Mama au mke?

Mama au mke?

Nenda taratibu ndg yangu,akili ni nywele na kila mtu ana zake. Wapo pia kina dada wanaopenda sana kujua kipato cha waume zao si kwa kujenga ila ili akubane,humu utapata ushauri ila finally mwamuzi ni wewe. Doooh bora umeuliza niliyoyategemea ndio nimeyasikia.

Yap ndio maana tumemshauri na tumemwambia achanganye na zake. Na tumemwonyesha mwisho wa hayo anayofanya. Still yeye ni mwamuzi wa mwisho katika hili. Hatumjui hatujui, na tunaamini atafanya kile ambacho moyo wake utaona ni sahihi. Be blessed!!
 
Aki i dont know what to say to you br. Najaribu kukuelewa lakini nina maswali kama matatu ya kukuuliza.

1. Mahusiano yako na mkeo yakoje
2. Mahusiano ya mkeo na mama yakoje.
3. Na mahusiano ya mkeo na biashara zako yakoje.

Ukishajiuliza maswali hayo yote na ukapata majibu kwamba ni mazuri. Step no 2 jadiliana na mkeo kuhusu swala hilo. Umuulize is she confortable to handle your business knowing that she is still in college (according to what you said). If yes let her run the business, without involving your mother. If no now you can go to your mom.

Kama sivyo unajipalia makaa kwa ndoa yako.

Jiulize angekuwa ni yeye anaenda masomoni na akamwachia mama yake shughuli zake. You know how you could have felt. So fanya kile chenye ungetaka ufanyie.
All the best Bro.
 
Kwanza pole kwa majereha uliyoyapata kwa jamaa zako, hadi ukafikia kutomwamini mtu unayelala naye kitanda kimoja. Naomba kuuliza tena. Wewe unamwamini mama yako kuliko unavyomwamini mkeo?? Yani moyo wako unafunguka kwa mama yako kuliko kwa mkeo?? Sio lazima ujibu hapa jijibu hata moyoni. Halafu fikiria maisha ya mkeo wakati ambapo labda Mungu ameamua kukuita kabla yake.

Mwenzako anafikiria maisha ya mama yake, wanaume wengine bwaba, HOVYOOOO! Hili ni tatizo kubwa sanaa lililopo kati ya wanaume wengi na mama zao. Unakuta mtu kaoa, lakini kwa sababu kabla hajaoa alikuwa close na mama yake, na kuwa mama yake alikuwa ndiyo mshauri wake, utakuta hata mambo yan kwenye ndoa yake anayeamua ni mama. Akipata changamoto anampelekea mama. Wewe unajua kichwa ni yeye, kumbe mama anaiendesha familia kwa remote control. Ndoa za hivyo huwa hazidumu, zinawatesa wanawake mno. Huyo mama ananyumba yake, aendeshe ya KWAKE, huyu bibie amwache naye aendeshe nyumba yake na mume wake. Kwa kweli nimekasirika sana. Wanaume fungukeni macho, tunajua kuwa mnapendana na mama zenu, lakini ujue mkeo ni mwenza wako wa maisha!

Mfano ukiwa hoi hujiwezi atakayekuhudumia ni mama yako? Ukiumwa hoi usiku wa manane atakayekupa msaada wa jkaribu ni nani? Ukipata matatizo ya kikazi atakayekubeba mjini hapa kwa vijisenti vyake hata kama ni vidogo ni mkeo! Huyo mama yako hatakuwa na msaada wowote, yeye ataangalia watoto wake wengine wenye vipato. Mtoa mada unaonekana una mfumo duni, jifunze kumheshimu mwanamke, ana uwezo mkubwa kuliko unavyodhani si tu kununua mapambo ya ndani kama unavyodai. FUNGUKA PLEASE UNAAIBISHA
 
Back
Top Bottom