Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 227
- 246
Anaandika: Mohamed Ismail Rwabukoba
Mbona hasemi, mbona haongei au wanataka tuamini huo nao ni ukorofi? La hasha huo siyo ukorofi bali samaki ana mengi ya kuzungumza ila akifungua kinywa chake itabaki ni historia. Ilishasemwa ya Ngoswe tumuachie Ngoswe mwenyewe.
Mama anaupiga mwingi ni maneno machache ambayo yamekuwa maarufu sana tangu alipoapishwa kuwa Rais wetu. Naam! Mlimwengu mimi naafiki kabisa kwamba mama anaupiga mwingi. Rais Samia siyo kwamba ni Rais bora kuliko wote ila ndio Rais bora kwa sasa ambaye alitakiwa katika kipindi hiki. Tuvushe mama, tuvushe Rais wetu, sisi ni wanao usisikilize kelele zetu, tumeamua tu kulalamika kwa sababu tunajua mama yetu ana upendo na hapendi kuona watoto wake wakiwa na sononeko la moyo. Mama unaupiga mwingi mimi nitasema hivyo kutokana na kusikia na kuona kwa macho yangu ambayo umeyafanya kwa kipindi kifupi tangu uanze kupeperusha kijiti cha Urais.
Ni nadra sana kupata bahati kama tuliyo nayo ya kutoka kuondokewa na mtu mliyemuamini sana halafu anatokea mtu ambaye anakuja kuwafuta machozi. Ni wewe umetufuta machozi .Rais Samia uliposema kazi iendelee kilikuwa ni kitendawili kwenye ngoma za masikio ya waliowengi. Lakini sasa macho yamekuja kuthibitisha kile kilichosikika kwenye masikio yao. Tunaona miradi yote ya kimkakati iliyoanzishwa ikiendelea. Achana na porojo za mtaa wa pili, wao kusema na kulalamika ni desturi yao. Kiu ya wenye kutaka mema na nchi yao ni kuona ujenzi wa SGR ukiendelea, kuona site ya bwawa la Mwl Nyerere kazi inaendelea, kuona vituo vya afya vijijini vikijengwa, huku kwetu Muleba tukiona shule zikiboreshwa. Na huko kwa watani wangu wakiona huduma za kijamii kwao zinazidi kuimarishwa ndio furaha yao.
Kikwetu asiyeshukuru siyo uungwana. Mama unaposema kwamba diplomasia ya kiuchumi inaimarishwa wanajifanya hawaelewi. Ni muda mfupi sana tangu uingie madarakani lakini tayari tumeishaaminika kwa taasisi nyingi za kifedha pamoja na mataifa mengi. Juzi tu tumepata Tirioni 1.3 hata yule ndugu yangu wa Kabuku huko Handeni kaniambia hiyo hela anaona inavyoboresha miundombinu ya kwao. Achana na njomba wangu wa Mtwara ananiambia zile safari za kufuata kituo cha afya umbali mrefu itabaki stori maana kinapojengwa ni kinywa na pua.
Ukienda ughaibuni tunajua ni kuboresha mahusiano yenye kuleta tija katika taifa letu. Wao wanaamini unaenda kupiga picha. Unaifanya dunia kuwa kijiji leo mnakaa pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza mnajadili namna ya kuwasaidia watu wa Katavi, kesho upo na Biden mnajadili namna ya kuwasadia ndugu zangu wa mwisho wa reli. Huu ndio uwakilishi jengeshi. Hizo picha zitabaki kumbukumbu kwa vizazi na vizazi kwamba huyu ndio Mwanamke wa kwanza aliyejifunga kibwebwe huku kichwani kafungia shungi lake linalomeremeta na kiunoni kafunga mkwiji ambao ulitumika kutuletea chakula kutoka mahangaikoni.
Mlimwengu mimi nina mengi ya kusema kuhusu Rais wangu. Kichwa changu kimesheheni kurasa nyingi zilizopambwa na maandishi yanayoelezea nia yako ya dhati ya kuhakikisha taifa letu linasonga mbele. Naomba nitamatishe hapa kwa kurejea salamu yenye sauti yako ya upole na mamlaka ndani yake....
KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
#mlimwengumimi
#RaiswetuMamayetu