Mama Mkwe amenishangaza! Anamwambia mke wangu (Mwanaye) ataachana na mimi kama yeye alivyoachana na Baba Mkwe

Habari wana JF

Last week imekuja na familia ukweni huku Ifakara. Wakwe zangu yaani baba na mama mkwe walitengana. Baba yupo hapa mjini mama yuko nje kidogo ya mji. Baba kaoa mke mwingine na mama kaolewa. Kabla hawajatengana walishazaa watoto wanne. Watatu wa kike na mmoja wa kiume. Me nmeoa binti mmoja wao kwa ndoa mwaka jana.

Baada ya kukaa kwa baba mkwe tukaenda nje ya mji kumtembelea mama mkwe.

Nilitoka kuzurura na shemeji yangu, ile narudI home nakuta kuna mzozo, mama na mke wangu. Nikaingia nikakaa, mama akaendelea kuongea, maneno yaliyonishangaza. Maneno hayo ni haya.

'Nyie watoto mnadharau sana ndoa yangu, kisa nimeachana na baba yenu basi mnaona mimi sina maana. Kutwa mnanipa mimi lawama kwamba nilimkimbia baba yenu, ila hamjui ukweli ni upi ulionifanya mimi niondoke hasa wewe umeolewa mwaka jana, unaona kama ndoa ni rahisi, kisa mnaishi kwa amani, me nakuambia huu ni mwanzo tu. Hata mimi na baba yenu tulikua na amani zaidi ya hivi kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo.

Kwahiyo nakuambia na wewe, usijidai sababu ya huu mwaka uliokaa katika ndoa. Nakuambia magumu yanakujia, utaiona ndoa chungu, na utasema heri mimi mama yenu nilieikimbia ndoa ya baba yenu. Kama mimi ni mama yenu basi lazima na nyie mtafata mkondo wangu. Itafika siku hatutachekana. Usidanganyike na huu upya wa hii ndoa.

Sasa Wakuu, haya maneno mnayachukuliaje? Ikizingatiwa sio ya siri. Yalikuwa yanasemwa mbele yangu. Hadi nikaamua kuingilia na kuwatuliza. Nimekosa amani ya moyo. Sababu nilikuwa nadhani wazazi watakua mstari wa mbele kuombea ndoa hii ikae salama. Badala yake wana imani ipo siku tutavurugana katika ndoa.
Kemea tu kama kweli unampenda mkeo. Mi aliyewahi kuwa mwanamke wangu aliniambia kuwa mama yake alinwambia hataolewa na mwanaume anayependana nae kwa dhati. Pia alikuwa akimwambia hakuwahi kumpenda baba yao (marehemu). Ni muda tumeachana sasa
 
Habari wana JF

Last week imekuja na familia ukweni huku Ifakara. Wakwe zangu yaani baba na mama mkwe walitengana. Baba yupo hapa mjini mama yuko nje kidogo ya mji. Baba kaoa mke mwingine na mama kaolewa. Kabla hawajatengana walishazaa watoto wanne. Watatu wa kike na mmoja wa kiume. Me nmeoa binti mmoja wao kwa ndoa mwaka jana.

Baada ya kukaa kwa baba mkwe tukaenda nje ya mji kumtembelea mama mkwe.

Nilitoka kuzurura na shemeji yangu, ile narudI home nakuta kuna mzozo, mama na mke wangu. Nikaingia nikakaa, mama akaendelea kuongea, maneno yaliyonishangaza. Maneno hayo ni haya.

'Nyie watoto mnadharau sana ndoa yangu, kisa nimeachana na baba yenu basi mnaona mimi sina maana. Kutwa mnanipa mimi lawama kwamba nilimkimbia baba yenu, ila hamjui ukweli ni upi ulionifanya mimi niondoke hasa wewe umeolewa mwaka jana, unaona kama ndoa ni rahisi, kisa mnaishi kwa amani, me nakuambia huu ni mwanzo tu. Hata mimi na baba yenu tulikua na amani zaidi ya hivi kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo.

Kwahiyo nakuambia na wewe, usijidai sababu ya huu mwaka uliokaa katika ndoa. Nakuambia magumu yanakujia, utaiona ndoa chungu, na utasema heri mimi mama yenu nilieikimbia ndoa ya baba yenu. Kama mimi ni mama yenu basi lazima na nyie mtafata mkondo wangu. Itafika siku hatutachekana. Usidanganyike na huu upya wa hii ndoa.

Sasa Wakuu, haya maneno mnayachukuliaje? Ikizingatiwa sio ya siri. Yalikuwa yanasemwa mbele yangu. Hadi nikaamua kuingilia na kuwatuliza. Nimekosa amani ya moyo. Sababu nilikuwa nadhani wazazi watakua mstari wa mbele kuombea ndoa hii ikae salama. Badala yake wana imani ipo siku tutavurugana katika ndoa.
Huenda wana tatizo la kiukoo kwahyo Mambo hayo hutembea na damu
 
Sasa umeenda kusalimia ukweni ukalale wapi? Labda kama hakuna nyumba au chumba, utaenda guest si utaambiwa unajidai au dharau?
Mimi silali ukweni hata kuwe na nyumba kubwa kiasi gani.na hili hata mkewangu3na familia yao wanalitambua.si kuwa dharau hapana lakini ni utaratibu niliojiwekea.
 
hakuna ubaya hapo mama mkwe anamkumbusha mwanaye asijisahau sana naana wanaume tunabadilika muda wowote so wasimdharau na kuona hana akili kwa kumuacha baba yao inawezekana kuna kitu nyuma ya pazia hakuwahi kuwasimulia...

hio ni challenge kwako pia
 
Maamuzi ya kuachana hana mtu yoyote isipokua wewe mwenyewe ukiamua ndio unalotaka ila hakuna ambae anaweza kuleta msukomo itakua vzr kama ukiwatenga kwa mda inaweza kusaidia
 
We si mlokole...ndo mawazo yenu hayo walokole.so tumekuelewa
Huwezi kunielewa ila walionielewa watakuwa wameelewa lakini pia nimeongea based on my own experience kwamba nimeoa familia ambayo baba na mama waliachana so naongea nachokijua na sio story za kusimliwa. Kwa hiyo please acha kugeneralize sijui walokole ama wapagani hapa hayahusiani tujikite tu kwenye mada tumsaidie ndugu yetu kama kuna mwenye mawazo chanya
 
Broken homes huzalisha watoto wanaokuwa na machungu ya kukosa upendo wa asili , uchungu huo ni wa asili hautoki kwa kumpata mme au mke ukubwani . Oa au olewa ukijuu una tatizo la uchungu izalishayo chuki na gubu lisilo na sababu leo utampenda mtu ukiwa ndani ya ndoa unafikiri ile furaha ya ndoa itaondoa uchungu baada ya mda unajikuta ule uchungu wa asili upo na unashindwa kuhimili ndoa sababu nguzo kuu ya ndoa ni kupendana sasa wewe kiasili upendo wa asili umevurugwa na uchungu wa malezi duni au ya single parent au ya baba au mama wa kambo , hapo mtatakuwa mji wekee ratiba za ibada zile za roho ba kweli ndipo mtapata faraja na mkifika kanisani msali kweli sio mzuge mjifanye mko ok , kama ni nyie waislam tafuteni wahubiri wazuri wa familia na ndoa yupo sheikh mmoja jina limenitoka you tube anaptikana ni ana mahubiri mazuri kuvunja hizi curse . Na muache kujilinganisha hasa wake utakuta kihistoria ana hiyo curse lakini anajilinganisha na wenzake anayewaona wana furaha na ndoa zao hajui wenzake wana furaha za asili za kulelewa na both parents na wana experience kuona how marriage is handled , anaishia kuona hawezi mpa furaha mumewe cos anajiona amejawa na machungu aliyoshindwa kuyatoa kumpenda mme anaona haijasaidia , anaenda kwa vibenteni nako anakuta uchungu haotoki anaamia kwa mume wa mtu nako hivyo sasa anakutana marafiki wadangajj hapo ndio anaingia kuzimu kabisa , dawa ni kujikibali historia zenu furahieni uhai wenu na watoto Mungu kama amewajalia jitahidini kupendana kwa kumtanguliza Mungu itawawia ngumu lakini muwe hodari ili
mji wekee historia tofauti na historia waliziweka wazazi wenu za kutengana , wazazi wenu wasameheni waheshimuni lakini ushauri wao muwe mnauchukua kwa tahadhari kwani bible imesema mtaachana na wazazi wenu mtaambatana ninyi wawili muwe kitu kimoja , msianfalie pembeni
Jikubalini mlivyo chekeni
Mfurahie maisha yenu Mungu aliwajalia msijilinganishe na yeyote wala msishindane na yeyote bali kuweni na amani na hata walio wazidi furaha , maisha nk pambaneni kuurahia leo yenu mkijenga kesho bora yenu.
My friend umemaliza kila kitu kwenye hili andiko lako, yaani kama ni thesis haihitaj kwenda kwa external examiner
 
Back
Top Bottom