Malori ya mkutano wa CCM

Mimi sitaenda mpaka nijue msanii gani anaperfom siunajua ela ya viingilio kuwaona ni kubwa sasa hapa live alafu free...naomba mnijuze wasanii wangapi watakuepo
 
Mafuso yanakimbia utafikiri yanaendeshwa na Michael Schumacher ili yaende trip nyingi mengi yanatokea bagamoyo, mkuranga kibiti chalinze na kibaha
 
CCM yamwaga mamilioni kuivaa CHADEMA
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Kinyume na madai ya CCM kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na CHADEMA ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo wa CHADEMA ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho. Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa CHADEMA kwa kupata watu wengi, CCM imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.


Mbali ya kusombwa kwa magari, CCM pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.
Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.


Kana kwamba hiyo, haitoshi, CCM imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.
Baadhi ya wasanii hao ni Diamond, Marlaw, Frola Mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya Rais Jakaya Kikwete.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.
Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa CCM unaoendelea katika ngazi mbalimbali.


"Kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na Mzee Mkapa, Mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete hatakuwepo jukwaani," alisema Nape.
Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC), Abdulrahman Kinana na Nape mwenyewe.


"Mzee Kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha Uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.
"Wasira atajikita kwenye uchumi, Dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, Magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini Dar es Salaam," alisema Nape.

Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA, CCM nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na Televisheni ya ITV na baadhi ya vituo vya redio.
Aliwataka wananchi, wanachama wa CCM na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015.


CHADEMA yaipa masharti magumu
Akizungumzia mkutano huo wa CCM, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.
Akizungumza kutoka Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema CCM inatakiwa kuwaambia Watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za Watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.
CHADEMA pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa CCM waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie Watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

"CCM isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.
"Tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo," alisema Dk. Slaa.
 
attachment.php
 
Wana JF magari yamekodiwa ni balaa niko huku mbweni kuna coaster za kufa mtu zote zimepigwa private kwa ajili ya CCM. Hivi hawa jamaa bila kutoa usafiri hivi watu wanaweza kwenda kweli hii ni aibu
 
RC apiga marufuku malori kubeba abiria
Send to a friend
Saturday, 09 June 2012 08:15
0diggsdigg

Salim Mohammed, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, amepiga marufuku magari ya mizigo kubeba watu kwenda kwenye mikusanyiko ya watu wengi, ikiwamo misibani na harusini lengo likiwa ni kuepusha maafa yanayotokana na ajali.

Agizo hilo limekuja baada ya kukithiri kwa vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, ambazo husababishwa na magari ya mizigo kubeba watu kwenda misibani, maharusini na minadani.
Mwaka jana watu 24 walipoteza maisha na wengine 39 kujeruhuiwa na kupata ulemavu wa maisha.
Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafirishaji na wamiliki wa magari ya mizigo juzi, Gallawa alisema kuanzia sasa ni marufuku magari ya mizigo kubeba watu na kuwapeleka katika mikusanyiko.

Gallawa alisema imekuwa kawaida kwa watu wa Tanga kutumia magari ya mizigo kwenda katika shughuli za jamii na kusahau maafa ambayo yanaweza kutokea, huku wakiacha usafiri wa mabasi.

“Kuanzia sasa ni marufuku kwa magari ya mizigo kubeba watu na kuwapeleka katika sherehe au misibani, tunashuhudia maafa ya mara kwa mara yanayotokana na ubebaji watu kwenye malori, sasa basi!” alisisitiza Gallawa.

Aliwata wakazi wa mijini na vijijini kuacha kutumia usafiri huo, kwani umekuwa ukipoteza roho za watu wengi na watumie mabasi ambayo ndiyo wenye haki za kisheria kubeba abiria.
Kuhusu tabia ya baadhi ya madereva kuweka miti na majani barabarani gari linapoharibika, Gallawa alisema watu hao wamekuwa wakichafua mazingira kwani gari hilo likitengenezwa hawaondoshi uchafu huo.

Alisema tabia hiyo imekuwa kero na wakati mwingine husababisha ajali bila sababu za msingi, hivyo kila kijiji kinatakiwa kuwa na walinzi ambao watanakili namba za magari yanayofanya hivyo.




Huyu RC wa Tanga nafikiri hajui anachokifanya!

Yeye ni mteule wa Rais Kiwete ambaye pia ni Mwenyekiti wake wa CCM Taifa. Sasa Kiwete akisikia kuwa RC wake Tanga anazuia malori yasibebe abiria haoni kuwa anajipalia mkaa? Maana MALORI hayahaya ndiyo yanatumika leo kubeba MAZEZETA wa chama cha CCM kwenda (Jangwani)CHADEMA square.

Hivi siku NEPI na KIWETE wakienda Tanga kufanya mikutano ya magamba watatumia usafiri gani?????????????

Kazi kweli kweli.
 
ikiwezekana hata picha kabisa,mie niko jangwani kwa sasa naona wanaendelea kusomba viti vya plastic vyeupe viko kama 1,000 na kujenga stage na wanaandaa mabango.Full ulaghai ukipita mgao wa 10,000 nitakujuza.
Mkuu vipi ubwabwa wameshaleta?? Mimi sisogei jangwani hadi kwanza niwe na uhakika na hilo.
 
Kubeba watu kwa maroli sio ishu, ishu ni mwitikio wa watu hao kupanda maroli kama mbuzi. Ikiwa unakipenda chama choko utapanda hata trekta achilia mbali roli.
 
Mkuu vipi ubwabwa wameshaleta?? Mimi sisogei jangwani hadi kwanza niwe na uhakika na hilo.

Ubwabwa bado ila sioni dalili, kuna dala dala za mbagali zinaleta watu wanatelemkia kariakoo then wana kuja kwa bashasha huenda wamepewa chao.Ngoja nijisogeze nione taratibu za mgao zilikuwaje.
 
Tuko Jangwani tunasubiri mgao kwani hapa tunakuja kuchukua ili tukachangie kwa pipoz power.

Kama hujafika nijulishe nikupe update.

Hivi ina maana jioni tukiona kwenye TV si wote mtakuwa members wa CCM!!!!!!!

Kumbe wengine mmefuata mgao na ubwabwa tu, lakini hamuna upenzi na CCM



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Mwenye taarifa kama Lusinde atakuwepo anijuze tafadhali ili nami nisogee nikasikilize matusi live.
 
Mimi sitaenda mpaka nijue msanii gani anaperfom siunajua ela ya viingilio kuwaona ni kubwa sasa hapa live alafu free...naomba mnijuze wasanii wangapi watakuepo

wafuatao watatumbuiza

.ay,diomond,fa,barnaba,lina, bi kidude,chege,temba, alikiba,mzee yusuph,mashauz classic,comedy original,mc mpoki, mzee wa matusi lusinde. Usikose chadema square
 
Tupate idadi ya Fuso zilizosomba wanachama.

kuna tatizo gani kusomba wanachama...?! si wanachama wa kwao wa CCM .... ama ulitaka watembee kwa miguu kwenda mkutanoni....

CDM mnaweza mkaiga mkihitaji .. ni uwezo tu wa kichama... na kujipanga vizuri ..
 
Back
Top Bottom