Mama yake ameshafariki ndugu wanamsubiri ajenge choo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Rafiki yangu ni mtoto wa pekee kwa mama yake. Mama yake ni mwenyeji wa Mtwara. Alikua mfanyabiashara na mzigo aliufuata Kariakoo. Katika mahangaiko ya kukusanya mzigo alikutana na mfanyabiashara kutoka Kaskazini. Walianza mahusiano kwakua mama alikua single.

Mzee alikua na familia yake na mama alishagonga 50. Baada ya muda mama akawa anasumbuliwa na afya, ndipo alipogundulika na uja uzito. Alimshukuru Mungu alilea mimba na kujifungua mtoto wa kiume huko kwao Mtwara.

Yule mzee kutoka Kaskazini alipofahamishwa ujauzito alisubiri mpaka mtoto anazaliwa. Kufika Mtwara alijiridhisha kuwa mtoto ni wa kwake. Alituma pesa kila mwezi na mara moja kwa mwaka alikwenda kuwajulia hali.

Mtoto alipofika umri wa miaka nane alimpeleka Nairobi kusoma shule ya boda. Mtoto aliendelea vizuri na masomo. Alifanikiwa kupata ajira. Aliweza kumjengea mama yake nyumba ya vyumba viwili vya kulala wana sebule kijijini bafu choo na jiko nje. Kwakua maji si ya uhakika. Kwa pale kijijini nyumba yao ilikua ni kivutio, iliitwa nyumba yenye chipping.

Mama alifariki ghafla kijana akiwa safari ya kikazi DRC Congo. Kutokana na imani ya dini, wajomba walimzika dada yao aliyeishi kufikia miaka 90+. Baada ya mazishi wajomba wamehamia kwenye nyumba ya dada yao.

Rafiki alifika kuona kaburi na kuwaonea wajomba. Sasa mti umeangukia choo, wajomba wanamtaka alete hela wakitengeneze. Sasa kijana anasema nyuma mnakaa nyinyi mimi ninahusikaje kutengeneza choo ilhali mama yangu ameshaaga dunia!
 
Kwani hakupewa urithi wake?
Hata kama alimkabidhi mama yake ikawa ya mama yake, alipofariki nyumba ulitakiwa officially irudishwe kwake (kwa urithi) au wagawane na watoto wengine wa mamayake.

Huo mgawanyo ni muhimu sana ili ijulikane nyumba ni ya Nani na Nani anahusika nayo, hata kama wajomba zake wanakaa, kama nyumba ni yake basi inabidi aikarabati,

Ila kama wajomba wamejimilikisha then ni juu Yao kuihudumia hiyo nyumba
 
Huyu mama hakuwahi kuwa a mtoto, alihangaika sana ujanani mwisho alimuachia Mungu, mpaka anampata huyu mtoto wake wa pekee akiwa na miaka 50.

Wajomba wamejimilikisha nyumba lakini wanamsubiri kijana aikarabati.
 
Then it's a good time kuulizia mirathi, waendelee kukaa yeye atakuwa anaikarabati as anavoweza, Ila officially iwe nyumba yake kama ilivo mwanzo
Hilo likipita then aendelee kulifanya kazi, Ila kama wamemnyanganya aachane nao tu, watamsumbua
 
Huyu mama hakuwahi kuwa a mtoto, alihangaika sana ujanani mwisho alimuachia Mungu, mpaka anampata huyu mtoto wake wa pekee akiwa na miaka 50.

Wajomba wamejimilikisha nyumba lakini wanamsubiri kijana aikarabati.
Mimi ni mzaliwa wa vijijini Sky Eclat . Huko umasikini ulikopiga kambi. Hata kitendo cha wajomba kuhamia kwa dada yao ni ishara ya umasikini unaowazunguka hao watu.

So dogo kama yuko vizuri kiuchumi. Si vibaya akipaboresha ukizingatia mama yake kalala hapo usingizi wa milele. Vitu vingine huwezi kuhesabu gharama.
 
Wanamuona huyu bwana ni kama Mo Dewji wakati na yeye anahangaika tu na maisha yake.
 
Back
Top Bottom