Mama yangu huyu naona anavuka mipaka, dizaini anataka kujimilikisha nyumba niliomwambia akae for free

Ni kweli kulea mtoto ambaye mwingine alikunya ni kazi sana..... Tena ni kazi hasa.... Ww mjengee sehemu nyingine mpe hati miliki afanyie chochote...... Ila marufuku kumwambie ahame hapo alipo..... Atakaa hapo mpaka afe.... Kule uliko mjengea mwambie hata apangishe apate pesa.... Kama ni sehemu ya kibiashara muombe ufanye tu kwenye hayo maeneo..... Sio lazima yy ahame.

Ww mwenyewe ndio uliingia chaka bovu... Ww mamaako mwenye mchango mkubwa kwenye malezi yako, unampaje sehemu ambayo baadae utaitaka bila notification ya kumpa nyumba yake huko mbeleni? Tena unashangaza kujijengea majumba bila ya kumridhisha mlezi wako kwanza. Utakuja ulogwe next time, tena nenda haraka umweke sawa psychologically, umpe ahadi kibao atulie... Kwakuwa ni mwanamke atapoa mapema na atajuA unamtetemekea
Sahihi
 
Umefanya makosa kuto kumtaarufu kabla,masikini ya mungu labda alijua kuwa hiyo ndio zawadi yake toka kwake.Sasa ghafla anastushwa na ujio wa mafundi bila taarifa.Lazima apaniki
 
Umefanya makosa kuto kumtaarufu kabla,masikini ya mungu labda alijua kuwa hiyo ndio zawadi yake toka kwake.Sasa ghafla anastushwa na ujio wa mafundi bila taarifa.Lazima apaniki
Nilimjulisha kabla mafundi hawajaanza ujenzi...pia kuhusu kumilikisha anafahamu wazi sijafanya hvy maana katika hilo eneo haipo nyumba moja hivyo mpangaji alipotoka nikamwambie akakae nimpunguzie mzigo wa kodi lakini sikumpa kuwa yake
 
kwa type ya huyo mama ulitakiwa umlipie Kodi sehemu nyingine na sio kukaa free kwako. KuombA radhi kwake haipingiki lakini utakua umekaribisha Mambo Fulani ndio mwanzo was kukupelekesha Kila kitu ufanye Kama anavyotaka yeye. Uamuz wwt utakaofanya cheza na akili yake
 
Umekosea sana ,Fanya halaka umpigie simu ama uende kwake umuombe msamaha mzazi wako kumtoa hasila.

Kumbuka aliye kulea ndio mzazi wako, na kuzaa siyo kazi kazi ni kulea.
 
Nina mpango wa kumjengea somewhere nimepanga iwe kama suprise kama shukrani kwangu siku ya ndoa yangu. Kwa pale siwezi kumpa aisee ni eneo zuri kibiashara
Atakupiga kipande huyo,chunga sana
 
Ukisoma maelezo yangu vizuri...ni kwamba simtozi hata mm na namsaidi vilevile. Kuhusu kumjengea kuna sehemu nimenunua..naanza ujenzi January mpk mwezi wa sita namkabidhi nyumba yake, ila nataka iwe surprise

Kwasababu umeshakutana na changamoto hiyo mimi ningeshauri ustopishe kwingine kote uanze tu na kwake as soon as possible... jishushe muombe radhi ila na wewe pambana uanze kumjengea pasipo yeye kujua na hapo anapokaa stopisha kwanza ujenzi wowote. Ukishamuhamishia kwake then go ahead na hapo kwako. Naamini utakua na uhuru zaidi na eneo lako kama na yeye yupo kwake- Jan si kesho kutwa tu anza tu leo
 
Uyo mama ilipaswa umpangishie kwengine yani uwe unamlipia kodi huku ukiendelea na ujenzi wa nyumba yake, so jitaid umalize kibanda chake umuamishe hapo by ze way uyo mama anaonekana ni mtata sana uko mbeleni anaweza akajimilikisha ilo eneo akasema lake
 
Dah...nitakuwa sijatimiza lengo ingawa anafurah....ila kwa tabia yake nikimuonesha tu...nitakuwa najenga underpresha maana namjua hanaga jambo dogo mashoga zake wote atawapeleka akawaoneshe...anapojenga. Nitaulizwa kila siku nimefikia wapi, hao mafundi uko site hakuna rangi wataacha ona, watakavyokuwa wanabadilishiwa michoro....ila NDIO MAMA,
Ni kama vile unamzungumzia mama yangu mdogo?
Ana mtoto/watoto aliyezaa au hana?
 
Kitu ulichokosea kabla ya kutuma mafundi ungempa taarifa kiubinadamu kuheshimu uwepo wake pale. It doesn’t cost you anything angeona ameshirikishwa indirectly though hana mamlaka yeyote. Maana mwisho wa siku hata ikitokea dharura bado mafundi hao hao watahitaji msaada wake ama na ulinzi wa site yenyewe.
 
kwa type ya huyo mama ulitakiwa umlipie Kodi sehemu nyingine na sio kukaa free kwako. KuombA radhi kwake haipingiki lakini utakua umekaribisha Mambo Fulani ndio mwanzo was kukupelekesha Kila kitu ufanye Kama anavyotaka yeye. Uamuz wwt utakaofanya cheza na akili yake
Umeongea point kubwa sana mkuu
 
Umemjibu vibaya mama aliyekulea kipindi umefiwa na mama ako? Pengine alikuchukua ukiwa huna hata akili nzuri, sasahivi una akili na unaweza kujitafutia yote ni sababu ya malezi yake. Huyo mama hata awe mbaya kiasi gani kwa kutaka kuchukua nyumbani nakusihi urudi nyuma kumbuka wema wake. Kumbuka mazuri yake, mpigie simu muombe msamaha. Kama huwa unakunywa pombe singizia hata pombe, umefanya kosa kubwa mno. Kwasasa sichangii lolote kuhusu hiyo nyumba yako, umenikera sana kumjibu ovyo mama yako mlezi.
 
Sioni kosa hapo isipokuwa bi mkubwa itabidi umzoee tu!.. wazo lako ni zuri ila usije mnyima hata tu chenchi chenchi ndo atazidi zaidi kuteta si unajua wanawake Tena!
Ichukulie hiyo hali in a positive way.. take it as a spirit for you to fight hard until you make it.. uzuri ushajua nani anaweza simamia pesa vyema.
na akishika hela nzuri atashangaa mama atavyompamba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom