Mama Maria Nyerere adhulumiwa viwanja

Mama Maria Nyerere adhulumiwa viwanja

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,768
Reaction score
5,102
MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria amedhulumiwa viwanja vitatu tofauti mjini Dar es Salaam. Hali hiyo, imesababisha kuwapo na mgogoro mkubwa kati ya familia ya Nyerere na watu ambao wanadai wameuziwa viwanja hivyo miaka kadhaa iliyopita.
Viwanja hivyo ambavyo vipo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kimoja kipo Mikocheni ‘B’ Plot 402 Block C na kingine kipo Msasani Beach Namba 778, ambacho kinadaiwa kugawanywa kwa watu wawili.

Viwanja hivyo, vinadaiwa kuvamiwa na mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, Paul Mushi na mkwe wa Hayati Rashid Kawawa aitwaye Issa Majura Mshangama.

Habari za uhakika kutoka ndani ya familia hiyo, zilizothibitishwa kwa MTANZANIA Jumatano na nyaraka mbalimbali, zinasema kutokana na hali hiyo, Mama Maria amelazimika kuiandikia Serikali barua akitaka msaada wa kurudishiwa viwanja vyake.

Katika nyaraka hizo, zinaonyesha viwanja hivyo ni mali halali ya mtoto wa tatu wa Mwalimu, John Nyerere.

Katika barua yake ya malalamiko kwa Kamishina wa Ardhi ambayo Mama Maria aliiandika Mei 28, mwaka huu inasema; “kijana wangu, John Nyerere ni mmiliki halali na kwamba ana vielelezo kamili vya kisheria.

“Ofisi yako ilimpa Letter of Offer ambayo anayo mpaka sasa. Lakini ameshindwa kujenga katika eneo hilo kwa sababu ya uvamizi wa nguvu wa mtu aitwaye Paul Mushi, ambaye ameweza kuhodhi kiwanja hicho kwa miaka mingi, bila kujali au kuogopa sheria za nchi.

“Kwa vile mwanangu, John anaumwa na hawezi kutetea haki yake dhidi ya mvamizi huyo, nathibitisha kuwa John amemuomba na kumteua George Francis Mlawa ambaye ni mwanasheria, amsaidie kupigania haki hiyo iliyo wazi, lakini anazuiwa kuipata.”

Nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa Machi 12, mwaka huu, John alimuandikia barua Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, akikana kufanya mauziano ya kiwanja Na.778 kwa Issa Majura.

Sehemu ya barua hiyo inasema: “Kwanza kabisa nakana kufanya mauziano na ndugu (Issa Majura), kiwanja changu sijakiuza kwa mtu yeyote yule, kama kuna mtu anadai kuwa nimemuuzia anadanganya, naomba aitwe na mimi nije mbele yako athibitishe jinsi nilivyomuuzia kiwanja hicho.

“Ninachokumbuka, ndugu Majura alivamia kiwanja changu baada ya kumuondoa kwenye kiwanja hicho, hajarudi tena mpaka ninapopata taarifa kutoka kwenye ofisi yako kwamba kauziwa kiwanja changu,” ilieleza barua hiyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo, John aliiomba manispaa impatie nyaraka zinazothibitisha mauziano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo.

Miongoni mwa nyaraka hizo, ni pamoja na nakala ya hati ya makubaliano ya mauzo (Deed of Transfer, Sales Agreement), Stakabadhi za kodi za Serikali zilizolipiwa, barua ya toleo aliyopewa Majura na kodi ya malipo (Capital Gain tax) alilipa nani.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya familia hiyo, zilieleza kuwa manispaa hiyo hadi sasa haijatoa nyaraka hizo.

Pamoja na wavamizi hao kuendelea kuhodhi viwanja hivyo, familia bado inaendelea kulipia gharama za ardhi kila mwaka, huku wanaotumia rasilimali hiyo ni wengine.

Chanzo cha habari kilieleza kuwa: “Kwa muda mrefu familia ya Nyerere inafuatilia jambo hili bila mafanikio, tunaona kuna hali fulani ya ukiukaji wa sheria, hawa watu wana fedha nyingi.

“Mushi ni mfanyabiashara, ndio sehemu ya wamiliki wa baa maarufu ya Corner iliyopo Sinza Africasana, inasemekana anahodhi maeneo mengi sasa hatujui anayapata kwa njia kama hii anayoitumia au vipi.

“Ni kweli Majura alikuwa rafiki wa John, kuna kipindi mke wake ambaye ni mtoto wa Kawawa, aliweka kontena kwenye kiwanja cha John cha Msasani Na. 778, baada ya mvutano kontena liliondolewa akaja Mushi akaweka likaondolewa tena.

“Hicho kiwanja kimegawanywa na kutoka viwanja viwili, kimoja kina Na. 782 wamegawana Mushi na Majura.”

Chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kueleza kuwa, Manispaa ya Kinondoni iliwahi kubomoa majengo yaliyokuwamo katika kiwanja namba 402, hali ambayo iliifanya familia kuamini kuwa imeshinda vita hiyo.

“Tuliamini kuwa mvamizi ameshindwa, tukaanza kujipanga ili kupaendeleza, sijui jambo gani limefanywa ukienda utashangaa mwenyewe.

“Eneo limeshazungushiwa uzio wa mabati, na ndani kuna biashara inaendelea ya kuuza matofali na saruji,” kilisema.

Chanzo hicho kilieleza kuwa licha ya ucheleweshwaji wa haki hiyo, familia bado inaendelea kufuatilia jambo hilo kwa kufuata misingi na sheria za nchi kama zinavyoelekeza.

MTANZANIA Jumatano ilipomtafuta waziri mwenye dhamana ya Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka simu yake iliita bila kupokelewa.
 
huyu bwana Mushi na pesa zake naona kabug sehemu ya kupora!!
 
Kile unachofanyia wenzako na wewe utafanyiwa, Mumewe alitaifisha mali za watu sasa kibao kimegeuka na bado!
 
wamevamia pote sasa wanahamia na kwenye Familia ya mzee Kweli Pesa ndo kila kitu.
 
Mama Maria Nyerere adhulumiwa viwanja
MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria amedhulumiwa viwanja vitatu tofauti mjini Dar es Salaam. Hali hiyo, imesababisha kuwapo na mgogoro mkubwa kati ya familia ya Nyerere na watu ambao wanadai wameuziwa viwanja hivyo miaka kadhaa iliyopita. Viwanja hivyo ambavyo vipo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kimoja kipo Mikocheni ‘B’ Plot 402 Block C na kingine kipo Msasani Beach Namba 778, ambacho kinadaiwa kugawanywa kwa watu wawili.

Viwanja hivyo, vinadaiwa kuvamiwa na mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, Paul Mushi na mkwe wa Hayati Rashid Kawawa aitwaye Issa Majura Mshangama.

Habari za uhakika kutoka ndani ya familia hiyo, zilizothibitishwa kwa MTANZANIA Jumatano na nyaraka mbalimbali, zinasema kutokana na hali hiyo, Mama Maria amelazimika kuiandikia Serikali barua akitaka msaada wa kurudishiwa viwanja vyake.

Katika nyaraka hizo, zinaonyesha viwanja hivyo ni mali halali ya mtoto wa tatu wa Mwalimu, John Nyerere.

Katika barua yake ya malalamiko kwa Kamishina wa Ardhi ambayo Mama Maria aliiandika Mei 28, mwaka huu inasema; “kijana wangu, John Nyerere ni mmiliki halali na kwamba ana vielelezo kamili vya kisheria.

“Ofisi yako ilimpa Letter of Offer ambayo anayo mpaka sasa. Lakini ameshindwa kujenga katika eneo hilo kwa sababu ya uvamizi wa nguvu wa mtu aitwaye Paul Mushi, ambaye ameweza kuhodhi kiwanja hicho kwa miaka mingi, bila kujali au kuogopa sheria za nchi.

“Kwa vile mwanangu, John anaumwa na hawezi kutetea haki yake dhidi ya mvamizi huyo, nathibitisha kuwa John amemuomba na kumteua George Francis Mlawa ambaye ni mwanasheria, amsaidie kupigania haki hiyo iliyo wazi, lakini anazuiwa kuipata.”

Nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa Machi 12, mwaka huu, John alimuandikia barua Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, akikana kufanya mauziano ya kiwanja Na.778 kwa Issa Majura.

Sehemu ya barua hiyo inasema: “Kwanza kabisa nakana kufanya mauziano na ndugu (Issa Majura), kiwanja changu sijakiuza kwa mtu yeyote yule, kama kuna mtu anadai kuwa nimemuuzia anadanganya, naomba aitwe na mimi nije mbele yako athibitishe jinsi nilivyomuuzia kiwanja hicho.

“Ninachokumbuka, ndugu Majura alivamia kiwanja changu baada ya kumuondoa kwenye kiwanja hicho, hajarudi tena mpaka ninapopata taarifa kutoka kwenye ofisi yako kwamba kauziwa kiwanja changu,” ilieleza barua hiyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo, John aliiomba manispaa impatie nyaraka zinazothibitisha mauziano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo.

Miongoni mwa nyaraka hizo, ni pamoja na nakala ya hati ya makubaliano ya mauzo (Deed of Transfer, Sales Agreement), Stakabadhi za kodi za Serikali zilizolipiwa, barua ya toleo aliyopewa Majura na kodi ya malipo (Capital Gain tax) alilipa nani.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya familia hiyo, zilieleza kuwa manispaa hiyo hadi sasa haijatoa nyaraka hizo.

Pamoja na wavamizi hao kuendelea kuhodhi viwanja hivyo, familia bado inaendelea kulipia gharama za ardhi kila mwaka, huku wanaotumia rasilimali hiyo ni wengine.

Chanzo cha habari kilieleza kuwa: “Kwa muda mrefu familia ya Nyerere inafuatilia jambo hili bila mafanikio, tunaona kuna hali fulani ya ukiukaji wa sheria, hawa watu wana fedha nyingi.

“Mushi ni mfanyabiashara, ndio sehemu ya wamiliki wa baa maarufu ya Corner iliyopo Sinza Africasana, inasemekana anahodhi maeneo mengi sasa hatujui anayapata kwa njia kama hii anayoitumia au vipi.

“Ni kweli Majura alikuwa rafiki wa John, kuna kipindi mke wake ambaye ni mtoto wa Kawawa, aliweka kontena kwenye kiwanja cha John cha Msasani Na. 778, baada ya mvutano kontena liliondolewa akaja Mushi akaweka likaondolewa tena.

“Hicho kiwanja kimegawanywa na kutoka viwanja viwili, kimoja kina Na. 782 wamegawana Mushi na Majura.”

Chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kueleza kuwa, Manispaa ya Kinondoni iliwahi kubomoa majengo yaliyokuwamo katika kiwanja namba 402, hali ambayo iliifanya familia kuamini kuwa imeshinda vita hiyo.

“Tuliamini kuwa mvamizi ameshindwa, tukaanza kujipanga ili kupaendeleza, sijui jambo gani limefanywa ukienda utashangaa mwenyewe.

“Eneo limeshazungushiwa uzio wa mabati, na ndani kuna biashara inaendelea ya kuuza matofali na saruji,” kilisema.

Chanzo hicho kilieleza kuwa licha ya ucheleweshwaji wa haki hiyo, familia bado inaendelea kufuatilia jambo hilo kwa kufuata misingi na sheria za nchi kama zinavyoelekeza.

MTANZANIA Jumatano ilipomtafuta waziri mwenye dhamana ya Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka simu yake iliita bila kupokelewa.

Mama Maria Nyerere adhulumiwa viwanja
 
Safi sana na ipo siku wamdhulumu na Ndugai

Ndugai hana kitu ni mavi kunuka tu yeye anawekeza kwa wanawake alikuwa na mwanamke wake mchaga wa ujanani alipopata ubunge akaongeza mwingine mpare, ana shell pale Kongwa na kibanda kule kijiji cha Ikowa karibu na charinze nyama. hana upeo wa kuwekeza miradi mkubwa mkubwa ila chini anauwezo mkubwa sana kiasi hajui hata idadi ya wake zake.
 
Kama hata ya familia baba wa taifa inafanyiwa hivi, vipi kwa sie akina kapuku.?
 
Kile unachofanyia wenzako na wewe utafanyiwa, Mumewe alitaifisha mali za watu sasa kibao kimegeuka na bado!
Acha hizo, mumewe alitaifisha: maana yake alivifanya kuwa vya Taifa sio alijibinafsishia, hizo mali alizotaifisha nyerere ndio zilizomfanya kikwete na Lipumba wasome mpaka vyuo vikuu bure. Sasa kibao kipi kimgeukie maria nyerere?
 
Ndugai hana kitu ni mavi kunuka tu yeye anawekeza kwa wanawake alikuwa na mwanamke wake mchaga wa ujanani alipopata ubunge akaongeza mwingine mpare, ana shell pale Kongwa na kibanda kule kijiji cha Ikowa karibu na charinze nyama. hana upeo wa kuwekeza miradi mkubwa mkubwa ila chini anauwezo mkubwa sana kiasi hajui hata idadi ya wake zake.
Mkuu unamaanisha kale kakibanda kake ka kuuza nyama pale Mbande..Kimeendikwa Mbande Bucha..ahahahahaa..nina picha zake hapa ngoja nitupie..
 
inasikitisha!ingekuewa Riziwan anafanyiwa haya serikali ingekaa kimya?
 
Dah
Nasikitika sana kama serekali imemua kucheza Na Familia hii..!!
Kweli hii serekali ya Ccm haifai..!!
 
Ndugai..!! Photo-0108.jpg
 
waliomdhulumu wakibainika kwenye vyombo vya sheria wafukuzwe nchini vinginvyo nitawapiga maombi wafe
 
amedhulumiwa kivipi sasa, mahakama si zipo aende ktk vyombo vya kutoa haki sasa tatizo liko wapi? lakini pia hii tabia ya viongozi na watu maarufu kuwa na viwanja kila mkoa nalo ni tatizo, na vingine wamevipata kwa magumashi,
 
uwezi kujua labda yeye ndio anataka kumuibia mtu,kama uyo mtu ana document zote,mama maria awezi kupata sababu alikuwa mke wa baba wa taifa,haki itatendeka tu sababu walalamikaji wote wana uwezo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom