Mama Mwl Janet Magufuli ni mama wa mfano wa kuigwa Tanzania pamoja na maneno yanayosemwa..yuko imara

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Mama Mwl Janet Magufuli nakuheshimu sana na nakupa hongera sana kuwa mwanamke wa mfano ktk nchi za Africa kwa kuonyesha kuwa uko pamoja na mume wako ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ktk kuendesha nchi ktk awamu hii ya tano.

Wewe ndiye ndiye mwanamke wa kiafrika kweli uliyelelewa haswa nakukubali mama Janet.

Mengi tunaongea juu yako lakini jua kuwa Mungu yuko nawe usiku na mchana wewe na familia yote ktk kipindi hiki chenye kila aina ya upinzani.

Sala zako na salaam zetu naamini Mungu huzisikia wala usiwe na shaka.Tuko pamoja na watanzania wa nakupenda sana.

Wanafunzi na walimu pale Mbuyuni primary wanakumiss sana ila wanakuombea siku zote uwe na amani kama ulivyokuwa pale shuleni.

Usijal maneno ya mitandao na vyombo vya habari hizo ni chuki binafsi wala zisikukatishe tamaa.

MUNGU yuko na wewe siku zote mama yangu.
 
Moja ya wanawake ninaowaheshimu sana hapa Tanzania akiwepo mama yangu,mke wangu na wengineo ni mama Janeth Magufuli. nimekuwa kwa karibu sana nikimfuatilia mama huyu na kugundua ni mwanamke wa kipekee hasa ambaye katika miaka takribani 30 hajatokea First Lady wa aina yake nchi Tanzania. ni mwanamke ambaye ana moyo ulioshiba kujiamini na wenye umaskini wa majivuno.

huyu mama amekuwa akisimamia anachoamini na mara nyingi ameonekana akiwa katika picha au video mbalimbali akionesha alicho nacho moyoni ni kikubwa kuliko kile tunachokiona. ni mama ambaye aliridhika ana ameridhika na kazi yake ya ualimu pamoja na kuwa mumewe alikuwa waziri serikali iliyopita na hata sasa bado anaonekana kutamani kuendelea na kazi yake ya ualimu ingawa inakuwa ni ngumu kutokana na mazingira ya nafasi ya mumewe kwa sasa.

mama huyu ambaye amekuwa makini sana kusikiliza kila linalosemwa juu ya mumewe ambaye ni rais wa nchi na kulipokea kwa hisia nzito sana akihusisha na hali halisi ya maisha ambayo wamekuwa wakiishi na mumewe. na hii imemfanya kuwa mama wa karibu na ambaye aliamua ku msupport mumewe agombee urais katika mazingira magumu sana kisiasa nchi tanzania.

mama janeth alikubali ku msupport mumewe na kuzunguka naye nchi nzima akimfanyia kampeni akionesha ustaarabu wa hali ya juu sana. mama huyu si mwingi wa maneno... mara nyingi amekuwa mkimya na unaweza msoma vizuri kupiia sura yake ya upole na yenye utulivu.

naamini huyu atakuwa mmoja ya first lady ambao hawatajilimbikizia mali kupitia miradi na mifuko mbalimbali kama ilivyotokea huko nyuma. tuzidi kumwombea Mungu amtie nguvu na ninaamini kwa namna ambavyo amepitia mengi mpaka kufika hapo alipo tuna mengi ya kujifunza toka kwake.

na mwisho tumpongeze mh rais kwa kuweza kupata mke kama mama janeth magufuli naamini analielewa hili kwa upana kabisa kuwa amepata mwanamke ambaye ni wa aina yake katika siasa za tanzania. mwenye msimamo imara lakini pia mwenye busara na kuamini anachoamini siku zote.
 
We jamaa mjanja sana... hapo usikute unamsemaga yule mwenye kimbelembele? Shauri yako
 
Compare and contrast:
de4e68a7de07d9f13b456d83b4708ffc.jpg
 
Acha uongo na kumsingizia mambo ya ajabu mama wa watu!Mama Janeth hakuzunguka na Magufuli nchi nzima kufanya kampeni,mama huyu alijiweka kando kabisa!Hili nalikumbuka vyema!Tokea mwanzo mpaka mwisho wa kampeni kaonekana jukwaani mara 2 tu
 
wanaume wengi wa kisukuma wanawapa majeraha mengi ya moyo wake zao.......wakati wake wa kisukuma ni wavumilivu sana na wana heshima ya kweli.................
 
Back
Top Bottom