Mama Wema mikononi mwa Polisi kwa kumtapeli Msama

e2n

JF-Expert Member
Dec 24, 2015
637
793
MAMA WEMA MIKONONI MWA POLISI KWA KUMTAPELI MSAMA.

DAR ES SALAAM: Msala tena! Miriam Sepetu, mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu, amejikuta mikononi mwa polisi, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Chanzo kimelidokeza gazeti hili kuwa mama huyo amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay, akidaiwa kumtapeli mfanyabiashara Alex Msama, kiasi cha fedha kinachotajwa kufikia shilingi milioni 16.
* “Mama Wema alipatwa na matatizo, akataka kuuza nyumba yake ile ya Sinza Lion, sasa katika kutafuta wateja akakutana na Msama, lakini Msama akamwambia kwa wakati ule alikuwa hana hela, lakini kuna mkopo wake katika benki moja ulikuwa umeiva, hivyo avute subira kidogo angeinunua nyumba hiyo (bei haijatajwa). “Wakakubaliana, sasa mama akamwambia Msama hata hivyo ana shida kidogo ya hela, basi jamaa akawa anampa mara leo milioni mbili, mara tatu hadi zikafika hizo 16, lakini ghafla Msama akaja kusikia ile nyumba imeshauzwa kwa mtu mwingine, alipofuatilia akakuta ni kweli, kumuuliza mama akawa haeleweki hadi jamaa akaamua kwenda polisi,”kilisema chanzo hicho. *

Ili kuweka sawa mambo hayo, Risasi Jumamosi lilifika nyumbani kwa mama Wema, Sinza Mori Jumanne iliyopita, lakini lilizuiwa kuingia ndani kwa maelezo kutoka kwa mlinzi kuwa mama hakuhitaji kuonana na mtu yeyote siku hiyo. Kesho yake, alipigiwa simu yake ya mkononi na akaipokea, lakini mwandishi alipojitambulisha na kuanza kumsomea tuhuma hizo, alisema hana muda wa kuzungumzia jambo hilo kabla ya kukata simu.
*

Kwa upande mwingine, Risasi Jumamosi lilifika ofisini kwa Alex Msama, iliyopo Kinondoni Block 41, lakini mfanyabiashara huyo hakuwepo. Mmoja wa maofisa wa ofisi hiyo, ambaye alikataa utambulisho wake kwa kuwa siyo msemaji wa Kampuni ya Msama Promotions, alikiri kuwahi kumsainisha mama Wema kiasi cha shilingi milioni tatu. Hata hivyo, gazeti hili lilimfikia Msama kwa njia ya simu yake ya mkononi na alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema; “Ni kweli nimetapeliwa na mama Wema, lakini kwa kuwa jambo hili nimeshalifikisha polisi, nadhani mkondo wa sheria utafuatwa,” alisema na kuomba asilizungumzie zaidi suala hilo. Jalada la shauri hilo limefunguliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay kwa namba OB/RB/3358
Visit website
 
Duuu kwahiyo imekuwa ni mwendo wa. "muosha huoshwa". Ama kweli ule wimbo WS " wacha waisome nambaaaaa eheeeee....."
 
1488731074508.jpg
 
Isije ikawa Ni janja ya kutaka kupata pesa kutoka Chadema
 
sinza kuna nyumba ya 16m
na hilo ni suala madai ...ulimpa 3m....mdai mahakaman
 
Lakini juzi kuna habari za magazeti ya udaku zinazomhusu wema kuhamia chadema zilipostiwa hapa picha za hayo magazeti yakiwa yamesheheni hiyo na full kushangiliwa.
Au tatizo siyo magazeti bali tatizo ni habari kama inawafurahisha au haiwafurahishi..
Ilikua baada ya wema kufanya conference!
Kama unabisha basi subiri tuone litakalo endelea!
hilo mbona halifichiki
 
Kwa Tanzania kujiunga na upinzani ujuwe kama ulikuwa jambazi au mhaini miaka ya 70s au 80s, basi jua kama kesi yako itarudi mahakamani kwa kosa la kujiunga na upinzani na sio kwa kesi asilia.

Ndukiiiii
 
Back
Top Bottom