwaa kama ileee af ukichukuliaa ye n mwanamkee anastahili pongeziii.....
Huyo mama alishawahi kulikubali goli la mkono la striker wa Yanga Mburundi, Simba wakang'oa viti. Siwezi kumlaumu mechi ilikuwa kali sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,392,176
Members 528,565
Posts 34,100,975
Top