Mama awang’ata wanawe, mumewe aomba msaada asema wako hatarini

Mama awang’ata wanawe, mumewe aomba msaada asema wako hatarini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya firauni! Ndivyo unavyoweza kusema kwa mama huyu wa wato wawili anayefahamika kama Mama Theresia (18), mkazi wa Kata Maweni, Mtaa wa Jaribu Tena, jijini Tanga ambaye huwang’ata watoto wake kisha kuomba radhi kwa mumewe.

Hali hiyo imemfanya mume wake, Patrick Peter (75) kuomba msaada kwa wasamaria wema na serikali kumsaidia kuwachukua watoto wake wawili ambao wako hatarini kutokana na mama yao kuwafanyia vitendo vya ukatili.

Aidha, Mzee huyo amesema mke wake huyo waliyedumu kwa miaka mitano hupandisha hasira na kufanya matukio yasiyo ya kawaida na baadaye kuomba radhi.

Akisimulia mikasa hiyo ya mkewe, Mzee Parick amesema mama huyo amekuwa akifanya vitendo vya ukatili kwa watoto hao kwa kuwang’ata na meno na kuwasababishia majeraha makubwa mwilini.

“Hata mimi amewahi kunishikia panga akataka kunipiga nalo, ila niliwahi kumshika, hivyo unaweza kuona namna gani mama huyu amekuwa tishio kwa familia,” amesema.

Kwa upande wao majirani wa Mama Theresia, wameshangazwa na vitendo vya mama huyo na kuomba serikali kuwapatia msaada watoto hao kwa kuwahamisha kutokana na maisha hatarishi wanayoishi na wazazi wao.

“Sisi tulikwenda kujumuika msibani hapo kwa Mzee Patrick aliyefiwa na mtoto wao mchanga, baada ya kumaliza shughuli za mazishi ndiyo ndugu mmoja akasema jamani humu ndani pia kuna kabinti kadogo kana majeraha makubwa mwilini na amedhoofika sana anaweza kupoteza maisha tusipochukua hatua,” amesema mmoja wa majirani.

Hata hivyo, mtoto huyo wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitano, ameonekana kudhoofika kutokana na vidonda vikubwa vinavyoonekana dhahiri ni alama za meno.

Aidha, mtoto huyo aliyefariki Jumanne wiki hii, imedaiwa kifo chake kilisababishwa na mama huyo kumpa uji mwingi uliosababisha mtoto huyo wa wiki mbili kuvimbiwa na kupoteza maisha.

Akizungumzia suala hilo, Mama Theresia mwenyewe amekana kuwangata watoto wake na kwamba amedai huwa wanaanguka wanapojifunza kutambaa hatua inayowasababishia kupata majeraha hayo.

Mtanzania
 
Umeona hizo age na wewe ? Halafu wameishi miaka 5 . Au ni sisi tu ndio tumeshangaa labda huko Tanga binti miaka 13 ni wife material [emoji1495][emoji1495][emoji1495][emoji1495]
Nimewaza labda miaka 18 tangu aolewe...awe mama..?
 
Kweli vituko havitakaa kuisha chini ya jua.

Yani binti wa miaka 18 ana experience ya miaka mitano ndoani wakati kuna mama zake wana miaka 40+ na mpaka sasa hawajawahi kuonja ladha ya ndoa hata ya mkeka kwa walau dakika kadhaa wameamua kuwa na vimarioo tu
 
Kwa Tanga sishangai. Tanga ndo mapenzi yalipozaliwa buana, ila hii inatakiwa iingizwe kwenye records, babu wa miaka sabini ameoa binti miaka 13
 
Duuuuhh

Mume miaka 75..
Mke miaka 18
na ameishi nae " miaka 5.
means alipomuoa.. Mke alikuwa na miaka 13 ""
na mume alikuwa na miaka 70 ..
na kazaa nae Watoto wawili ndani ya miaka 5
tamaa nyingine hizi "" Yaani unaumri wa Miaka 70 halafu bado unazalisha "" hao Watoto wako unataka waje kuishi katika Mazingira yapi " usikute hapo wanaishi maisha ya dhiki mnoo"" so Hawa Watoto watalelewa na nani wakati katika huo umri wa miaka 75 mtoa roho ameshaanza kukunyapia nyapia "" masikini dada wawatu bado mdogo " lakini ataingia kwenye maisha ya ujane "" halafu hapo unakuta anatokea mtu anasema kuwa wazazi huwa hawakosei "" !! wazazi huwa hawakosei " wakati wamemuoza mtoto mdogo kiasi hicho"" kwa mtu ambaye nimzee "kiasi hicho.? "" wazazi huwa hawakosei wakati lijitu lizee limekwenda kukaowa kabinti kadogo ambacho nisawa na kitukuu chake ""
?

usikute huyo binti kapatwa na kichaa kilicho sbabishwa na kuwa over stress baada ya kushurutishwa kuolewa na hilo lizee"" haiyumkiniki " mtu timamu awe anatenda vitendo kama hivyo'"'
hilo lizee na wazazi wa huyo Binti wote wafungwe "" PUMBAVU
 
Ninaomba mamlaka husika ziwahoji

Huyo mzee na

Wazazi wa huyo mwanamke

Maana hapa nimepata uchungu uliopiliza kumbe kuna watu wanafanyiwa ukatili kiasi hiki bado tunaambiwa watoto wa kike wako salama

Hapa nawaza kwa sauti tu
 
yaani "" mpaka nimestaajabu...wajua kuna mambo mengine huwa yanatokea mpaka unajiuliza hivi " hao watu wanaishi duniani kweli ..yaani bila hata haya " wazazi wa huyo Binti " wanashiriki kufanya kitendo cha udhalilishaji jinsia kama " hicho"

AMA KWELI " UKOSEFU WA AKILI NIMZIGO
 
Back
Top Bottom