Mama hajawahi kustaafu

Na katika kufanya kazi kwao huko miili yao inakuwa imara ndiyo maana hawaondoki mapema. Sisi wanaume kubweteka tu eti mzee wa kaya kucheza bao siku nzima halafu sigara, sijui pombe kufikisha 70 bahati sana. Hongera zao akina mama [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Una bahati sana mkuu kwa kuwa na mama. Hakikisha unamwangalia na kumtunza sana. Tena wao hawana maneno mengi. Hata kama huna pesa kumjulia hali mara kwa mara. Kumwambia kuwa unampenda sana. Vizawadi vidogo vidogo vya mara kwa mara. Hata kama ni kipande cha sabuni. Na usipitishe wiki bila kusema naye...

Hakuna kitu kinachouma kama kuondokewa na mama. Na siku akiondoka kama mtu hukuwa sawa naye au kama ulikuwa unamchukulia hivi hivi tu aisee utajuta sana. Wapendeni na kuwaangalia sana mama zenu jamani [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…