Mama Kahaba!!!!!

Kaka mwenye tatizo
Kuwa makini sana na ushauri unaopata hapa, akili za mwenzio changaya na za kwako...
Bahati nzuri sana naona wengi wanatoa ushauri mzuri, ushauri wowote unaokuelekeza ufanye maamuzi ya
kumtosa mama ako ni ushauri wa kishetani kabisa.

Hata uamuzi wa wewe kumfuata mother face to face na kudiscuss hii issue sio mbaya, tatizo lake ni approach tu ndio inamatatizo.

Japo hata tunaposema umuombe Mungu, jiulize kwanza Mungu gani?
 
Am speechless here!

Pole sana. Mshukuru Mungu kwa kukufikisha hapo ulipo. Usisahaku kumtii na kumheshimu mama yako, kama maagizo ya Mungu yanavyotutaka. Kisha muombee kwa Mungu. Mungu wetu ni wa ajabu, utashangaa atakavobadilika. Kuwa na Imani. Sema AMINA!
Well said Asprin,
mimi pia nilitaka kumshauri hivyo. Amwombe Mungu tu kwani ni mweza wa yote. Amuheshimu mama na aendelee na maisha yake.
 
holy crap..hamkuandikishana mkataba...mshukuru kwa mchango wake ktk maisha yako ila mwambie hakubaliani na aina ya maisha yake... endelea na maisha yako...sala muhimu!!:eyeroll2:
 
mimi ni kijana(mwanaume) na ni mtoto pekee kwa huyu mama.
Ni mama yangu mzazi na kanilea yeye mwenyewe bila baba, na nikimuuliza baba yangu ni nani hanijibu zaidi tunagombana tu!!!
Kanisomesha vizuri sana bila tabu yoyote wala msaada tena kwenye shule expensive sana though sikuwa najua kazi yake (huko utotoni).
Nimemaliza chuo wandugu!! Nimegundua kuwa kazi ya mama yangu kumbe ni ukahaba na ndiyo kazi iliyonilea, kunivisha, kunisomesha na hata vijigari vya kupigia misele na pia kajenga nyumba nzuuri tunayoishi.
Sasa nina kazi nzuri tuu, na nilipogundua kuwa kazi ya mama ni ukahaba, niliongea na mtu mzima akaongee nae ili aachane na ukahaba ilishindikana, zaidi ya yote alimtukana sana na mie pia nikapata na matusi yangu kiasi.
Pia nikagundua kwanini haelewani na ndugu zake kama dada, kaka, wazazi wake na ndugu wengineo ni sababu ya kazi hiyo na hajali kuhusiana na hilo.
Nishaurini ndugu zangu nifanye nini, kwani kiukweli naona fedheha sana hata raha ya maisha haipo tena kwangu.


kwa kuanza tu hii ni kujiaibisha kwako na kwa mamako na familia yako kwa ujumla\

hata kama mamako alikuwa kahaba ama anaendeelea na ukahaba nadhan kuna watu kwenye familia wanauwezo wa kumsaidiakabla ya kuja kumvua nguo hapa...kumbuka yule ni mamako alikuvua ama kukusukuma toka sehemu hizo hizo za sir na wewe kuitwa leoo hii mwana jf
chunga na mawazo ya watu ila kabla ya kukusaidia ama kutoa maoni nenda ukamwombe mamako radhi kwa huu una......uliofanya hapa..unless uniambie ndugu zako wote wameisha kama ndugu zetu wa kashenye bukoba..lakini natumaini ujafikia kumchafua sehemu kama hii unless uniambie ulimwomba akakunyima....la kukumbuka maishan mwako mama ni mama ..ungetafuta njia gani ya kumsaidia na si kuja jf kumuanika utaishia kumvua nguo mamako...binafsi hata nikitoa mawazo naisi kutoa kwa mtu alielaanika..so nenda omba radhi urudi jf ukiwa safi na topic ya namwomba radhi mama..ook tutakusaidia

pole
 
kaka mwenye tatizo
kuwa makini sana na ushauri unaopata hapa, akili za mwenzio changaya na za kwako...
Bahati nzuri sana naona wengi wanatoa ushauri mzuri, ushauri wowote unaokuelekeza ufanye maamuzi ya
kumtosa mama ako ni ushauri wa kishetani kabisa.

Hata uamuzi wa wewe kumfuata mother face to face na kudiscuss hii issue sio mbaya, tatizo lake ni approach tu ndio inamatatizo.

Japo hata tunaposema umuombe mungu, jiulize kwanza mungu gani?

namwona roho mtakatifu akikutumia
 
Binafsi sina heshima hata chembe kwa single mothers (isipokuwa wajane, waliobakwa na walioachika), sembuse huyo kahaba! Kusema kweli kama ningekuwa mimi mngenilaumu tu, lakini siwezi kuvumilia. Katika hali ya kuwa mtoto 'asiye na baba' au 'asiyefahamika babake' mtu unavumilia mengi katika jamii, sasa ukiongezewa tena na hilo kombora la ukahaba, ni unyanyapaa mbaya sana.

Siwezi kumshukuru mama kwa kunizaa kwa sababu hakuna faida yoyote tunayopata kwa kuzaliwa, kwanza hakuna ushahidi wa lipi bora kati ya kuzaliwa au kutokuzaliwa. Kwa hiyo hilo la kuzaa linamhusu mzazi mwenyewe, ilikuwa choice yake kutokuzaa pia, yeye akachagua kuzaa sidhani kama anastahili shukrani yoyote kwa hilo.

Lakini si wote wanaozaa wanatimiza ipasavyo wajibu unaofuata baada ya kuzaa, nao ni malezi. Kwa hili la malezi nitamshukuru mamangu kwa kunilea, kuhakikisha niko salama, kunisomesha nk. Kwa hilo anastahili shukrani za dhati. Lakini hakuna jema linalofuta ubaya. Kwa hiyo bado nitamlaumu kwa kuniingiza katika mazingira ya unyanyapaa na kunikosesha amani rohoni kila ninapofikiria nina mama kahaba, na hili ningemweleza waziwazi kuwa "mama asante kwa kunilea, lakini unaniaibisha, unaninyima nafasi ya kujivunia mamangu kama wenzangu wenye mama zao wanavyofurahia na kujivunia".
 
Back
Top Bottom