Mama wa Kambo amtesa kinyama mtoto wa kike. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama wa Kambo amtesa kinyama mtoto wa kike.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rubi, Dec 18, 2009.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  MWANAMKE Hadija Nzali [30] mkazi wa Kimara King'ong'o anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kudaiwa kufanya ukatili kumuingiza mtoto wa mume wake mwiko sehemu za siri na kumchoma moto sehemu zake za mwili

  Jeshi la polisi nchini limesema linamshikilia mama huyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya kitendo hicho cha ukatili dhidi ya mtoto huyo.

  Awali ilidaiwa na baadhi ya majirani wanaoishi karibu na familia hiyo kuwa, wao walikuwa wakimuona mtoto huyo na makovu lakini kila walipokuwa wakijaribu kumhoji kwanini anakuwa hivyo aligoma kuelezea kwa kumuogopa mama huyo ambaye alimwambia akisema kwa watu anamuua kabisa.


  Wamesema kuwa, mwanamke huyo alikuwa akidiriki hata kumnyima chakula mtoto huyo ambapo afya yake ilikuwa ikizidi kudorora siku hadi siku zinavyoenda.


  Amesema kuwa mateso ya mtoto huyo walianza kuyasikia kupitia kwa watoto wenzake ambao alikuwa akicheza nao na binti huyo kuugulia maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na majeraha ya kipigo kutoka kwa mwanamke huyo.


  Imedaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa akielezea kuwa mama yake huyo amekuwa akiweka kijiko kwenye moto kisha kuanza kumbandika nacho mwilini mwake huku akimuingiza mwiko sehemu za siri.


  Binti huyo (jina limehifadhiwa), aliliambia jeshi la polisi kuwa alikuwa akipata mateso makali kutoka kwa mama huyo hali ambayo ilimsababishia kukaa ndani muda mwingi bila ya baba yake mzazi kujua na aliogopa kumwambia baba yake kwa kuwa alikuwa hamuamini.


  Amesema kuwa “majirani zetu walipoona hali yangu inazidi kudidimia na huku mwendo wangu ukibadilika na kukosa furaha kila kukicha ndipo waliponihoji na walipogundua mateso hayo na kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi ili niweze kusaidiwa .


  Hata hivyo mwanamke huyo alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alikana kuhusika ingawa mtoto huyo amekuwa na alama za majeraha mwilini mwake.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema kuwa, Jeshi lake linaendelea kumshikilia mwanamke huyo na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.  Binti huyo anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mwananyamala chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.
  source www.nifahamishe.com
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hii habari ilirushwa na TBC1 juzi na Elisha Eliya alifanya kazi kubwa kuwatafuta wahusika wote na kuwahoji. Mtoto alikuwa kafichwa Mbagala na mama naye alikuwa mafichoni. Ni hadithi ya kuhuzunisha sana. Hata hivyo inaonesha kuwa sisi binadamu ni wanyama wakatili kuliko viumbe vyote alivyoumba Mwenyezi Mungu.
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,696
  Likes Received: 8,232
  Trophy Points: 280
  AAaa..unyama huu uko Tanzania kweli!??
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  Baba mzazi naye ana makosa makubwa. wewe kama mzazi kwa nini uwe bandidu kwa mwanao tena wa kike?? hata anashinda kukuelezea mateso anayopeta toka ndani tena nyumbani kwako inabidi wazazi mbadilike sasa ule wakati wa baba na mtoto kuwa kama chui na swala umeisha . au mnataka kuniambia kuwa baba yake alikuwa bussy sana..aua kila siku anarudi na stress?? tubadilikeni jamani hiki kipindi cha sasa hivi ni hatari sana kwa wanetu hasa mabinti .
   
 5. m

  mTZ_halisi Member

  #5
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kha jamani....yule mama mkatili sana... sijawahi kuona m/mke kama yule

  inasikitisha ukimwangalia bint mwenyewe she is still very young
  yani hata viziwa havijaota... halafu akishateswa hivyo anafichwa chumbani
  baba yake anaambiwa amevunja ungo yuko ndani
  hata kama mwanamme, kwa jinsi alivyo yule mtoto ilibidi agundue tu
  mwanae yuko matatizoni... makovu mwili mzima...
  I really blame the dad for irresponsibilities...
  sad!!!1
   
 6. B

  Bumbwini Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu mama aliefanya kitendo hiki chakikatili aozee jela ikiwezekana afungwe jela maisha yake yooooote ili iwe fundisho kwa watu wengine na baba wa mtoto nae anafaa aadhibiwe japo kwa kuchapwa viboko 40 inakuwaje mtoto wako anapata mateso ya kikatili namna hiyo wewe umekaa unaangalia au ndio mume ***** ameshalishwa limbwata.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,089
  Trophy Points: 280
  Huko kimara hii sio mara ya kwanza kwa mama wa kambo kumfanyia ukatili wa hali ya juu mtoto.
  Kuna mtoto alichomwa moto na mama wa kambo kwa kula chakula cha house girl
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nakuunga mkono mpwa, huyu baba ni mwehu tena na yeye akamatwe. Mshenzi kabisa, inakuwaje baba unashindwa kufuatilia hali ya mtoto hadi majirani wajue kwamba hali ya mwanao si nzuri na wewe umo humo ndani. Mshenzi kabisa huyu baba tena ***** kwelikweli.
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Huyu baba ana makosa na hawezi kukwepa lawama. Llakini kwa wanaume wa kiswahili, ni jambo la kawaida kumsikiliza mama wa kambo na kuishia hapo bila kumwangalia mtoto hata kama anaumwa sana. Akishawekwa kwenye 18 za mama, biashara imekwisha. Ndo maana hata alipoambiwa kuwa mtoto wa ~10yrs amevunja ungo, zee zima la zaidi ya miaka 30 hapa duniani lilikubali tu kama taahira! Nadhani alikuwa amekamatika kisawasawa. Kama ni shuntama (limbwata) basi huyu yake imeagizwa toka Ulaya. Mtu na akili zako kamili huweze kuwa naive kiasi kile. Lakini wanaume wengi wakikamatika ni heri ukutane na kondoo tena yule mzee kabisa! Hili kubwa jinga nalo linastahili kwenda lupango likabebe mtondoo ili lijue kuwa kuzaaa hakuishii kitandani! :mad:
   
Loading...