Mama yangu huyu naona anavuka mipaka, dizaini anataka kujimilikisha nyumba niliomwambia akae for free

puker

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
464
1,000
Habar za muda huu wana JF.

Kuna mambo kwenye maisha yanatokea yanatatiza kwa namna fulani mpaka unashindwa kuelewa usimame au ukae.

Iko hivi, kuna mama yetu mdogo alietulea baada ya mama yetu kufariki. Mzee alishafariki kitambo kidogo.

Tulikuwa wadogo, kwa nafasi yake siwezi kumdharau hata kidogo kwangu ni mama.

Sasa katika pilika za maisha nikafanikiwa kujenga kakibanda kangu cha wapangaji somewhere, huyu M/mdogo aliwahigi kuolewa, lakini kwa mapenzi ya Mungu waliachana na mumewe.

Sasa nikaona siwezi kuona mama yangu anaishi nyumba za kupanga wakati mimi nina nyumba zaidi ya moja hivyo nikamwambia akakae kwenye moja ya apartment ya sehemu nilipojenga.

Changamoto, inakuja kwamba mama yangu huyu naona anavuka mipaka dizaini kama anataka kujimilikisha nyumba niliomwambia akae for free.

Leo nimewatuma mafundi wakafanye vipimo na kuanza kuchimba msingi, jambo lililonishangaza amewazuia na kuwahoji maswali kibao kana kwamba yeye ndio mmiliki. Mafundi wakanipigia, nikamuelewesha nini malengo yangu, Chakushangaza ananiambia huwezi fanya chochote hapa bila idhini yangu, kiukweli kama binadamu nilikasirika sana na sijawahi mvunjia heshima hata kwa bahati mbaya, nimejikuta naongea maneno ambayo sio mazuri.

Hivi ninavyoandika hapa ameanza kupigia simu ndugu analia anasema nimemtukana na kumdhalilisha kisa yupo kwangu.

My point ilikuwa ni kumuonesha mipaka anayotakiwa kuwa nayo yeye kama mama, angekuja kama mshauri wala tusingefika huko.

Ila kiukweli sijamtukana ila nilikuwa naongea kwa jazba. Hivi kiuhalisia kuna jambo nimekosea, nisije kosa radhi maana kwa umri alioanza kutulea ni mama yangu kabisa.

Naombeni busara zenu katika hili. Natanguliza shukrani
 
puker

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
464
1,000
Omba radhi, hiyo surprise isiwe surprise tena. Mpeleke mwambie mama hapa ndio nakujengea nyumba yako.
Dah...nitakuwa sijatimiza lengo ingawa anafurah....ila kwa tabia yake nikimuonesha tu...nitakuwa najenga underpresha maana namjua hanaga jambo dogo mashoga zake wote atawapeleka akawaoneshe...anapojenga. Nitaulizwa kila siku nimefikia wapi, hao mafundi uko site hakuna rangi wataacha ona, watakavyokuwa wanabadilishiwa michoro....ila NDIO MAMA,
 
troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
15,401
2,000

Ukweli ni kuwa una makosa, hata kama ingekuwa umeipangisha si busara kupeleka tu watu wakafanye shughuli yeyote bila kumtaarifu anayeishi pale. Maana yake kesho wakija watu wenye lengo baya eti awaache kisa si pake hapamuhusu.
Kaombe radhi.
 
Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
972
1,000
Kwa historia ya huyo mama (kama ulivyo eleza)
Na kwa uwezo Mungu alio kujalia, ungechagua yafuatayo
1. Tafuta mahala, Mjengee kanyumba kake mkabidhi; mf: bedroom mbili, choo jiko na bafu
2. Tengeneza Nyumba yako ila muache aishi hapo na usimtoze kodi kwa maisha yake yote.
Nyongeza:
Kwa huo mchango wake kwa mafanikio yako/yenu; anastahili kabisa kumilikishwa nyumba yake wala sio kupangishwa;
Kumbuka, Mungu amekupa uwezo wa pesa na mali ili uwasaidie na wengine; kama huwezi kumsitiri mama yako utamsitiri nani?
 
Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,491
2,000
Nina mpango wa kumjengea somewhere nimepanga iwe kama suprise kama shukrani kwangu siku ya ndoa yangu. Kwa pale siwezi kumpa aisee ni eneo zuri kibiashara
muombe radhi umweleze isiwe suprise tena
 
Ukisoma maelezo yangu vizuri...ni kwamba simtozi hata mm na namsaidi vilevile. Kuhusu kumjengea kuna sehemu nimenunua..naanza ujenzi January mpk mwezi wa sita namkabidhi nyumba yake, ila nataka iwe surprise
 
MBEGU YA BINADAMU

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
220
250
Kama una nyumba zaidi ya nyumba moja na hiyo nyumba kaishi kwa mda mrefu, isitoshe yy ndiye kakuwezesha kufika hapo ulipo, kwa ushauri wangu mwachie hiyo nyumba tena mwambie kuwa ni nyumba yake hata Mungu akimchua warithi watoto wake.

Nasema hivyo nikiwa na maana moja kubwa. Kina mama ni watu wenye roho ndogo sana. Usishangae anakufanyia ubaya ambao hutausahau maishani mwako. Hata kama hana uchawi mwanamke yu tayari kuununua ili atimize malengo yake. Kwani yeye anajua hiyo nyumba umempa kama shukrani pamoja na kwamba hukwambia hivyo.
 
sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
3,631
2,000
Pole mkuu , muombe msamaha , Ila ni vyema kabla ya hao mafundi kwenda ungemjulisha kua kuna kitu wataka kufanya hapo nyumbani , ili akae akijua kua siku fulani kuna mafundi watakuja hapa na kufanya kitu Fulani ,

Taarifa ni muhimu hata Kama sio kwake
 
CRYPT

Senior Member
Jan 26, 2014
145
500
Mkuu kama ungewasiliana nae kabla ya kupeleka mafundi sidhani kama mngefika hapo.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
103,120
2,000
Kamuombe radhi usiongee chochote kuhusu nyumba hiyo anayoishi na hiyo uliyopanga kumpa kama surprise siku ya ndoa yako.
Nina mpango wa kumjengea somewhere nimepanga iwe kama suprise kama shukrani kwangu siku ya ndoa yangu. Kwa pale siwezi kumpa aisee ni eneo zuri kibiashara
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom