Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,503
- 6,376
Mimi ni kijana(mwanaume) na ni mtoto pekee kwa huyu mama.
Ni mama yangu mzazi na kanilea yeye mwenyewe bila baba, na nikimuuliza baba yangu ni nani hanijibu zaidi tunagombana tu!!!
Kanisomesha vizuri sana bila tabu yoyote wala msaada tena kwenye shule expensive sana though sikuwa najua kazi yake (huko utotoni).
Nimemaliza chuo wandugu!! Nimegundua kuwa kazi ya mama yangu kumbe ni UKAHABA na ndiyo kazi iliyonilea, kunivisha, kunisomesha na hata vijigari vya kupigia misele na pia kajenga nyumba nzuuri tunayoishi.
Sasa nina kazi nzuri tuu, na nilipogundua kuwa kazi ya mama ni ukahaba, niliongea na mtu mzima akaongee nae ili aachane na ukahaba ilishindikana, zaidi ya yote alimtukana sana na mie pia nikapata na matusi yangu kiasi.
Pia nikagundua kwanini haelewani na ndugu zake kama dada, kaka, wazazi wake na ndugu wengineo ni sababu ya kazi hiyo na hajali kuhusiana na hilo.
Nishaurini ndugu zangu nifanye nini, kwani kiukweli naona fedheha sana hata raha ya maisha haipo tena kwangu.