Jay_the_analyst
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 206
- 151
- Thread starter
-
- #41
Asante.. nashukuru brother kwa ushauri.mkuu i think umesoma katikati ya mistari na kuelewa tatizo liko wapi...
1- mama anahofia chaguo la mwanawe na kwa vile ni first born tena wa kichaga....hapendi atoe boko. kwa wachaga mtoto wa kwanza wa kiumme "mmbele" huwa ndio symbol ya ukoo na familia pia.....dogo mzazi hataki kuharibu image ya ukoo. dogo unao wajibu wa kuonyesha kwa mama yako kuwa wewe ni kidume na hakuna mwanamke wa kuku-brainwash ukasahau majukumu yako kama kijana wa kiume wa kichaga na hasa wa kwanza..nguzo ya familia.
2- mkurya sio tatizo sana ila umesema ana misimamo kwelikweli....hapa napo naliona tatizo...misimamo kwa mwanamke wa kikury inaitwa "kiburi" kwa watu wa makabila mengine...ndio maana mama anaona huyu mkeo atakuwa dominant kwa vile ni kiburi..na wewe mchaga hujui kupiga na kuchapa kama wanaume wa kikurya....mama anayo haki ya kukutetea mwanawe ila pia wewe unao wajibu wa kumwambia mchumba wako juu ya cultural diferences and perceptions za baadhi ya tabia zake. mama anahofia mpora asije kumchapa vibao akija kukutembelea mwanawe.
3- hili la form 4 nalo ni tatizo kwa mama...nadhani hata kwako baadae linaweza kuwa tatizo kama hutokubali kufanya yafuatayo...muendeleze kielimu atleast awe na diploma yoyote...pia mueleweshe mama nia hiyo ya kumuendeleza.
Mkuu unaweza kupiga makofi vizuri?Kujibu maswali yako.. nianze na hili.
- nyumbani mimi ndie wa kwanza
-nyumbani tumezaliwa watatu, wakiume wawili ,wakike mmoja
-nimelelewa katika malezi ya baba na mama.. na but mostly mama kwa sababu baba alikuwa hakai nyumban mara nyingi kutokana na kazi yake.
-imani ya mpenzi wangu na mimi viko sawa, kwani wote huwa tunaenda kanisani pamoja.
-mpenz wangu ana swag zankawaida tu.. ni mtu muelewa sana.. alaf mpole but ana msimamo sana.
-mpenz wangu hakai mtaa mmoja na mimi
-kabila lake ni mkuria... mimi mchaga
-familia yangu na ya mpenzi wangu hawajawahi kugombana kwa sababu hawafahamiani na wala hawaja wahi kuonana.
-umri wa mpenz wangu ni 22.
Kila mtu anachaguo lake la moyo.. lakini sasa kama ndio hivyo anataka mwanamke wa kichaga.. na mimi hao nafahamu tabia zao..Mkuu unaweza kupiga makofi vizuri?
Mama anataka upate sweetmangi! Wachaga wengi hua wanapenda ivyoo... SIO WOTE LAKINI
Mkuu naomba kudeclare interest mama yupo right unacho ongea mm kilinitokea 2010 na mbaya zaidi mpenz alikuwa mjamzito wa miez 7 bi mkubwa alichoniambia its similar to urz but its 4years now naamin what she was saying ni true but life lipo na litaendelea mkuuHabari za asubuhi ndugu zangu, natumai mmeamka salama.
Lengo la kuleta hii mada ni kuomba ushauri kwa ajili ya jambo linalo nisumbua kwa muda mrefu.
Mimi ni kijana mwenye miaka 25, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita na namshukuru Mungu maisha yanaenda vizuri. Ndugu zangu nimekuwa kwenye mahusiano kwa miaka miwili na mchumba wangu. Tumesaidiana mengi na ameonesha mapenzi ya kweli kwangu kwani amejitoa kwa mengi nami nampenda sana kutoka moyoni.
Tatizo ni kwamba toka nilipomtambulisha kwa mama, mama ameonesha chuki waziwazi kwake. Nilijaribu kukaa na mama na kuongea nae lakini sasa hana sababu maalumu ya kumkataa.
Niliwahi kumuuliza pole pole lakini akasema kuwa hajisikii amani moyoni mwake kuhusu mchumba wangu. Nikamuuliza kwanini hajisikii amani? Akakosa jibu akanipotezea.
Sasa mchumba wangu ameumia mno kiasi kwamba anataka tuvunje mahusiano baada ya kujua mama hampendi. Kwakweli nimejaribu kila njia katika kusuluhisha hili jambo lakini naona naelemewa.
Ndugu wa mwanamke wananielewa sana na imetokea kwao wamenikubali sana, haswa mama yake na baba yaani wakiniona wanafurahi. Lakini mama yangu mimi hamtaki na hana sababu maalumu ya kumkataa.
Nifanyaje wadau? Naombeni ushauri wenu.
Mama hataki ubebe mzigo. Anajua familia yote itakuelemea wewe.Kuhusu elimu kwa upande wetu. Watu wamesoma sana, wamefika vyuo vikuu. Ila kwa upande wa mwanamke hawaja fika ngazi za juu kielimu.
Na kiuchumi kwa familia yetu , uchumi ni level ua kati.. nikimaanisha si matajiri sana.
Kwa upande wa mwanamke uchumi wao si mzuri.. ni watu wa hali ya chini kias fulani.
Shida ya wazazi wetu hawataki kwenda na mabadiliko ya utandawazi...Kila mtu anachaguo lake la moyo.. lakini sasa kama ndio hivyo anataka mwanamke wa kichaga.. na mimi hao nafahamu tabia zao..
kama bi mkubwa ana interest zake why iwe ngumu kusema?
Siendi kwenda against her... thats why natafuta solution kwa nguvu zote. Because nina hope kuwa anakitu ila hakisemi.Usijaribu, nasema usijaribu kabisa kwenda against mama ama mzazi wako. KUna hadithi nyingi tu za watu walioharibikiwa kwa kutokuwasikiliza wazazi wao, wazazi Mungu kawapa kipawa cha kuona mbali sana kuhusiana na watoto wao. wameshauri hapa wakina uso wa nyoka nadhani ni ushauri mzuri kidogo tafuta mashangazi wako ama mtu ambae mama yako anamuheshimu sana Muombe akaongee na mama kuhusu suala hilo, nenda taratibu kaka usichukulie pupa.
Hapo ndipo mgongano wa mawazo unapotokea. But nini sasa kifanyike?Shida ya wazazi wetu hawataki kwenda na mabadiliko ya utandawazi...
Kwanza pole braza. Lakin ningependa kujua nini kilikutokea...? nataka nijifunze kutokana na story yako. Unaweza kunitumia inboxMkuu naomba kudeclare interest mama yupo right unacho ongea mm kilinitokea 2010 na mbaya zaidi mpenz alikuwa mjamzito wa miez 7 bi mkubwa alichoniambia its similar to urz but its 4years now naamin what she was saying ni true but life lipo na litaendelea mkuu
Nitalifanyia kazi ... lakin braza.. kama anamchukia sasa hivi akiwa hana mimba...? Atamkubali akiwa anayo?mkuu ni kawaida mama kuonyesha (chuki?) wasiwasi kwa mawanamke mwingine anayeingia kwenye teritory yake kwani naye hutaka undivided attention. Usihofu we jifanye kama haujali anza taratibu za ndoa kisha oa.Kisha mpe ujauzito haraka baada ya kujifungua utashangaa wanakuwa maswahiba wa kutosha.Cha kufanya kama unaishi kwa mama yako ondoka haraka katafute sehemu nyingine ya kuishi.Ni usijaribu kumuambaia mchumba wako kwamba mama yako anamchukia, nae ataanza jitihada za kupigania attention yako.
Mr jose.. uko right. I need to dig more deep.. mpaka nipate jibu sahihi ..na niweze kufanya maamuzi sahihiSome times kuna kitu anaweza akawa ameona, muulize vizuri.
kuna wengine baadae mkiwa pamoja likatokea tatizo anakwambia mimi nilishaliona hili ndo maan nikasita. anaweza (anaweza) akawa sahihi. muulize vizuri.