Mama zetu humu JF je haya Wanayotufanyia Mabinti zenu nanyi mliyafanya?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,841
2,000
Nadhani sasa itanibidi tu ama nimfunge Kizazi au nitafute tu Mwanamke Tasa ili niondokane na hizi adha au kero ninazozipata kila mara Mpenzi wangu akiwa na Mimba yangu kwani kwa aina ya maudhi yake haya yanayokuja na style yake katika kila Mimba ninayompa kuna siku Jamhuri itanifadhi katika moja ya Majengo yake kutokana na hasira nilizonazo.

Mimba ya Kwanza alinitesa mno kumtafutia Miguu ya Kuku tena usiku wa manane nikamvumilia kwakuwa niligundua ana Ujauzito wa Mtoto wa Kike ambao nilikuwa napenda sana Mwanangu wa Kwanza awe Baby Girl.

Mimba yangu ya Pili kama kawaida yake alinitesa tena huku akinitaka mara kwa mara kumtafutia Mchicha tena akisema bila uwoga kabisa kuwa anapenda Mchicha ule wa Mto Msimbazi na nikajaribu kumkatalia katakata kuwa si mzuri kwa Afya ya Mtoto wetu yeye akakomaa tu kuwa anautaka huo huo na hivi Mtoto aliyekuwa tumboni mwake alikuwa ni wa Kiume hivyo alitaka kuanza kumkomaza mapema tokea tumboni ili akizaliwa awe Jasiri na Mvumilivu wa shida / taabu.

Sasa ni hivi majuzi tu nimegundua kuwa Mpenzi wangu ana Ujauzito tena wa mwezi mmoja sasa lakini kwa masikitiko makubwa mno style aliyokuja nayo sasa Mpenzi wangu nadhani muda si mrefu nitakuwa Chakula cha Jamhuri Kolokoroni kwani nahisi ananifanyia makusudi au ana uwendawazimu.

Sasa hivi kila tukilala tu ikifika Saa 8 usiku lazima niamshwe na ananilazimisha tutizame SKYNEWS taarifa ya Habari hadi Saa 9 na ikifika Saa 9 tena ananilazimisha nichukue Kitabu cha Pambio na anaanza kuniimbisha nyimbo za Kusifu kiasi kwamba sipati muda mzuri wa kulala na nabaki tu kusinzia kila siku ndani ya Madaladala na Ofisini kitu ambacho kiukweli kinanikera na najijua mwenyewe huyu Mwanamke ana muda mfupi tu atachezea Kichapo changu halafu nilaumiwe.

Najua humu JF kuna Mama zetu hivyo naomba kuwauliza na Wao je hizi Kero tunazozipata sasa kutoka kwa Mabinti zao na Wao enzi zao walikuwa wakiwafanyia Baba zetu? Na je ni hali yao tu ya Kimazingira au wanatufanyia tu kusudi?

Kutokana kwamba sasa sipati muda mrefu wa kulala hata macho yangu yamebadilika rangi na yamekuwa Mekundu mno na wiki ijayo nina Safari ya Kikazi ya kwenda Mkoani Shinyanga ambako nasikia kuwa huko ukionekana una macho mekundu automatically Wewe ni Mchawi na Kuuliwa ni jambo la kawaida sana hivyo najishauri kwenda au kuichomolea tu hiyo Safari.

Mama zangu wa JF humu nayasubiri majibu yenu tafadhali kwani kiukweli nimechoka!
 
Bukwabi

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
3,281
2,000
Ndio Unapata experience. Jaribu mpaka watoto saba hivibhutawauliza kina mama tena.
 
niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
6,555

Hii ni kati ya Theses zako za Phd. au ndo unaanza kuandika short stories book? Mimi kama mama/ bibi nakujua story zako kuanzia binti kuvunja ungo ukiwa single mpaka nyingine kibao na leo unakuja na huyu mpenzi kuwa na mtoto wa tatu? Kuna watu wakisoma wanapita tu ila kuna sisi wengine tunarecord kila story tunayoisoma na kucomment.
 
Mkushi Da Gama

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
3,716
2,000
Hii ni kati ya Theses zako za Phd. au ndo unaanza kuandika short stories book? Mimi kama mama/ bibi nakujua story zako kuanzia binti kuvunja ungo ukiwa single mpaka nyingine kibao na leo unakuja na huyu mpenzi kuwa na mtoto wa tatu? Kuna watu wakisoma wanapita tu ila kuna sisi wengine tunarecord kila story tunayoisoma na kucomment.
Tupo wa chache sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom