Mama Salma Kikwete tukumbuke wenzio! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Salma Kikwete tukumbuke wenzio!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwalimu mpole1, Aug 2, 2012.

 1. m

  mwalimu mpole1 Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAMA SALMA TUKUMBUKE WENZIO
  Kwako Mama Kikwete, Saalam,

  Pole kwa majukumu mengi uliyonayo mimi binafsi nakutakia mfungo mwema wa Ramadhan na nina imani mwezi huu utakua na manufaa mengi kwako na kwetu kwa ujumla MAANA UTATUOMBEA WALIMU WENZIO.


  Pamoja na salamu hizi napenda nieleze wazi kuwa mzee alipata kura nyingi zetu walimu kutokana na wewe, ndo maana tulidiriki kumwita shemeji yetu, tuliamini urais kuwa kwake utakua kwako pia na hatimae kwetu walimu wenzio. Tulijua tuna mtu wa kutusemea sasa ambae ni wewe, Tulijua unayajua vema maisha ya walimu wenzio na kwamba utapata muda wa kumshauri baba kuhusu kundi hili ambalo wewe ulikua mdau kwa muda mrefu.

  Mzee wakati wa kampeni mwaka 2005 nakumbuka alikua Mwanza alisema serikali yake itamaliza matatizo ya walimu nao wabaki na kazi ya kusomesha watoto tu. lilikua jambo lililoibua hisia za walimu wengi, na kwakweli tulikua tayari kufa na shemeji yetu. alishinda vema naamini walimu wengi walitoa uungaji mkono nikiwemo na mimi. Dada/mama taaluma hii bado ina hali mbaya maisha yetu yamejaa mashaka, tumeshindwa kupata milo mitatu kwa siku, tumeshindwa sasa kulipa ada za watoto wetu mashuleni, tumekopa kila pahala penye kukopesha ili tuweze kupata ada za wanetu ambao wanaunyafuzi kutokana na milo duni tunayoawalisha kutokana na uwezo wetu mdogo. Wapo wenzetu wanapata mshahara sh 0/= kutokana na mazingira kama hayo niliyoeleza hapo juu!


  Tumejaribu kuyaeleza haya kwa muda mrefu bado hatujapata faraja wala nafuu, chama chetu cha walimu kikajaribu kuhangaiika kuona kama tunawez kufikiriwa, na hatimae tupate aheri. wameenda mahakamani hapakutokea mabadiliko, ikabidi watangaze mgomo ambao kwakweli tulitamani mzee na wewe msikie walimu wanamateso gani huku kwenye profession yako bado nako tumechinjiwa baharini

  1/8/2012 mzee akatoa hotuba nzuri sana ingawa ndani yake tuliona hukumu itakauaje siku ya leo tarehe 2/8/2012, mama wakati tukisubiri hukumu wengi walitubeza kuwa hukumu tayari imetolewa na mzee na mahakama itatimiza unabii tu! Nikweli imekua hivyo.

  Mama/dada unaweza ukaona tunavyohangaika ili kupata nafuu ya maisha katika nchi hii ambayo inaongozwa na mtu aliyeoa dada yetu itakuaje akija mtu ambae hana kabisa uhusiano nasi? Natamani sana mwanangu au ndugu yangu asijiingize kwenye taaluma hii maana haithaminiwi tena na wala haionekani kama ina umhimu wowote.

  Mama kwani wakati mnapoongea na mzee kwa masuala ya kifamilia au ya kitaifa huwezi kumshauri walau awe na huruma kwa kaka na dada zako sisi? Naamini ukijipa assignment ya kufanya hivyo kila jioni utatuokoa na kwakweli hata baada ya 2015 tutakukumbuka kwa kutupigania.


  Mwisho dada utakapokua kuwa ukila na kunywa hapo magogoni, ukumbuke wenzio huku hata kuamkia mhogo au kiazi haiwezekani tena maana hata mvua hazinyeshi vizuri hata mavuno hatupati kwenye vishamba vidogo tunavyomudu kukodi vijijini,


  Utakapo kuwa ukilala na kusinzia ukumbuke wenzio tunafukuzwa na wenye nyumba kwa kukuchelewa kulipa pango la nyumba za udongo tulizopanga kutokana na kutokuwepo kwa nyumba mashuleni. Aidha utakapo kuwa ukisafiri kwenye ile ndege ndani au nje ya nchi, tukumbuke wenzio hata matairi ya baiskeli zetu yameisha tunasubiri mshahara walau tununue mengine ili tujiepushe na pancha za mara kwa mara.

  ujapoita watoto yatima na wanawake kuwafuturisha jioni hapo pembeni ya bahari tukumbuke wenzio hatuna hata uwezo wa kutoa mchango wa rambirambi mtaani ila tunakopa kila misiba inapotokea tukisubiri mwisho wa mwezi.  Mama/dada najua unafahamu kuwa kile ambacho kingetupa kipato kidogo ni kuuza ubuyu na barafu lakini tumezuwiwa na walimu wa kuu. Tumetii yote hayo tumejaribu tuiition bado madiwani na wazazi wametushtaki. Tumeshindwa kote sasa TUNAKUANGALIA WEWE TU. Tafadhali fanya haraka kumshauri mzee vinginevyo utatukuta tumekufa kwa njaa, shinikizo la damu au utapiamlo. Utakuta ndugu zako huku hatuna tumaini hata stori hatutakupa juu ya maisha ualimu uliyoyaacha kwa miaka 10.

  Nakutakia maisha mema na utetezi mwema wa walimu wenzako.

  Mwalimu Mpole
   
 2. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijui kama kweli alikuwa mwalimu au ni yale yale ya kuunga unga. Maana ukiangalia uwezo na kiwango chake cha kuelewa unashangaa alikuwa akifundisha nini na nani wakati naye alipaswa kufundishwa? Kama huyo mama alikuwa mwalimu na akawa mfano wa walimu mliopo basi nchi yetu inaelekea kuzimu. Hata hivyo nani anajali iwapo watoto wa wakubwa wanasoma nje kwenye vyuo vizuri tena kwa pesa yenu wenyewe? Poleni walimu wenzangu mlioko huko.
   
 3. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MWL Mpole,
  pole kwa kudhani mna mtetezi. jililieni wenyewe huyo si mwenzenu, ana tyme hata ya kusoma hayo?
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Karibu Mwalimu Mpole, nina hakika mwalimu mwenzio ameisoma utapata majibu soon.
   
 5. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,093
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  na hatawakuta, atakuta makaburi tu
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,816
  Likes Received: 36,909
  Trophy Points: 280
  kenge huwa hasikii hadi umtandike mpaka damu zimtoke maskioni ndo ataskia.
   
 7. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Salma siku zote yuko bize kuchuma kama Anna Mkapa akijua kuwa kuna siku itakula kwake au madaraka yatamtoka mmewe. Hawezi kuwakumbuka walimu iwapo yeye hata hajikumbuki angalau kusoma akapata cheti hata kujua kujenga hoja kama mtu aliyekanyaga darasani. Binti Kinyozi huyu ana akili za kimachinga yaani kuhangaika na vitu vidogo vidogo kama anavyohamanika na WAMA anayotumia kuwaibia akina mama.
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,816
  Likes Received: 36,909
  Trophy Points: 280
  kwako mwalimu mpole;
  kuanzia leo hii, ukiingia darsani wafundishe wanafunzi kuichukia serikali hii legelege.
  Wafundishe wanafunzi kuwa historia ya mwanadamu hapo zamani mwanadamu alikua mamba.
  Wafundishe watoto kuwa 1+1= 11
  Wafundishe watoto kuwa kuwa wakikuta bendera ya taifa inapandishwa wao wakimbie mbio kumshambulia anayeipandisha.
  Wafundishe watoto wapige mawe msafara wa viongozi utakaopita mbele yao.
   
 9. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Achieni egemezi hili batili,
  la kunona mashavu na midomo,
  limekalia uhabithi limbukeni,
  shingoni vidoleni lajaa vyuma,
  mapambo limbukeni lakuja,
  choyo limejaa moyoni.

  Tangu lini nunda na habithi,
  ni tegemeo la wanyonge?

  Mtetezi wenu mkuu,
  ni nguvu yenu pamoja,
  panga pambana teza,
  CCM serikali ulimi nje,
  Mahakama kiburi ngii.

  Serikali ya CCM haina moyo wala akili,
  haia macho wala masikio,
  Simanzi kwao nyuchi za wakweze,
  Unyama asili yao ukatili kwao tabia.

  Lugha nzuri kwao si nyingine,
  ni ile ya hoja nguvu changanya,
  Vitendo matendo tekeleza,
  longelonge haiwatoi pangoni,
  vitendo ndiyo dawa pekee,
  Vyawatikisa mcheche kuwatia,
  Wote hakuna aso tetema.
  si CC ya CCM jaa vigagula,
  wa hirizi chale matakoni,
  vibabu hivi ubabe vimekali,
  kufa kamwe havitamani.

  Walimu si watu wa kuonewa huruma,
  wala si watu wa kupuuzwa,
  kazi yenu daraja jamii,
  mjinga ndo atawapuuza,
  nguvu yenu ni kubwa mno,
  mara kumi ya ile muijuayo,
  Ninyi ni viongozi wa viongozi,
  ongozenu nasi twaja nyuma yenu.

  kwa miaka aidha miongo yote,
  mmesaidia kuwasimika vitini,
  nguvu yenu ndo imeiweka,
  serikali ya CCM madarakani,
  mkishurutishwa kufanya hivyo,
  kwa ujira wa hofu na mashaka.

  chukueni hofu na mashaka yenu,
  na kuwanywesha yote kwa nguvu,
  wapeni kiapo na tarehe,
  ya malipo na kiama chao.
  Wanataka wakaoge,
  Mwisho wao Novemba 2015.
   
 10. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwenye maisha hakuna wa kukutea ni wewe mwenyewe na bidii yako. Kazana kusoma achana na kufundisha badilisha ajira. Hata kama ukisoma kwenye hiyo hiyo fani utakuja badili tu baada ya kufundisha utakuwa unafanya kazi nyingine ambazo zina kipato zaidi katika hiyo hiyo fani. Ukikalia kuwa Ualimu ni wito basi usilalamike wala usimpe lawama bi mkubwa wa watu yeye hapangi bajeti ya nchi. Hebu watanzania tuachane na hiyo tabia kuomba kusaidiwa ndio inatudumaza. Kazi hailipi achana nayo tena mapema kabla hujapoteza muda tafuta kitu kingine ufanye.
   
 11. B

  B.Panther Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JK Nyere(Good)

  Salma Kikwete(Sijui nisemeje)

  Mwantumu Mahiza.
  Alikuwa Mwalimu wa Mama Lwakatale pale St Marrys,Alikuwa swahiba sana na Salma,Salma alipo pata shavu la JK akampigia pande naye akala shavu.
  Mchango wake.
  Waalimu kama mnaona mishahara yenu midogo acheni kazi.(Foolish)
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yupo kwenye jengo jeupe vumbi la chaki alisha lisahau siku nyingi
   
 13. d

  decruca JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Salma kikwete yuko bize na maanadalizi ya kustafu, c unajua 2015 sio mbali? huyo mahiza unategemea aende against na waliompa shavu?
   
 14. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Nina mashaka na uwezo wa baadhi ya member
   
 15. u

  umumura Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwenzio anamiliki youtong 100, zimejaa barabara zote nchini, nyota njema ya asubuhi, anakusanya mapato, mtoto anamiliki malari, usiseme na visimaa vya mafuta, asiseme mahoteli, muda wa kusoma autoe wapi, seuze wa kukumbuka shida za wanzie. POLE SANA WALIMU WAPOLE, SHIDA YENU NI UPOLE WENU.
   
 16. MAN OF CHANGES

  MAN OF CHANGES JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  TZ kila kukicha matatizo afadhali ya jana.Natamani hata kuli,na mbele sioni njia.
  KAMA MUNGU ALIWATOA WANA WA ISRAELI MISRI KWA MTESI FARAO,BASI NA SISI ATATUTOA MIKONONI MWA MTESI CCM NA VIONGOZI WAKE WASIOJALI UTU NA MAISHA YA WENGINE.
   
 17. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tatizo la watanzania hamkomagi...mateso yote haya lakini nina uhakika uchaguzi 2015 ukifika hawa walimu madaktari na wananchi huko vijijini ambao wanalalamikaga kila siku kua hawana huduma za afya,maji,umeme, viwanja vyao vimechukuliwa na serikali, hakuna maendeleo yoyote kwenye vijiji vyao lakini bado tulivyo hatuna akili timamu au sijui ni kutoelewa nini kinachoendelea lakini bado watu wataipigia kura CCM...hapo mimi ndio hua sielewagi. Ni bora kama hupendi ccm na huna imani na cdm ni bora ukae nyumbani kura yako ipotee kuliko kuamka na kwenda kuipigia kura ccm ambayo imeshaharibu hii nchi na tupo hapa tulipo kwa sababu yao.
   
 18. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mwalimu Mpole, kwa kweli nakupa pole!!!

  Kwanzan nalaani sana jinsi vyuo vya walimu vilivyo, hawa walimu walikuwa wakisia FOE/UDSM tumegoma walikuwa wanasema yale magomaji bana...na kejeli zoote wazijuazo. Wao walikuwa wanfundishwa kuwa wapole kupita kiasi, na kujazwa maneno kama yale ya ukipigwa kofi upande wa kushoto, mgeuzie na wa kulia....this is all rubbish. Na haya ndo yamewafikisha hapo mlipo, kwa wengi wenu ni wanafiki sana, mnapretend kugoma wakati in real sense hamjagoma!

  Nataka niwaamsheni na kuwakumbusha kuwa hakuna HAKI iliwahi kuombwa kwa namna yeyote ile. Haki INADAIWA maana ni mali yako!! Stand up, collect yourselves together mdai haki yenu. Period!!!

  Mama Salma, hawezi wasaidia kamwe! Anaweza kuwa na moyo wa kuwasemea, ;lakini nchi hii haina RAISI!!! Ni mfano tu wa rais, we have weak president!!!

  Get up, stand up, stand up for your rights!!!
   
 19. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,583
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  You have said it all.
  Kazi kwao walimu...waanzie na sensa.
   
 20. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  " the majority plead exploited
  Cheated
  Disregarded
  But brother.
  How the development can be brought? (by joe colie)

  Nipende kuwakumbukumbusha walimu kuwa ni wakati wao sasa kuunda umoja na kuunganisha nguvu na makundi mengine ktk jamii na most kuungana na CHADEMA ktk kuondoa hii brutal government ambayo imeshinda kutimiza our fundamental rights, tufanye hivyo haraka iwezekanavyo na liwalo na liwe "there is nothing to negotiate"

  FEAR NOT.
   
Loading...