Mama bado anaupiga mwingi?

Mama D, ni wewe kweli!? Huzuni na majonzi vimeisha? Au umepata uteuzi😂!
 
Anataka kukunwa sasa hivi.
 
Binafsi sikuwahi kuwa shabiki wa utawala wa MWENDAZAKE hususani kwa namna alivyokuwa akitumia nguvu kubwa kuwadhibiti wapinzani wake wa kisiasa lakini upande wa sera za kimaendeleo na uongozi kwa ujumla nadiriki kusema alikuwa chuma tena mwamba kweli kweli..ila kwa huu muda mfupi wa utawala wa mama yangu huyu niwazi taifa langu linapitia kipindi kizito sana sijui nyie wakuu magwiji wa siasa na uongozi mnalionaje hili??mama viatu vimekuwa vikubwa? au apewe muda zaidi baada ya 2025?
 
Tuache kumtegemea "Mtu" badala yake tujikite kwenye "Mfumo" hicho ndicho mimi ninaamini.... Mtu ataondoka... Akiondoka mwenye Falsafa A, atakuja mwingine mwenye Falsafa X - na ni kawaida kabisa kwa binadamu kutofautiana, wala sio ajabu. Ndio maana hakuna Nyerere mwingine, hakuna Sokoine mwingine, hakuna Samwel Sitta mwingine, n.k. Kwahiyo tusitegemee Mama atafanya kama fulani... ni ngumu sana, yeye naye ni binadamu na amelelewa kivyake, ana mtazamo wake, ana maono yake, ana namna yake ya kufanya maamuzi, na ana washauri wake ambao ni tofauti na Mwendazake.

Badala ya kutarajia "Mtu" atatuletea majibu ya changamoto zinazotukabili, nadhani tukubaliane kuwa kuondoka kwa Mwendazake kumetufundisha somo moja kubwa kwamba; tusimtegemee mtu... bali tujikite katika kujenga mfumo imara ambao utamuongoza kila anaeingia bila kujali mapungufu au ubora wake binafsi. Vinginevyo tutaendelea kuimba wimbo huu huu wa "bora alipokuwepo fulani."

Na si mara ya kwanza kutokea: Huenda alipoondoka Mkoloni akaingia Mwalimu, watu huenda walisema "Bora tungeendelea kutawaliwa" - pengine ndio maana akang'atuka! Na yeye alipoondoka akaingia Mzee Ruksa, watu wakasema "Bora.....", na Mzee wa Utandawazi nae huenda aliambiwa "Bora alipokuwepo...." mpaka leo tunaendeleza huo mnyororo. Swali ni, tutaendelea kulaumu mpaka lini?

Au tuchukue tu busara za Nyerere kuwa "Ukizoea kula nyama ya mtu, huwezi kuacha abadani!"
 
Usituulize sisi waulize "waliomuua"
Na kama ulimpenda sana kufa ili uzikwe pembeni ya kaburi lake kama alivyoshauri Ayatollah,,
 
Great Thinker!!
 
Na hawezi kurudi..kazi iendelee na mama yenu
 
Acheni kufananisha jiwe na vitu vya..........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…