Mama yake Zitto avamiwa

Mama yake Zitto avamiwa

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Mama mzazi wa Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, amenusurika kutekwa. Waliomvamia wamemtishia kumuua huku wakimtaka awape laptop,simu na mawasiliano yake mengine...

Habari zaidi magazeti ya leo.

=========
*Anusurika kuuawa kwa bastola nyumbani kwake
*Wauaji wamdai laptop, flash na simu yake ya kiganjani
*Amtambua mmoja, adai ni kada wa Chadema


SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakiwa na silaha za moto.

Habari zilizolifikia MTANZANIA Jumatano kutoka kwa watu walio karibu na mama huyo zilieleza kuwa, vijana hao walifanikiwa kumfikia akiwa katika sebule ya nyumbani kwake na kumuelekezea bastola kichwani, huku wakimlazimisha awakabidhi baadhi ya vifaa vyake vya kufanyia kazi na simu yake ya kiganjani.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, tukio hilo lilitokea Ijumaa ya Aprili 19, majira ya saa moja na nusu asubuhi.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tukio hilo, mama yake Zitto alisema ni kweli lilitokea na amekwisharipoti katika kituo cha Polisi cha Buguruni.

Mama Zitto alisema siku kadhaa kabla ya tukio hilo alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa mwanachama wa Chadema wa Tawi la Tabata Relini na kumuomba msaada wa mifuko miwili ya saruji kwa ajili ya kukarabati jengo la ofisi yao.

Alisema alikubali kuwasaidia vijana hao kwa kuwataka wafike nyumbani kwake mapema siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, kwa sababu alikuwa na ratiba ngumu na ndefu siku hiyo.

"Nilikubaliana nao hivyo, bila kuwa na fikra kwamba wanaweza kuwa watu wabaya, hivyo walipokuja nyumbani kwangu baada ya kuruhusiwa na mlinzi niliwakaribisha ndani na kuwaeleza kuwa nitawapatia Sh 20,000 na Sh10,000 waongeze wenyewe.

"Lakini niliposimama kuelekea chumbani kuwachukulia kiasi hicho cha fedha, mmoja wao alitoa bastola na kunielekezea kichwani huku akieleza kuwa hawana shida na pesa, bali wanataka laptop yangu, flash na simu yangu ya mkononi kwa sababu zina mambo muhimu," alisema mama Zitto.

Alieleza zaidi kuwa alipowauliza ni kwa nini wanataka vitu vyake hivyo, walieleza kuwa anajua sababu na hata siri yake ya kutumia nafasi yake ya uongozi wa chama cha walemavu kuzunguka nchi nzima akimnadi mwanaye Zitto kwa wana Chadema kuwa anafaa kuwa mwenyekiti wa chama hicho na rais wa Tanzania inafahamika.

"Nilijua kuwa ninakufa, sikuona haja ya kubishana nao sana, nikamwita dereva wangu, Mtana, alete simu yangu niliyokuwa nikiichaji chumbani na flash ili niwapatie, wakati akielekea kuvichukua aliwaona walivyokuwa wameniwekea bastola, akakimbia moja kwa moja chumbani akajifungia na kuanza kupiga kelele, wakatoka haraka wakakimbia," alisema.

Alipoulizwa iwapo hawakupata upinzani wowote kutoka kwa mlinzi aliyekuwa getini au majirani walishtushwa na kelele za dereva wake, alisema wakati wanatoka geti lilikuwa wazi na mlinzi alikuwa akiosha gari nje, hivyo ilikuwa rahisi kutoka na gari lao na kutokomea.

Alisema anaweza kuwatambua watu hao akiwaona na kwamba mmoja wao si mgeni machoni mwake, kwa sababu aliwahi kumuona mkoani Tanga katika moja shughuli za chama hicho.

Mama Zitto alieleza zaidi kuwa kabla ya tukio hilo, amekuwa akiulizwa na baadhi ya wafuasi wa chama na hata watu wengine mahali anakopata fedha za kuzunguka mikoani kumnadi mwanaye, Zitto kwa ajili ya kugombea urais na uenyekiti wa chama.

Alisema kwa sababu ya kuhofia maswali ambayo amekuwa akiulizwa mara kwa mara, alimfikishia taarifa Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Ahmed Sagula, lakini katika hatua ambayo hakuitegemea, naye alimhoji mahali anakopata fedha za kuzunguka mikoani kumnadi Zitto, kabla ya kumuahidi kushughulikia malalamiko yake.

Sagula mwenyewe hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake kutopatikana kila ilipopigwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, naye hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni, mahali ambako Mama Zitto ameripoti tukio hilo naye hakuweza kupatikana.

Chanzo: Mtanzania

Zitto said:
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba

"Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.

Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa.

Ushauri- tuwe makini na "Agente provocatuers" au in English "provocation agents" nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata"

Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Chamviga,

Tangu nimekuwa mwanachama wa JF au mtandao mwingine wowote daima nimeingia kwa jina langu kamili Dr.W.Slaa. Ni kwa kuwa naamini kutumia jina bandia ni dalili ya uwoga. Yeyote mwenye anaweza kupima ninachoamini kwa kuonyesha identity yangu halisi. Hata hivyo, si vema kuvumilia upotoshwaji na udanganyifu wenye hila mbaya.

1) Leo niliposoma Gazeti la Mtanzania kwa nafasi yangu ya Katibu Mkuu nilimpigia simu Mama Zitto, kwanza kumpa pole na pili kujua hasa yaliyomsibu. Aliyoniambia mama Zitto yanapingana na yote yaliyoandikwa humo, mengine yakidhaniwa yamesemwa na mama Zitto, na mengine yakiandikwa na wachangiaji kwa hisia kali. Ni hatari sana taifa kuachia watu wakifanya utani na mambo yanayohusu maisha ya binadamu. Tutakuwa sio Taifa serious, linalogeuza kila kitu kuwa utani au ushabiki tu! Labda Mama Zitto akiniambia kuwa alinidanganya, na sioni ni kwanini anidanganye!

2) Nataka niweke wazi, mama Zitto hakuzungungumza nami, na wala kwa wakati wowote, sikumwambia amwone Hemedi Sabula. Yeye aliniambia amenitafuta, akanikosa, akamtafuta Sabula akamkosa. Hatimaye alimpata kwa simu ya Tendwa, afisa Ugavi, Makao Makuu. Pili, nimeongea na Mwenyekiti Mbowe, naye amenithibitishia hakuongea na Mama Zitto. Kauli hiyo inalingana na aliyoniambia Mama Zitto kuwa hakuwa amemjulisha Mwenyekiti Taifa. Ni dhahiri kauli zilizoandikwa kwenye mtandao huu zina malengo ambayo ni ya makusudi, na muda si mrefu tutayajua yote, lakini kwa vyovyote, dalili za awali zinaonyesha hazina nia njema na Chadema na viongozi wake.

3) Nimeongea na Afisa wangu Sabula kinachozungumzwa hapa ni kinyume kabisa na alichozungumza na Mama Zitto, na nimethibitisha hayo kwa Mama Zitto Mwenyewe.

4) Nimewasiliana na viongozi wangu wa Jimbo na Kata, kuhusiana na kijiwe chochote kinachojengwa. Taarifa sahihi ni kuwa hakuna kijiwe chochote kinachojengwa na kilichoombewa fedha kwa Mama Zitto. Ila kuna Ofisi ya Kata inakarabatiwa ndiyo iliyoombewa fedha, na wahusika walifika kwa mama Zitto na wakapewa fedha 30,000. Sitaki kuingilia uchunguzi wa Polisi, ninataka tu kuwasaidia walioingia kwenye Mtandao wengi wao kwa ID bandia na kutoa kauli nzito juu ya mambo wasioyoyafahamu na kutoa uhukumu.

Nimetoa taarifa hii kwa wote wanaotaka kujadili kwa nia njema, na sijatoa taarifa kwa mujibu wa majukumu na nafasi yangu kwa kuwa wanaozungumzwa wote ni viongozi ninaowahudumia kwa mujibu wa Katiba ya Chadema. Aidha, ni jukumu langu kulinda jina la Chadema pale ninapoona inataka kuchafuliwa bila msingi, wala utafiti wowote. Mengine nitaendelea kuwajulisha au kuyaweka hadharani kwa kaduri yatakavyokuwa lazima. Naamini kwa wale wenye nia njema haya yatawasaidia kujadili kwa Tija thread hii.
 
GAzeti la Mtanzania linaripoti Mama mzazi wa zitto kabwe amevamiwa na majambazi.
Walikuwa wanataka computer na kiwekea kumbukumbu flash.
Kada wa CHADEMA atajwa kutambuliwa na mama huyo.Alikuwa miongoni wa majambazi waliomvamia.
 
Hao ni vibaka wa kawaida tu. Haina uhusiano na kazi za kamanda zitto.

 
Mama wa watu ni mlemavu maskini mbona wanakuwa hivyoo ?

Zitto kama kawaa rekebisha ile issue asibaki hata panya nyumbani kwa hawa watekaji, daaadeki !
 
Mtanzania na propaganda wamesema mama yake Zitto alimwona kada wa chadema na anamfahamu yale yale ya baba yake Mtela Mwampamba, mtu amuonye tu Shida binti Salum ana heshima kwenye jamii asijiingize kwenye propaganda za kusaidia usaliti wa mwanane wa masalia, mama tulia kula vya mwanao pole pole dhambi ya uongo ni mauti , sasa hili dili litakufa kama lilivyokufa la video, pole mama habari ya leo ni liwale
 
Sasa mama wa zito ana nini mpaka atake kufanyiwa unyama kwanza huyu mama si mlemavu,huyu ni malando pasipo shaka make yeye ndiye kapewa jukum la kumchafua zito.
 
Source Mtanzania??? hahahaaaa hahaaaha. niyale yale ya Zito kutaka kuwekewa sumu. Waambie wa rudi studio hiyo single bado
 
Tunatumaini Zitto atakuja ku-clarify hii taarifa hapa.
 
Mama mzazi wa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, amenusurika kutekwa. Waliomvamia wamemtishia kumuua huku wakimtaka awape laptop,simu na mawasiliano yake mengine...

Habari zaidi magazeti ya leo.
Mkuu haya mambo yanakuweje mbona zito anaandamwa sana cdm anasubili nini huko,asije kuwa na mzee wa sumu naye alikwepo
 
Hapa JF ndipo mahala pake wakuu mlio na taarifa zaid kuhusu hili hasa mliokigoma mtujuze zaid tafadhali.
 
Hii haina tofauti na kusema Mama Zitto avamiwa amtambua mmoja wao ni muumini mwenzake wa Kanisa la Yesu mfalme! Tungeshtuka?

msianze kuleta tararira hapa!
 
Acha uchochezi wako.Hata kama zito ndo kakuhonga ili uchafue chadema ni sawa na kinyesi cha mtoto kwa mama yake
 
MAELEZO YA MAMA ZITTO
Mama Shida alikwenda kuripoti tukio la kuvamiwa kwake katika kituo cha polisi cha tabata na kufunguliwa jalada na. TAB/RB/2898/CCY/13 lakini aliambiwa kuwa tukio hilo ni kubwa kwa hiyo akaripoti kituo cha polisi cha Buguruni ambacho ni kikubwa. Alikwenda kuripoti kituo cha buguruni na kufunguliwa jalada no.BUG/RB/5153 LA KOSA LA KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA.

Baada ya kutoka hapo polisi , Shida alimpigia simu katibu mkuu wa CHADEMA DR. WILIBROD SLAA na kumueleza juu ya tukio hilo, DR Slaa alimwambia kwamba aende kuripoti katika ofisi yao ya ulinzi na usalama makao makuu ya CHADEMA. Alipoenda ofisi ya ulinzi na usalama alimkuta Naibu mkurugenzi wa ulinzi na usalama aitwaye AHMED SABULA ambaye alimwambia Shida kwamba, wamepata habari juu ya tukio hilo na pia wanazo habari za yeye kupita mikoani kumnadi mwane Zitto Kabwe ili apate uenyekiti wa CHADEMA. Maneno hayo yalimkatisha tamaa, Akaamua kuondoka, lakini alipofika njiani alipigiwa simu na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alimfokea kwanini alikwenda kueleza tukio la kuvamiwa na vijana hapo makao makuu ya CHADEMA. Mama SHIDA shida alikosa la kusema na hatimaye akaanza kuamini kuwa vijana wale walitumwa na Mbowe ili kumtisha au kumdhuru.

MAMA ZITTO amesema kuwa alipokuwa mwanza, hotelini aliwahi pia kuvamiwa na vijana wawili wa kiume ambao walijifanya wamepotea chumba.
 
Back
Top Bottom