Mama na mtoto wauliwa kwa risasi!

Mama na mtoto wauliwa kwa risasi!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Mwanamke ajulikanaye kwa jina la Milembe Masanja na mtoto wake aitwaye Kulwa Madirisha wakazi wa kijiji cha Nyabusalu wilayani Kahama, wameuwawa kwa kupigwa risasi saa 2 usiku, wakati wakiandaa chakula.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangalla amesea Milembea aliuwawa kwa kupigwa risasi kwenye kwapa la kushoto huku mwanaye Kulwa akipigwa risasi kidevuni na tumboni, hali iliyosababisha vifo vyao papo hapo.

Hadi sasa chanzo cha tukio kinachunguzwa na hakuna mtu anayeshikiliwa, Kamanda Mangalla pia amesema bunduki ni aina ya gobore kutokana na majeraha waliyokutwa nayo marehemu.

Chanzo: EATV
 
Tunaelekea waou kuua si mwisho wa matatizo. Mume yupo? mketa habari tupe details.
 
"....dunia sasa imani imekwishaaaaa, mioyo ya watu imebadilikaaaa, kwenye watu kumii binaaadamu mmmmojaaaaa....." by Marijani Rajab, huu ni ukatili na dhuluma kwa roho za watu hata kama kuna ugomvi kati yao hiyo siyo njia ya kumaliza ugomvi huo, kutakuwa na visasi zaidi kutoka upande wa waliouawa kama ugomvi utakuwa wa kugombania vitu(labda shamba, nyumba nk), ngoja tutafute sababu za mauaji hayo ila ni ukatili na unyama uliopitiliza, vyombo vya dola vifanye uchunguzi na sheria na haki zichukue nafasi ili iwe fundisho kwa wahuni wengine wanaofanya upuuzi kama huu, Mungu atamlipa kila mtu sawa na matendo yake siku ya hukumu hata kama utaua mamilioni ya watu lakini mwishowe nawe pia utakufa na kuhukumiwa kwa mauaji hayo
 
Milembe haya majina sio mazuri jamani na kweli baba mtu anaitwa madirisha hivi wazazi wanakosa majina haya Sasa madirisha kaua mkewe na mtoto dirishani inasikitisha sana acheni majina yaajabu ajabu
 
Back
Top Bottom