Malow-income wamevamia Mbezi Beach!

Status
Not open for further replies.
Kwani mbezi beach inaanzia wapi na kuishia wapi hadi unashauri Sumatra waondoe daladala,,,mbezi mnaishi maskini watupu, njoo kule mbweni na ununio


Hata huko ni swala muda tu kabla hapajafurika!
 
At least the low income earners are working hard to make an honest living and live their dreams.

They are not arrogant sons and daughters of corrupt leaders and illegal businessmen typing from the balcony of their parents homes.

Much respect to them.
 
Kule Moshi mkoani Kilimanjaro kuna mitaa ya kawaida sana kuliko hata Masaki, Oyster Bay na Mbezi Beach,
Hata barabara zao ni vumbi na watu ni wa kipato cha kawaida sana na wanafanya sana biashara mtaani tena nje.
Lakini usafi wa wale Wachagga huwezi kulinganisha na O'Bay, Mbezi au Upanga kwenye High Income (Acha kuleta utoto wako wako hapa)
Moshi Ukitupa hata vocha au hata kutema mate chini utakiona cha mtema kuni; Utalipa faini ya 50000 na wanaweza kukufanyisha usafi siku nzima. Hapa ndiyo utakuja kujua kwamba tatizo siyo watu, tatizo ni kutotilia mkazo Sheria (By Laws) kwa viongozi na wananchi kwa ujumla wao.
Watu kama wachafu, wanaacha mifugo hovyo na wezi kamateni pelekeni polisi. Lazima wengine watabadilika tu....

Moshi kuna Middle- Class au Working class lakini ni Wasafi hadi walishawahi kuwa wa kwanza Afrika,
Tena hata wizi wa kijinga hakuna kabisa kama wewe unavyoleta hizi porojo zako za kipumbavu hapa.
Nilivyoenda Iringa sikuamini macho yangu kwa Usafi wa pale mjini hasahasa Sokoni pale Miyomboni.
Wahehe wanakuwa wasafi kwasababu Sheria zinalazimisha mtu awe msafi.

Unamsingizia Mzee Nyerere hapa: Hakuwa na mawazo ya kipuuzi kama haya. (Alikuwa ni Mjamaa sugu)
Hivi unajua hata kwanini Mzee Nyerere aliwapeleka viongozi wengi kule Masaki na O'Bay ??
Au wewe unahisi ni kwa ajili ya kipato na Ubaguzi kama walivyofanya Makabulu kule Afrika Kusini.
Wewe una akili za Kibaguzi na isitoshe wewe ni kabulu Mweusi ambaye unajihisi kusema hivi ndiyo Uzalendo.

Leo mtaanza kusema wamewavamia kwenye mitaa mtawafukuza,
Kesho mtasema Shule za Feza, Babro, Kaizirege na nyinginezo zisishushe ada kwasababu watoto wa masikini watakuwa wengi na kufanya Enrollment ya watoto wenu kuwa ngumu hivyo wakataliwe. Hamtaishia hapo, mtaenda hadi makanisani, mtakuja mahospitalini na mwishowe majikuta tayari mshatengeneza JIM CROW SOCIETY au APARTHEID SOUTH AFRICA.

Hii nchi siyo ya baba yako,
Watanzania wataishi popote wanapotaka (Haki yao kikatiba)
Kama wewe unajihisi ni High Income nunua Kisiwa au Kijiji kama wakina George Clooney au Johnny Depp.
Kwanza siku hizi HIGH INCOME wanaishi kwenye Yatch na wanaondoka na Helikopta kila siku iiendayo kwa Mungu.
Wewe unajenge kijumba cha Mil 80 na vihela vya kubadilishia mboga na kagari unajihisi HIGH INCOME. (STUPID)

Huu ubaguzi wako haukufikishi popote pale bwana mdogo.
Nakushauri uache mara moja na ubadilike na naendelea kukushauri kama siku zote (Tembea uone)
 
Ukizikwa hauozi nini ukiwa mkazi wa huko?!
 
Rudi ulikotoka kama una jehuri.. kilichokuleta nini!
 


Acha kujidanganya Bianadamu is unequal creature, Dunia nzima inalitambua hili, swali langu kwa nini ma low income hawavamii O’bey, Upanga au Masaki?
 


Lkn wanaweza kuishi Sinza, Tabata au hata Kinondoni, huko kote kulijengwa kwa ajili ya middle mpaka low income!
 
Mbezi beach shamba la mpunga ndiyo hii unayoiongelea au kuna Mbezi beach nyingine ambayo siifahamu?
 
Malcom Lumumba huyo dogo Barbarossa ana akili fulani hivi za kitoto,ubaguzi na itikadi kali fuatilia nyuzi zake nyingi na comments zake utanielewa .Akiendelea hivyo hivyo atakuwa kichaa
 
Nakumbuka nilivyohamia dar kwa ajili ya masomo,,,kila mtoto mkali alikua anatoka mbezi beach,,,shukrani Mayalla for showing me the city.
 
acha kujikweza na dharau, inawezekana huko uko kutokana na wazazi wako kutokuwa waaminifu na kujilimbikizia mali za nchi hii.
mji unasehemu nzuri na wako watu wenye kitato kikubwa na kizuri kuliko huko kwenye kustahili kuwa mashamba ya mpunga.
 
Mvua kidogo tu ikinyesha Mbezi beach yote ni mafuriko...


Unajua ni kwa nini? Kwa sababu wamejenga hovyo na kuziba Mito, hivyo maji yakitoka Kibaha huko hayana pa kupitia.
Na ndicho ninachokiongelea!
 
Acha kujidanganya Bianadamu is unequal creature, Dunia nzima inalitambua hili, swali langu kwa nini ma low income hawavamii O’bey, Upanga au Masaki?


Una akili ndogo sana Barbarossa,
Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inasema katika Ibara ya 12(1):
"Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa"

Binadamu wote wako sawa chini ya Sheria. (Equality Before the Law)
Awe tajiri au masikini, mwanaume au mwanamke, amesoma au hajasoma n.k
Na huu ndiyo msingi wa hili Taifa la Tanzania ambalo alilijenga Mzee Nyarere.

Wewe ni umesomea wapi shule ambako umefundishwa kwamba Binadamu ni Un-Equal Creatures ???
Hebu tutolee huu Ujinga wako hapa...
 
acha kujikweza na dharau, inawezekana huko uko kutokana na wazazi wako kutokuwa waaminifu na kujilimbikizia mali za nchi hii.
mji unasehemu nzuri na wako watu wenye kitato kikubwa na kizuri kuliko huko kwenye kustahili kuwa mashamba ya mpunga.


Mwingine huyu hata ninachomaanisha haukielewi, ni wapi ninapojikweza? Unaijua historia ya Mbezi Beach? Au kwa nini Nyerere alianzisha Mbezi Beach?
Au kwa nini Nyerere alifanya Mbezi Beach kuwa tofauti na Sinza?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…