stata mzuka
JF-Expert Member
- Nov 25, 2012
- 4,834
- 1,765
Kweli nimeamini ukishaondoka Madarakani Nguvu huna tena,,familia hii ni mara wakatiwe umeme mara hivi.
Kama hata ya familia baba wa taifa inafanyiwa hivi, vipi kwa sie akina kapuku.?
Naanza kupata picha, kumbe kuna viwanja ambavyo utavikuta katikati ya mji mkoa wowote huwa ni vya wakubwa na wajukuu zao, na vitukuu vyao,, Hivi mama maria au kiongozi yeyote wa serikali mwenye umri wa miaka 75 na kuendelea bado anapigania viwanja?, mbona nhata wajukuu zao ni wakubwa wana uwezo wa kuomba kiwanja ardhi bila kutumia jina la baba au babu.
Hivyo viwanja lini alipewa Nyerere? Kama ni Kabla ya 1999 Ina mañana ni zaidi ya miaka 15. Kila mmiliki anatakiwa kuendeleza kiwanja hicho katka muda wa miaka 3. La sivyo kiwanja kinarudi kwenye milki ya serikali na mtu yeyote a naweza kumilikishwa. Sasa viwanjwa hivyo vyote kwa nini hawakuviendeleza. Na wewe kakutuma nami Kuwa wakili wa Maria?
Mama Maria Nyerere adhulumiwa viwanja
MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria amedhulumiwa viwanja vitatu tofauti mjini Dar es Salaam. Hali hiyo, imesababisha kuwapo na mgogoro mkubwa kati ya familia ya Nyerere na watu ambao wanadai wameuziwa viwanja hivyo miaka kadhaa iliyopita. Viwanja hivyo ambavyo vipo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kimoja kipo Mikocheni B Plot 402 Block C na kingine kipo Msasani Beach Namba 778, ambacho kinadaiwa kugawanywa kwa watu wawili.
Viwanja hivyo, vinadaiwa kuvamiwa na mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, Paul Mushi na mkwe wa Hayati Rashid Kawawa aitwaye Issa Majura Mshangama.
Habari za uhakika kutoka ndani ya familia hiyo, zilizothibitishwa kwa MTANZANIA Jumatano na nyaraka mbalimbali, zinasema kutokana na hali hiyo, Mama Maria amelazimika kuiandikia Serikali barua akitaka msaada wa kurudishiwa viwanja vyake.
Katika nyaraka hizo, zinaonyesha viwanja hivyo ni mali halali ya mtoto wa tatu wa Mwalimu, John Nyerere.
Katika barua yake ya malalamiko kwa Kamishina wa Ardhi ambayo Mama Maria aliiandika Mei 28, mwaka huu inasema; kijana wangu, John Nyerere ni mmiliki halali na kwamba ana vielelezo kamili vya kisheria.
Ofisi yako ilimpa Letter of Offer ambayo anayo mpaka sasa. Lakini ameshindwa kujenga katika eneo hilo kwa sababu ya uvamizi wa nguvu wa mtu aitwaye Paul Mushi, ambaye ameweza kuhodhi kiwanja hicho kwa miaka mingi, bila kujali au kuogopa sheria za nchi.
Kwa vile mwanangu, John anaumwa na hawezi kutetea haki yake dhidi ya mvamizi huyo, nathibitisha kuwa John amemuomba na kumteua George Francis Mlawa ambaye ni mwanasheria, amsaidie kupigania haki hiyo iliyo wazi, lakini anazuiwa kuipata.
Nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa Machi 12, mwaka huu, John alimuandikia barua Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, akikana kufanya mauziano ya kiwanja Na.778 kwa Issa Majura.
Sehemu ya barua hiyo inasema: Kwanza kabisa nakana kufpaul mushi ni jambazi sugu kama alex ma
Hivyo viwanja lini alipewa Nyerere? Kama ni Kabla ya 1999 Ina mañana ni zaidi ya miaka 15. Kila mmiliki anatakiwa kuendeleza kiwanja hicho katka muda wa miaka 3. La sivyo kiwanja kinarudi kwenye milki ya serikali na mtu yeyote a naweza kumilikishwa. Sasa viwanjwa hivyo vyote kwa nini hawakuviendeleza. Na wewe kakutuma nami Kuwa wakili wa Maria?