Mama mkwe amevunja ndoa yangu

thanks
 
Pole ndugu kwa yaliyo kukuta.

Jua kwamba mustakabali wa ndoa upo ndani ya wanandoa wenyewe na wala si mtu mwingine yoyote nje ya wanandoa. Mimi kwa jinsi nilivyoisoma hiyo story, tatizo ni mke wako na wala sio mama mkwe wako. Ninacho kushauri, endelea kulitafakari juu ya kumrudia huyo mwanamke, jipe break huku ukifikiria na kutafakari juu ya mstakabali wa maisha yako endapo kama utamrudia huyo binti wa kinyarwanda. Tafakari kwa mwaka mzima ndipo ufanye maamuzi, Mwambie unahitaji break ya mwaka mzima ili uweze litafakari hilo swala.

Ila nakueleza kuwa; Ndoa sio jela hata kama ilifungwa kwa papa vatican.
 
Mwanamke anitukane kama mbwa ainyanyase kwa jeuri gani?? Hivi wanaume WA hivi mpo kweli?? Ingekua n mm ningepiga talaka na ukoo mzima wasinijue shwain!!
kiukweli nilimpenda kutoka moyoni, na pia imani yetu ni ile inayosema mpaka kifo kiwatenganishe ..
nimetumia muda mrefu kufikiria nichukue hatua gani, nimekuja hapa ili nichambue mawazo ya wale wenye kujua maisha ya ndoa na wasio na ndoa ,ili nijiridhishe na maamuzi yangu magumu.
asante dada yangu.
 
Msamehe......nila usiyumbe kwenye misimamo.......kamwe usimpige.........mnyooshevtu kisaikolojia
 
ubarikiwe sana,
asante
 
Nadhani nimapema sana kurudiana kwa saza muache ajifungue kisha mtoto afikishe hata miezi sita ndio utajua kama amebadirika aubshida ndizo zilizomrudisha kwako
 
Heading na content tofauti!
sio tofauti kwan mama mkwe ndio kila kitu kwake , ni marafiki wakushibana na hata kwenye harusi utambulisho... mama ndio rafiki na pacha wangu , pia m-pesa zote nimefatilia voda alikuwa anamrushia mama mkwe. yeye ndio source kwa hili suala, esides wamefanana mpaka sura
 
Sio mbaya kuomba ushauri, washauri watakushauri tu vyema, ila ikifika hatua ya kufanya maamuzi magumu ya maisha yako, listen to your heart then mshirikishe Mungu kikamilifu, nina uhakika utafanya uamuzi ulio sahihi usio na majuto. Watu wawili mnaweza kupitia situation ya kufanana na Kila mtu akadeal na hiyo situation kivyake, afu still mambo yakamnyookea kila mtu kivyake vyake. Hope utapata muafaka
 
Kaka yangu mpaka hapo hebu fanya mambo yako huyo bishost achana nae atakupa Bp bure tena mpe kichogo yeye na familia yake
 
Heri ya mwaka mpya mom..... Huyu mwanamama kaniboaa hahahha Ama kweli mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe
 
Heri ya mwaka mpya mom..... Huyu mwanamama kaniboaa hahahha Ama kweli mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe
Namshukuru Mungu nimeuona, heri ya mwaka mpya na kwako pia ma. Na kweli maandiko hayakukosea hata, asubiri tu atakachokiamua mumewe. Sijui hata alipatwa na nini sasa mwee
 
Matunzo toa,ila mtoto akizaliwa hakikisha ni wako kweli....umesema si Mtz..ana vibali vya kuishi nchini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…