Jay_the_analyst
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 206
- 151
Habari za asubuhi ndugu zangu, natumai mmeamka salama.
Lengo la kuleta hii mada ni kuomba ushauri kwa ajili ya jambo linalo nisumbua kwa muda mrefu.
Mimi ni kijana mwenye miaka 25, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita na namshukuru Mungu maisha yanaenda vizuri. Ndugu zangu nimekuwa kwenye mahusiano kwa miaka miwili na mchumba wangu. Tumesaidiana mengi na ameonesha mapenzi ya kweli kwangu kwani amejitoa kwa mengi nami nampenda sana kutoka moyoni.
Tatizo ni kwamba toka nilipomtambulisha kwa mama, mama ameonesha chuki waziwazi kwake. Nilijaribu kukaa na mama na kuongea nae lakini sasa hana sababu maalumu ya kumkataa.
Niliwahi kumuuliza pole pole lakini akasema kuwa hajisikii amani moyoni mwake kuhusu mchumba wangu. Nikamuuliza kwanini hajisikii amani? Akakosa jibu akanipotezea.
Sasa mchumba wangu ameumia mno kiasi kwamba anataka tuvunje mahusiano baada ya kujua mama hampendi. Kwakweli nimejaribu kila njia katika kusuluhisha hili jambo lakini naona naelemewa.
Ndugu wa mwanamke wananielewa sana na imetokea kwao wamenikubali sana, haswa mama yake na baba yaani wakiniona wanafurahi. Lakini mama yangu mimi hamtaki na hana sababu maalumu ya kumkataa.
Nifanyaje wadau? Naombeni ushauri wenu.