Mama Mgwhira asisitiza kwamba hajaachia Uenyekiti wa ACT Wazalendo hadi Juni 15

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,649
2,000
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema hajaachia ngazi yake ya uenyekiti wa Chama cha ACTWazalendo mpaka Juni 15 Kamati Kuu ya chama hicho itakapokaa na kujadiliana kuhusu suala hilo.

Akihojiwa na mwandishi wa habari hizi jana kabla ya kwenda mtamboni kuhusu nafasi yake kwenye chama kukaimiwa na Yeremia Kulwa mpaka Machi mwakani wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho, Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa chama kimemweka kaimu na ni kitu cha kawaida pale mtu mwenye nyadhifa fulani anapokuwa nje ya ofisi.

Alisema, “Sijaacha Uenyekiti, kwa kawaida nikiwa mbali na ofisi au nikiwa nimesafiri, nafasi yangu imekuwa ikikaimiwa ili shughuli za chama ziendelee. “Kwa kuwa nipo Kilimanjaro na nitakuwa na majukumu mengi kwa kipindi hiki, ni sawa nafasi yangu kukaimiwa na mtu mwingine.”

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa leo ataanza kazi na shughuli ya kwanza itakuwa ni kufika ofisini na kusaini kitabu cha mahudhurio kisha atafanya kikao na kamati ya ulinzi ya mkoa huo.

Pia alisema atakutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa mkoa huo ili kufahamiana na kujua jinsi atatekeleza ilani ya chama hicho, kisha ataenda kuhani msiba wa Mbunge wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyezikwa juzi mjini Moshi.

Baada ya kufanya hivyo atarejea ofisini na kuendelea na majukumu mengine yatakayokuwa mezani kwake. Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba iliyotolewa jana, Kamati ya Uongozi (kwa mujibu wa Ibara za 29 (24) ya Katiba ya ACT Wazalendo) ilitangaza kumteua Yeremia Maganja kukaimu nafasi hiyo ya Mghwira mpaka uchaguzi mkuu utakapofanyika.

Chanzo: Mtanzania
 

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,009
2,000
Kuna mijitu hata kura haikumpa leo nayo inacomment!Kama mlimpenda sana si mngempa aongoze nchi akiwa mwenyekiti na Rais ili akwepe hizi teuzi!Mama piga kazi haya maneno hata kwny kanga yamejaa
 

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,246
2,000
Aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Anna Mgwira amesema yeye hajapinga kuondolewa uenyekiti wa ACT wazalendo ila amepinga utaratibu uliotumika.

Hapingi utaratibu kwa ajili yake ila ni utaratibu unaotakiwa kuwa kwenye vyama vyote, kuwamteuliwa wa mkutano mkuu hutenguliwa na mkutano mkuu, mteuliwa wa halmashauri kuu pia hutenguliwa na halmashauri kuu na ACT wamefanya haraka mno na alikuwa ameshawaomba wakutane tarehe 15 lakini wakaharakisha

Amewashangaa waandishi wa habari kuchukua habari nusu na kuacha habari za muhimu kwa maendeleo

Chanzo: Millard Ayo
 

Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,616
2,000
Aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Anna Mgwira amesema yeye hajapinga kuondolewa uenyekiti wa ACT wazalendo ila amepinga utaratibu uliotumika.

Hapingi utaratibu kwa ajili yake ila ni utaratibu unaotakiwa kuwa kwenye vyama vyote, kuwamteuliwa wa mkutano mkuu hutenguliwa na mkutano mkuu, mteuliwa wa halmashauri kuu pia hutenguliwa na halmashauri kuu na ACT wamefanya haraka mno na alikuwa ameshawaomba wakutane tarehe 15 lakini wakaharakisha

Amewashangaa waandishi wa habari kuchukua habari nusu na kuacha habari za muhimu kwa maendeleo

Chanzo: Millard Ayo
Kama anaujua utaratibu na yeye alitakiwa kuwashirikisha waliomchagua, kuwa mwenyekiti wao, kabla hajaamua kukubali uteuzi wa mwenyekiti wa chama kingine kuwa mkuu wa mkoa na mjumbe wa mikutano ya chama hicho ambacho kinapingana na cha kwake?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom