brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,393
Habari kubwa pengine ambayo inatazamwa kama habari ya msimu
baada ya Emmanuel Adebayor kudai kuwa mama yake ndiye chanzo
cha kushuka kiwango kwa kuwa amekuwa akimchawia na kupelekea
kumfukuza nyumbani kwake, sasa imechukua sura mpya. Nyota huyo wa kimataifa wa Togo amekuwa hana maendeleo mazuri
katika kiwango akiwa na klabu yake ya Tottenham ambapo amefunga
magoli mawili tu msimu huu alidai kuwa mama yake ndiye chanzo cha
kusababisha ukame wa magoli. Taarifa kupitia gazeti la The Sun zimesema kuwa familia ya
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 imekosa raha na
tuhuma hizo na imedai kuwa kitendo cha mshambuliaji huyo
kumfukuza mama yake kimepelekea mama huyo kuingia mitaani na
kuanza kuuza nyanya. Gundu bado limeendelea kumuandama Adebayor baada ya
kuondolewa kikosini katika mchezo wa timu yake dhidi ya Everton
hapo jana.