Mama au mke?

.....hivi bado wanaume wa aina hii wapo ktk dunia ya leo!! Yaani unamficha mkeo mapato yako ili iweje? Eti ndoa ina mwaka....mkeo alitakiwa ajue mapato yako tokea kipindi cha uchumba wenu. Ina maana nyie kama wanandoa hampangi mipango yenu pamoja ya maendeleo? Hebu mkabidhi mkeo na sio mama,na kama unamuona hajui matumizi inabidi umfundishe....je umeshaandika mirathi wewe? Au nayo utamuandika mama urithi badala ya mkeo na watoto.
 
Naam Pretty hapo ni ukweli mtupu.
 
Thenx Lizzy, LD, Carmel, kwa ushuriwen mzuri, mpaka jama kaelewa hi ndio JF nawakubali. hatamimi nimepata kujua, bongo wanaume wengi wanawaficha wakezao biashra zao na vipato, Asanteni
 
Ok,ok punguzeni jazba wapendwa najua ni topic inagusa. Please twendeni pole pole.
Nampenda sana mke wangu mpaka watu wapumbavu wanasema nimelogwa. Hii ya wife ku run shughuli naona itampa wakati mgumu kwa kasociety kangu kakijinga kanakozua hayo mambo ya kulogwa. Halafu hatuishi kwenye kisiwa hii society ikimkataa wakati sipo ataishije?
VoA asante I am thinking or at least i'm thinking that i'm thinking. Get it? Lol.

Mna watoto? Ikitokea ukafia huko hako ka society katampa share yake ambayo wewe ulishindwa kumkabidhi au unataka anyanyasike milele? Be a man.
 
Thenx Lizzy, LD, Carmel, kwa ushuriwen mzuri, mpaka jama kaelewa hi ndio JF nawakubali. hatamimi nimepata kujua, bongo wanaume wengi wanawaficha wakezao biashra zao na vipato, Asanteni

Thank you Kasopo, tunamshukuru Mungu ameelewa, na Niimani yetu atabadilika,
kwa furaha ya ndoa yake, nafsi yake na nafsi ya mke wake.
Halafu na jamii yake itajifunza kitu.
Ashukuriwe Mungu.
 
Nyamgluu, naamini kuwa ulimuoa mke wako ukiwa unampenda na kwa sababu hiyo sioni sababu ya yeye kutofahamu kipato chako. Hapa ndipo wanaume tunafanyaga makosa kwa kuishi katika ndoa huku hatujadhamiria/kuamua kikwelikweli au kwa mashaka kuwa inawezekana tukaachana.

Mkeo ni sehemu yako na ndiye anayepaswa kuwa mtu wa kwanza wa karibu sana kuliko mtu yeyote. Kama ni siri yeye ndiye anayepaswa kujua asilimia kubwa ya siri zako. Jitahidi usiishi na mke kama girl friend tu wa kawaida kana kwamba hamjafunga ndoa.

Jaribu kujiuliza kama baba yako asingempenda mama yako na wakakaa vizuri nyumbani je wewe ungeweza kupata malezi uliyoyapata? Kwa sababu hiyo unapaswa kumjali mke wako na kuhakikisha mnashirikiana katika mipango yenu. Kama kuna mahali ana udhaifu muelekeze/mjenge uwezo na naamini ataweza.

Sikubaliani na suala la kusema yeye ana hela zake au akaunti yake na mimi ya kwangu na kuwa mahitaji yote natoa. Kinachopaswa kufanyika ni kuwa pesa zako ni zenu na pesa za kwake ni zenu pia, kaa pamoja kila mwezi mkubaliane mnazitumiaje.

Mimi na mke wangu tuna akaunti tatu katika benki tatu tofauti, moja inatumia majina yangu, ya pili inatumia majina yake na ya tatu ni joint account ya mimi na yeye. PIN numbers/Namba za siri za akaunti zote tatu kila mmoja anafahamu na kulingana na hitaji lililopo nyumbani yeyote anaweza kukimbia benki na akaleta hela. Hivyo hakuna siri kwetu kwani mipango ya mwaka/mwezi tunakaa pamoja tunakubaliana. Nikisafiri kwenda mahali ambako kadi haitatumika naacha nyumbani na mke wangu anabaki kama mkuu wa familia kusimamia mambo yote.

Namalizia kwa kusema kama unampenda mkeo, mshirikishe kipato chako na mipango yako, amini kuwa anaweza na kama kuna udhaifu msaidie na umwezeshe. Kwa kufanya hivyo utafurahia maisha ya ndoa na mtakuwa mnaweka msingi mzuri kwa watoto wenu.
 
Hii mada ni tamu sana!

SASA NAOMBA TUIGEUZE IWE "VICE VERSA OF THE fACTS" ili tujadili na upande wa pili, yaani badala ya kuwa mwenye Mshahara na anayekwenda kusoma ni mme, pawe ni mke.
 
Hii mada ni tamu sana!

SASA NAOMBA TUIGEUZE IWE "VICE VERSA OF THE fACTS" ili tujadili na upande wa pili, yaani badala ya kuwa mwenye Mshahara na anayekwenda kusoma ni mme, pawe ni mke.

hata mimi nilikuwa nawazo hilo mkuu !
 
Hii mada ni tamu sana!

SASA NAOMBA TUIGEUZE IWE "VICE VERSA OF THE fACTS" ili tujadili na upande wa pili, yaani badala ya kuwa mwenye Mshahara na anayekwenda kusoma ni mme, pawe ni mke.

CNJR, mi nadhani kuigeuza haitanoga kwa sababu tutkuwa tunasema uongo. Yani tuna act tu, hatumsaidii mtu wala nini tunajifurahisha tu labda. Lakini akitokea mwanamke ambaye analeta tatizo kama hili atashauriwa kutokana na mahitaji yake na wakati husika. So kwa leo nashauri msaidieni huyu kaka tu!!
 
Hahahaha LD kumbe swala likigeuza haliwi straight forward tena. Mbona hamsemi kua mke nae amwachie mume ila eti inabidi ijadiliwa.
Umepoteza busara hapo.
 
Hahahaha LD kumbe swala likigeuza haliwi straight forward tena. Mbona hamsemi kua mke nae amwachie mume ila eti inabidi ijadiliwa.
Umepoteza busara hapo.
Secondly wengi wenu mnashauri ajue mshahara wangu mh hapana na nitawapa sababu vizuri nikiwa kwa pc not via mobile.
 
Hahahaha LD kumbe swala likigeuza haliwi straight forward tena. Mbona hamsemi kua mke nae amwachie mume ila eti inabidi ijadiliwa.
Umepoteza busara hapo.

Samahani mkuu, nilikuwa namaanisha hivi? Kuifanya hii thread kuwa kinyume itaharibu maana ya thread, nikiamini kwamba bado kuna watu wanamawazo na ushauri mzuri tu juu ya hili swala lako. So libaki kama lilivyo lakini ikija kesi inayomhusu mwanamke? Tunamshauri na yeye kama yeye. Asante kama utakuwa umenilewa.

Halafu kwa bahati nzuri, naye akawa amegundua hilo akaanzisha thread inayomhusu mwanamke, na nimetoa maoni yangu kule. Hebu itembelee kama bado hujaiona.
Barikiwa sana jpili njema.
 
Habari wakuu. Naomba tubadilishane mawazo kwa hili.
Naenda kusoma nje. Mshahara wangu utaendelea kuingia kwenye akaunt yangu ambayo nayo ndio naitumia kwa biashara zangu. Sasa navyoondoka sijui kadi nimpatie mama au mke kwa ajili ya kuendelea ku run shughuli na matumizi mengine. Wife hajui kipato changu taslimu na ni vizuri,ila kwenda kuomba kwa mama inaweza ikawa kero.
Mwalioneje hili?
dah! Hili lisredi nimelichelewa... Lizzy ld, carmel mmemshauri vizuri.

Hivi mtu unaeshare nae kila kitu hadi hisia lakini bado umuamini!!!!!!
Halafu unasema wanawake wanadanganyika lakini katika wanawake hao mama yako umemtoa.
 
Ok,ok punguzeni jazba wapendwa najua ni topic inagusa. Please twendeni pole pole.
Nampenda sana mke wangu mpaka watu wapumbavu wanasema nimelogwa. Hii ya wife ku run shughuli naona itampa wakati mgumu kwa kasociety kangu kakijinga kanakozua hayo mambo ya kulogwa. Halafu hatuishi kwenye kisiwa hii society ikimkataa wakati sipo ataishije?
VoA asante I am thinking or at least i'm thinking that i'm thinking. Get it? Lol.

Unajisikiliza lakini unapoandika haya maneno yako? kama kweli unampenda huyo mkeo kwa kiwango unachosema, nini kinakufanya usikilize ya hao nje? yaani kama mimi ndo ningekuwa mkeo, ukimwachia kadi mama yako sitakaa niende kuomba hela kwako, hata nikiwa na shida kiasi gani, huko ni kudhalilishana
 
Habari wakuu. Naomba tubadilishane mawazo kwa hili.
Naenda kusoma nje. Mshahara wangu utaendelea kuingia kwenye akaunt yangu ambayo nayo ndio naitumia kwa biashara zangu. Sasa navyoondoka sijui kadi nimpatie mama au mke kwa ajili ya kuendelea ku run shughuli na matumizi mengine. Wife hajui kipato changu taslimu na ni vizuri,ila kwenda kuomba kwa mama inaweza ikawa kero.
Mwalioneje hili?

Eti umesemaje hapo kwenye red??????? Aisee nimesikia hasira hata kuchangia nimeshindwa kila la heri
 
Nenda taratibu ndg yangu,akili ni nywele na kila mtu ana zake. Wapo pia kina dada wanaopenda sana kujua kipato cha waume zao si kwa kujenga ila ili akubane,humu utapata ushauri ila finally mwamuzi ni wewe. Doooh bora umeuliza niliyoyategemea ndio nimeyasikia.
 
Mke mambo yote bwana usijali kabisa atawakilisha tu. Mama nae si ana mumewe we kaka
 
Back
Top Bottom