madala mujipa
JF-Expert Member
- Feb 23, 2017
- 1,417
- 860
Salaam wadau,
Namshukuru mungu pamoja na umri kwenda lakini kwa kuwa bado nipo town najiita babu mbishi,
Bahati nyingine mke wangu amepata mtoto na tamu zaidi mtoto wangu mwingine niliezaa na mke wangu wa kwanza huko tanga ameniletea zawadi ya gari,toka huko falme za kiarabu japo ni kama kile cha lodi lofa lakini naamini kuna wengineo hamjamiliki
Jamani kubwa lilionikuta mpaka nimeamua kuwafikishia ndugu zanguni ni huyu mama mkwe,mke wangu bado ni msichana mbichi kabisa kamaliza form six nikamuoa,na mama ya mke wangu nae bado anadai yaani wakisimama na mwanawe kama mtu na dada yake,
Sasa tangu aje hapa huyu mama mkwe na mtoto wangu nae yupo hapa nyumbani,simuelewi huyu mkwe wangu kwanza hupita na khanga moja tu kwenda kuoga baadae akitoka huko kuoga na khanga imelowa na mbaya zaidi amejaliwa kumshinda mwanawe ma-ashallah,
Akitoka hujilaza na mkeka hapa sitting room na huichukua miguu yake na kuikunja nne huku amelala chali majipaja yote nje muda mwengine kifudifudi ikifikia hapo mimi huwa naondoka ,na yule mtoto wangu mpaka ameniuliza kuhusu ule uzushi wa bibi yake wa kufikia,
Sasa kubwa na la kushangaza ni juzi kati tumekwenda madukani kununua nguo za watoto ,mama mkwe amenga'ng'ania nimchagulie chupi, nimnunulie mpaka aibu,hadi dada muuza nguo ameshangaa na kuniuliza nani wangu kwa vile alivyokuwa analalamika ,jibu lake ni kuwa cha ajabu ni nini,neno lake la mwisho kama mimi sitaki basi huyu mtoto wangu jesse amchagulie mtoto akaona uchuro akajikataa,
Kwa kuwa ameona hii gari analazimisha kutolewa out yaani naona kero sasa na halali mpaka yeye ndio anifungulie mlango,nafikiria nimweleze mwanawe ili ampe nauli aondoke lakini naona kama nitawagombanisha na pia nafikiria labda,nimwambie ukweli tu mama mkwe lakini sina hakika nitaanzaje.
Jamani nimemchoka huyu mama mkwe nimfanyaje mwanangu kaamua kwenda kwa mama yake baada ya vituko kuzidi