Aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Anna Mgwira amesema yeye hajapinga kuondolewa uenyekiti wa ACT wazalendo ila amepinga utaratibu uliotumika.
Hapingi utaratibu kwa ajili yake ila ni utaratibu unaotakiwa kuwa kwenye vyama vyote, kuwamteuliwa wa mkutano mkuu hutenguliwa na mkutano mkuu, mteuliwa wa halmashauri kuu pia hutenguliwa na halmashauri kuu na ACT wamefanya haraka mno na alikuwa ameshawaomba wakutane tarehe 15 lakini wakaharakisha
Amewashangaa waandishi wa habari kuchukua habari nusu na kuacha habari za muhimu kwa maendeleo
Chanzo: Millard Ayo
Hahahaha kwa kweliLipumba in making,
akae kimya afanye kazi.
Mbona "umepanic". Kulikoni?Kwa mujibu wa nani na minajili ipi?
Nani kapinga kuhama chama?
Kwa nini umetaja CHADEMA na si CUF wala chama kingine chochote cha upinzani?
Kinachokufanya uone nimepanic ni kipi?Mbona "umepanic". Kulikoni?
Kwanini CUF na sio Chadema. Kwani Lowasa alihamia CUF?Kinachokufanya uone nimepanic ni kipi?
Hata chafya sijapiga bado.
Unataka nione kwamba akili yako ni ndogo sana kiasi kwamba pahala ambapo hata chafya sijapiga, umeona nimepanic.
Hujajibu maswali niliyouliza. Tunaenda kwa hoja hapa.
Angalau kama hutaki kujitambulisha kama guluguja.
Lowassa anahusiana vipi na mimi au na maneno niliyosema hapa?Kwanini CUF na sio Chadema. Kwani Lowasa alihamia CUF?
Kwa nini unzunguka mbuyu?Lowassa anahusiana vipi na mimi au na maneno niliyosema hapa?
Angehamia Chadema angekuwa mama bomba haijawahi kutokea.
Angehamia Chadema angekuwa mama bomba haijawahi kutokea.
Hujajibu swali langu.Kwa nini unzunguka mbuyu?
Ni sawa na kupoteza muda.Hijajibu swali langu.
Lowassa anahusiana vipi na mimi au maneno niliyoyasema hapa?
Wewe, kwa kukataa kujibu swali la wazi na linaloeleweka kabisa, ndiye unayezunguka mbuyu.
Mbuyu ni swali langu.
Ili usizunguke mbuyu, unatakiwa kulijibu.
Swali lako ya kuniuliza "Kwa nini unazunguka mbuyu" ni jitihada zakobwewe kuzunguka mbuyu.
Lowassa anahusika vipi na mimi au maneno niliyoandika hapa?
Hujanijibu swali hili.
Hata humu jf yupo unaweza kumuita akakusikiaMsema kweli mpenzi wa Mungu, mama ameniangusha sana,
Acheni tu,
Mama Mungu anakuona
Kupoteza muda unatupotezea wewe uliyejitoa akili na unayeruka maswali yote unayoulizwa. Unanukuu maswali na kujibu maruweruwe.Ni sawa na kupoteza muda.
Aendelee kubakia ACT awavuruge kama alivovuruga kura za UKAWA,,MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema hajaachia ngazi yake ya uenyekiti wa Chama cha ACTWazalendo mpaka Juni 15 Kamati Kuu ya chama hicho itakapokaa na kujadiliana kuhusu suala hilo.
Akihojiwa na mwandishi wa habari hizi jana kabla ya kwenda mtamboni kuhusu nafasi yake kwenye chama kukaimiwa na Yeremia Kulwa mpaka Machi mwakani wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho, Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa chama kimemweka kaimu na ni kitu cha kawaida pale mtu mwenye nyadhifa fulani anapokuwa nje ya ofisi.
Alisema, “Sijaacha Uenyekiti, kwa kawaida nikiwa mbali na ofisi au nikiwa nimesafiri, nafasi yangu imekuwa ikikaimiwa ili shughuli za chama ziendelee. “Kwa kuwa nipo Kilimanjaro na nitakuwa na majukumu mengi kwa kipindi hiki, ni sawa nafasi yangu kukaimiwa na mtu mwingine.”
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa leo ataanza kazi na shughuli ya kwanza itakuwa ni kufika ofisini na kusaini kitabu cha mahudhurio kisha atafanya kikao na kamati ya ulinzi ya mkoa huo.
Pia alisema atakutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa mkoa huo ili kufahamiana na kujua jinsi atatekeleza ilani ya chama hicho, kisha ataenda kuhani msiba wa Mbunge wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyezikwa juzi mjini Moshi.
Baada ya kufanya hivyo atarejea ofisini na kuendelea na majukumu mengine yatakayokuwa mezani kwake. Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba iliyotolewa jana, Kamati ya Uongozi (kwa mujibu wa Ibara za 29 (24) ya Katiba ya ACT Wazalendo) ilitangaza kumteua Yeremia Maganja kukaimu nafasi hiyo ya Mghwira mpaka uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Chanzo: Mtanzania
Duh, naona umeamua kuandika insha.Kupoteza muda unatupotezea wewe uliyejitoa akili na unayeruka maswali yote unayoulizwa. Unanukuu maswali na kujibu maruweruwe.
Kati yangu ninayeuliza maswali yanayoeleweka na wewe unayejibu majibu yasiyoeleweka wala kujibu maswali niliyoyouliza, nani anapotrza muda?
Wewe ni guluguja unayefikiri kila anayehoji hizi habari ni CHADEMA na hivyo unaweza kumbana kwa maswali ya Lowassa.
Katika kujibiringita kwako kiguluguja haijawahi kutokea ufikiri kwamba mtu asiye CHADEMA wala kumuunga mkono Lowassa anaweza kuhohi suala hiki.
Yaani huo ndio udogo wa upeo wako.
Kwa guluguja hata nukta ni insha.Duh, naona umeamua kuandika insha.