Mama huyu anatumalizia watoto wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama huyu anatumalizia watoto wetu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiroroma, Nov 10, 2009.

 1. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Najua kwamba nchi hii hakuna sheria inayowabana wenye virusi vya UKIMWI kutokuusambaza kwa wengine.

  Hivi karibuni mitaa ya kwetu kuna mama mmoja mwenye virusi vya UKIMWI kwa muda wa miaka kama sita hivi. Anachofanya ni kuhakikisha kuwa mtaa mzima umekumbwa na ugonjwa huo.

  Kwa akina baba sina hakika idadi iliyokwisha kutumbukia kwake, Lakini linaloniogofya saana hata kufikia hatua ya kuandika humu JF ni kwamba sasa anarubuni vitoto vidogo vya shule na kufanya navyo ngono tena kwa kuvihonga hela!

  Hivi majuzi jirani yangu alipata nyepesi nyepesi kuwa mtoto wake wa kidato cha pili anatembea na huyo mama.

  Alimshika na kumtwanga mtoto kikamilifu hadi akasema hadithi yooooote KUMBE MTAA KARIBU WOTE vijana wa umri wake wameshalambishwa libeneke la huyo mama. Kivumbi kuanza kutajana basi kila mzazi amerudi ndani asijue la kufanya, wapo walioenda kupima watoto wao sijapata taarifa wangapi wameathirika au la.

  Sasa hali hii tuifanyeje? Uongozi Serikali za Mitaa una habari hata na mume wa huyo mama ana habari pia naye ni mwathirika.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kiongozi hili suala sijui kama limeshatungiwa sheria, nilisikia kuna plan kama hiyo ila sijui maendeleo yake. Kama bado halijatungiwa sheria ndio hivyo tena vijana inabidi waanze mapema ARV, hakuna la zaidi.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Unaonekana uko RSA, sas sijui hii story ni ya bongo au wapi? Kama ni bongo, basi Ungewatendea haki watanzania kama ungetaja at least mtaa, kata, wilaya nk ili iwe rahisi watu kumfuatilia

  Kuna zaidi ya kata 800 bongo kwahiyo post yako inaweza kutoleta tija mazee
   
 4. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Ni kweli nili join JF wakati nikiwa Lady Brand SA,Sasa hivi nipo Bongo Succa NAJUA UMEISHA UPATA PATA MTAA HUO UKO KONA GANI YA jIJI HILI.
   
 5. C

  CHAUMBEYA Member

  #5
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 15, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Imefikia wakati sasa watu pamoja na wazazi wa watoto hao wavunje ukimya basing on the testmonies za watoto wao they can or rather you all can bring her to the justice ila kwanza mumuaibishe kwa kumtoa hadharani kabla ya kufikishwa mahakamani si unajua tena mahakama zetu anaruhusiwa kujifunika kwa mtandio usoni!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani hebu nendeni haraka kwenye vyombo vya usalama mtoe hii report ili waanza upelelezi juu ya hili na kama lina ukweli wachukue sheria fasta kabla kizazi hakijaendelea kuteketea
  kuna watu wana roho za kinyama hapa duniani looh
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kwa hili nashukuru umeweka mtaa, sasa nashauri, nikiwa kama mdau wa vita hii, tuandae pendekezo kwa uongozi wa mtaa, at the same time tumtege na tujipe wiki mbili tumalize kazi

  dont be surprised if you find my PM

  Tusikubali huyu shetani atuulie vitoto vyetu aisee
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mtaje jina na mtaa tulifanyie kazi
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi nashauri haraka sana weka mambo hadharani, Tuache USIRI, taja jina lake, mtaa na hata nyumba namba. Kwani kuwaficha watu kama hao ni kuliangamiza Taifa. Tusimwonee aya
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  na kweli huyu bibie awape jina kama ni kweli haina haja ya kuficha ufisadi huu wa mapenzi

  na hawa watoto nao loh kwanini wafate jimama ktk umri mdogo kizazi kinaendelea kupotoka tu
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  NI kuwa hawa watoto wamerubuniwa, na kama nimemuelewa mtoa mada huyu mama ajenda yake ni kuusambaza huo ugonjwa.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Umri wa mtu anayerubuniwa ni upi? Maana kulia u-victim lazima kuendane na kuwajibika wajameni.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  eeh form two wanarubuniwa ni tamaa ya mapenzi katika umri mdogo
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Shukran kiongozi,


  Hii sheria ilivyokaa imekaa ki-subjective sana, halafu utatumia kigezo gani ku-establish A alipata ngwengwe kwa kutoka kwa B na sio C au kinyume chake?

  Halafu hiyo adhabu yenyewe ya miaka 5-10 jela inaendana kweli na taathira anayoiacha mkosaji?

  Tupo mwaka 2008+ lakini bado tu!, hivi kwanini sheria zetu ni vituko kwa kiasi hiki?
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni sheria bubu kwa kweli si unakumbuka mkuu wa nchi alivyopigaga chenga juu ya tuhuma za Mr. RED? Alisema yeye mwenyewe mkulu alishawahikusikia kuwa kuna mtu kama huyo anayeambukiza but kama kuna mtu mwenye ushahidi wa kutosha basi aupeleke kunakohusika ili mtuhumiwa akamatwe! Wapiii mbona bado anadunda tu barabarani except kwa kosa lingine mbadala?
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nashangaa..

  Hii sheria imekaa 'kutishia nyau' zaidi kuliko kuzingatia ukweli unaoweza kuhakikishwa kitaalam.  Kwa mfano hapo utaithibitisha vipi intention ya mtu? Je, alipoenda kupima na kugundulika ameambukizwa tukishindwa kupafahamu huyu mtu si anakuwa huru?

  Je, kwenda hospitali kupekua mafaili ya wagonjwa sio kupingana na ethics za utabibu? etc etc

   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni mbaya sana, inabidi mtoa mada awe mstari wa mbele kulishughulikia hasisubiri serikali ya mtaa au kuu au mumewe huyo FISI kulishughulikia. Play your part Kiroroma
   
 19. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada inabidi u-play role yako kumkomesha huyo fisi na sio kusubiri serikali ya mtaa
   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ....by the way wewe Kiroroma unazungumzia mtaa gani, maanake nasoma location yako umeandika uko Lady Brand RSA? Ni hapa Bongo au maana naona watu wameanza kujadili sheria zetu na kauli za Rais wetu. Isije kuwa uko ng'ambo
   
Loading...