Umtama Mula
Member
- Jan 11, 2021
- 83
- 201
- Thread starter
- #221
Mkuu Mungu atusaidie Sana. Ni hatari Sana. Ni changamoto. Inafika point unachukua Likizo unatamani uende home ukutane na washkaji, marafiki wa utotoni na ufurahie zile flashback za street na Wana. Lakini ukiwaza unaona unaenda kutafuta maumivu unaamua kutafuta machimbo mengine!
Ndugu @ummtama mula, kwanza nikupe POLE kaka, kwa haya mazito uliyoyabeba moyoni kwa kipindi chote hiko.
Na la pili, NIKUPONGEZE kwa ujasiri huu uliokuwa nao, uliokupelekea wewe kufika hatua ya kuja hapa jukwaani na kufunguka hayo mazito uliyoyabeba moyoni kwa muda mrefu. Kwanini nasema huo ni "ujasiri", kwasababu UKWELI ni kwamba aina hiyo ya changamoto ya mzazi tena wa kike, imekumba vijana wengi sana katika jamii zetu hizi za kiafrika. Lakini 85% ya vijana hao wamebaki wakilia na kusononeka kwa uchungu vyumbani kwao, huku wakishindwa hata kutoka nje na kuongea kwa uwazi yanayowasibu, ili waweze kusaidiwa. Na hii yote imetokana na kasumba iliyopo kwenye jamii zetu, kuona wazazi hasa wa kike ni WATAKATIFU SANA, hivyo kijana chochote atakachokieleza juu ya *****, ataishia kuenekana yeye ndio mpumbavu na wengine watafika mbali zaidi na kumuona kama kalaanika! Wahanga wa hii psychological torture ni wengi sana.
Ila la tatu, naomba nikupe ASANTE kubwa kama ilivyo hapo, maana umenigusa au kunisemea moja kwa moja, ingawa tunatofautiana kwa kiasi fulani.
Kiukweli nami pia nina changamoto kama yako ya mzazi, tena afadhali wewe unaye baba, dada na bibi wa kukufariji.
Mwenzio hapa nilipo faraja yangu ni mke wangu tu. Maana baba, bibi na babu walishatanguliaga mbele za haki over ten years ago, wadogo zangu nao ndio tumesha sambaratishwa kila mmoja kona yake (hakuna maelewano) na ndugu nao ndio hawashikiki. Yaani taflani tupu....
Ila yote na yote, maisha lazima yaendelee kaka. Kikubwa ni kumuomba Mungu atufanyie wepesi, huku tukizidi kupambana na harakati zetu za kimaisha, ingawa mioyo inavuja damu. Kama kuna siku kutatokea mabadiliko, basi tutashukuru kwa hilo.
Ila kwa upande wako, kama asilimia kubwa ya wadau walivyokushauri humu, kwamba wewe jitoe kwa anayehitaji mkono wako. Nami nakazia hapo hapo, haya masuala mengine..... jitaidi kuyaweka kando, kumbuka TUNAISHI MARA MOJA TU.
Tchao