1. Poleni kwa majukumu. Nusu mwaka imekata hivyo.
2. Naandika kwa wazazi/walezi kwenye maisha poa, hasa kina mama. Wengine wapo humu JF.
3. Akina mama wenye familia bora huwaringishia na kuwadharau kina mama wenzao wauza maandazi na watoto wao. Wengi wao hujisemea na kuwaambia watoto wao: maskini wale, wachafu, hawana akili, wananuka, watawaambukiza uchokiraa, wezi, ........
4. Hao wauza maandazi unaowakejeli ndio wanaojua maisha ya watoto wako vyema kuliko wewe. Wao wanaona mishe zote za watoto ili hali ewe wa matawi ya juu upo bize kusaka hela, ukipata muda kidogo unashinda saluni, na kutafuta wa matawi wenzio kupiga soga.
5. Huko ushuani kuna mambo ya hatari kwa familia. Nitaandika nfano mmoja kwa ufupi. Kuna familia moja baba tupo Madini, mama yupo taasisi ya UN.
Mtoto wa kwanza ni binti, ana akili sana, za darasani hata za kuwapiga fix watu wazima wakamuelewa. Wazazi wanamwamini hatari. Kama unata kutofautiana na mama yake, mweleze maovu ya nwanae. Mtoto wa pili ni binti, ana akili za wastani. Ila anaonyesha utatata na kutotofautiana na wazazi bila aibu. Hana unafiki kama dada yake.
6. Wazazi wanaamini pesa ndio kila kitu, na wamewaamisha hivyo watoto. Mama ana dharau balaa hasa dhidi ya majirani wenye uwezo mdogo kiuchumi. Baba ni mkimya sana, hajulikani mtaani.
7. Binti mkubwa ana uwezo mkubwa darasani, pia kucheza na akili za wazazi na hawawezi kujua naovu yake. Anajiandaa kuingia chuo kikuu. Ametumbukia kwenye ulevi hatari wa pombe kali akiwa na kampani nzito wa wapiga dili wa jijini (wauza unga, wakuu wa idara, ...), sambamba na uzinzi uliokubuhu na uvutaji sigara.
8. Majirani wanafahamu kila kitu, ila kwa kuwa mama yao na wao wanawadharau hawapo tayari kuwaambia wazazi. Pia wakiwaambia, wazazi watawatetea wanao na kuwwajengea najirani chuki.
Kuna siku binti mkubwa aliletwa na gari matata amelewa ile mbaya, majamaa yakambeba na kunwingiza ndani ya geti, na kumweka mlangoni. Wazazi hawakuwepo.
9. Mdogo mtu ameingia kidato cha tano.. Majirani wanafahamu anazini na house boy, na wabaune, vijana kadhaa mtaani. Alia na house boy tangu akiwa shule ya nsingi, na wabaishi kama mtu na mme wazazi wakisafiri. Wazazi hawajui, wapo bize kusaka heka. Pamoja na kuwa yuko bweni, ila kuna mchongo wa hatari unachongwa na matroni kuwatoa mabinti kwa wanaume wa jiji siku za wikiendi.
10. House girl nae ana mishe hatari. Ndio msiri mkuu wa uovu. Kuna jamaa anazini nae, jamaa anaaminika ni mwizi. Kuna siku jirani mmoja alimdokeza mama juu ya watu wasioeleweka wanaokuja nyumbani pindi wazazi hawapo, na kumtaka amtahadharishe house girl. Mama akakasirika, na kuanzia hapo urafiki baina ya mama na jirani ukakauka kabisa.
11. Kwa sasa zimebaki salamu za kinafiki baina ya mama na majirani. Huku familia ikiteketea, wazazi wakiamini katika kusaka hela. Na wasio na hela wamelaaniwa.
12. Enyi kina mama, kaeni vyema na majirani wenzenu, msaidiane kulea familia. Mtakuwa na hela, na familia itateketea kama nyasi za nyika.