Mama Mkwe amenishangaza! Anamwambia mke wangu (Mwanaye) ataachana na mimi kama yeye alivyoachana na Baba Mkwe

Clinker belite

Senior Member
Jan 19, 2020
135
1,000
Habari wana JF

Last week imekuja na familia ukweni huku Ifakara. Wakwe zangu yaani baba na mama mkwe walitengana. Baba yupo hapa mjini mama yuko nje kidogo ya mji. Baba kaoa mke mwingine na mama kaolewa. Kabla hawajatengana walishazaa watoto wanne. Watatu wa kike na mmoja wa kiume. Me nmeoa binti mmoja wao kwa ndoa mwaka jana.

Baada ya kukaa kwa baba mkwe tukaenda nje ya mji kumtembelea mama mkwe.

Nilitoka kuzurura na shemeji yangu, ile narudI home nakuta kuna mzozo, mama na mke wangu. Nikaingia nikakaa, mama akaendelea kuongea, maneno yaliyonishangaza. Maneno hayo ni haya.

'Nyie watoto mnadharau sana ndoa yangu, kisa nimeachana na baba yenu basi mnaona mimi sina maana. Kutwa mnanipa mimi lawama kwamba nilimkimbia baba yenu, ila hamjui ukweli ni upi ulionifanya mimi niondoke hasa wewe umeolewa mwaka jana, unaona kama ndoa ni rahisi, kisa mnaishi kwa amani, me nakuambia huu ni mwanzo tu. Hata mimi na baba yenu tulikua na amani zaidi ya hivi kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo.

Kwahiyo nakuambia na wewe, usijidai sababu ya huu mwaka uliokaa katika ndoa. Nakuambia magumu yanakujia, utaiona ndoa chungu, na utasema heri mimi mama yenu nilieikimbia ndoa ya baba yenu. Kama mimi ni mama yenu basi lazima na nyie mtafata mkondo wangu. Itafika siku hatutachekana. Usidanganyike na huu upya wa hii ndoa.

Sasa Wakuu, haya maneno mnayachukuliaje? Ikizingatiwa sio ya siri. Yalikuwa yanasemwa mbele yangu. Hadi nikaamua kuingilia na kuwatuliza. Nimekosa amani ya moyo. Sababu nilikuwa nadhani wazazi watakua mstari wa mbele kuombea ndoa hii ikae salama. Badala yake wana imani ipo siku tutavurugana katika ndoa.
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
16,282
2,000
Mwanangu ulikua unarekodi nn??

Poa tuyaache hayo.,.... Mama mkwe wako HAFAI.

Na kama mkeo atakua na tabia ya kumsikiliza kama mshauri wake mkuu, chamoto utakiona.

Siku nyingine kwakua ni mkweo... Safari anzia kwa Mama huyo halafu malizia kwa mzee..

Utanishukuru.
 

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,386
2,000
Kusema ukweli binafsi nimeoa familia ambayo mama na baba walitengana, ila mtu akija kuniomba ushauri kijana anaetaka kuoa mtanisamehe sana ila siwezi kumshauri akaoe kwenye nyumba ambayo baba na mama walitengana, kama kifo ndio kiliwatenganisha hapo sawa ila eti baba anaishi na mama anaishi huku wametengana mimi atakaenishauri ntamwambia asioe kwenye familia hiyo. Kwa kesi ya binti kuolewa kwenye familia ambayo wazazi walitengana sina experience nayo ila kwa mwanaume kuoa binti ambae baba na mama waliaachana mazima kila mtu anaishi kwake tafadhari fikiria mara mbili there is a consequences. Kwa ntakaemkwaza anisamehe ila ukweli ndio huo
 

privity

Member
Feb 6, 2020
93
400
Mfuate akiwa hana hasira unaweza kujifunza kitu.
Hatma ya ndoa yako ipo mikononi mwako na mkeo huku ukimshirikisha Muumbaji wenu.
 

Kiyawi

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
1,807
2,000
Awali ya kwanza, usimchukie mkwe upande wa baba wala Mama hata chembe. Chuki huzuia Baraka kutoka kwa Mungu. Pili kama wewe ni mtu mcha Mungu, usiwe na wasiwasi

Kumbuka katika familia kuna mgonjwa ambayo huridhiwa( generational inheritance like sickle cell, cancer, HBP, mental disorder, uchawi) magojwa na kuridhi.

Kwa kithungu huitwa “family curses, generational curse” ambayo ni Mtumishi wa Mungu wa kweli ndiye anaweza kuyavunja yaani healing and deliverance.

Kama mke wako hatakuwa delivered itafika kipindi yatatokea kwako! She has to be delivered by a True Man of God na siyo kwa Ma Pastor wa hivihivi.

Yaani siyo kuambiwa kupanda mbegu ndo aombewe, not at all. Mchungaji wa kweli hadai hata senti moja kabla au baada ya deliverance, ni free of charge.

Kama unataka msaada mtafute Mama Blandina Nyoni ambaye wakati fulani alikuwa Katibu Mkuu wa wizara, moja utapata maelekezo. Hii ni kwa faida yako ya familia yako else hiyo curse itawafika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom