Mall mpya Jijini Mwanza ni kituko cha karne

Kuna kigorofa naona anakipandisha kwa upande wa nyuma iv...huyu mbunge kinywa mgongo chake anakitumia vibaya
Tiyari kishazingua hata akijenga hicho kighorofa hakitokuwa na utofauti na ki-lodge cha uchochoroni kilichozungukwa na maduka.
 
Wanao haribu ni wanao simamia gorofa 3 kati kati ya mji wanafanya jiji lisikae kama Newyork
 
Hapo shida mi naona itakuwa kwa manispaa na halmashauri zetu maana wao lazima wapitishe design na michoro ya project husika. Sasa sijui ni ushamba? Upeo mdogo? Au rushwa? Wanapitisha design vituko vitupu...
Uongozi wa jiji la Mwanza ni tatizo, kwa sababu kuna madudu mengi sana yanafanyika katika halmashauri hizi mpaka unajiuliza iwapo kuna wataalamu na wasomi wanaona yanayoendelea au wapo tu kushibisha matumbo yao.
 
Huyo maboto ni muhuni kama wahuni wengine, na viongoz wa jiji hawana wanachowaza zaidi ya kunenepesha vitambi vyao.
 
Kwanza mwanza is not even a proper city, based on infrastructure, and urbanisation. People are right when they call it a big village.
Sote tunajua tukitafuta hizo proper city, hapa Tanzania kwetu ni matusi. Cha msingi nikuziboresha hivyo hivyo zilivyo kwa kujaribu kuzipa mwonekano mzuri unaokosekana, ebu fikiria barabara ya mjini kisesa endapo itapanuliwa kuwa barabara kuu ya njia nne ila pembezoni mwake ndipo zinapoendelea project za vituko namna hii, we unategemea hiyo sifa ya jiji lenye mvuto unaitoa wapi?
 
Msimuonee Maboto wivu. Pale siyo Mall bali amejenga kwa wafanyabiashara mbalimbali kukodi vyumba vya biashara. Acha wivu na wewe jenga kama Maboto.
Usitumie neno "Wivu" vibaya na pia acha ushamba, Mwanza ni jiji siyo kijiji kile cha kila aliyeuza mazao huko shamba akijisikia kujenga vibanda basi na ajenge kila mahali.

Kuna kanuni na sheria zinazoongoza maendeleo ya mji, hatuwezi kuwa na mji shaghala-baghala ambao hauna mpangilio.

Vilevile usijifanye msemaji wa Maboto sisi hatukumtuma atutangazie kuwa anajenga Mall ni yeye ndiye aliyeleta proposal nakutuaminisha hivyo na hamna kosa lolote tukioji kwanini amefanya sivyo tofauti na ilivyotarajiwa.
 
Yani mwanangu nikipita pale roho inaniuma sana.Kile kilichofanyika ni kuhujumu maendeleo ya mwanza.

Mijitu ipo ofisini inakuna vitambi kumbe inaruhusu ujinga ujinga
 
Huyo maboto ni muhuni kama wahuni wengine, na viongoz wa jiji hawana wanachowaza zaidi ya kunenepesha vitambi vyao.
Huyu jamaa wa mikopo humiza inaonekana ana mkono mrefu wa kula nao, hivyo hata akifanya madudu anafumbiwa macho tu. Maana kilichofanyika pale si cha afya kwa future ya jiji la Mwanza.
 
Maboto pale kaharibu sana lile eneo aise ,kajenga madarasa ya shule bana
[emoji23] Waambie wenda wakaelewa,[emoji124][emoji124] maana tukisema tunaonekana kama tunapinga maendeleo ya jiji la Mwanza[emoji1787]
 
Hiyo ngoma ilikuwa ni proposed kabisa na ilikuwa na mchoro wake kabisa ilikuwa imebaki tu utekelezaji, sasa sijajua ni mdudu gani aliingia kwenye kichwa cha investor mpaka akapindua plan na kufanya yake.
Mbona Kuna eneo limeachwa pembeni kubwa tu atajenga tu
 
Yani mwanangu nikipita pale roho inaniuma sana.Kile kilichofanyika ni kuhujumu maendeleo ya mwanza.

Mijitu ipo ofisini inakuna vitambi kumbe inaruhusu ujinga ujinga
Kwa mwenye akili timamu na mzalendo lazima ujue tu pale kuna shida na jambo la kipumbavu limefanyika lakini kwa hawa wachumia tumbo wazee wa viyoyozi hilo haliwanyimi usingizi, ni mwendo wa kuzorotesha maendeleo ya mji na kupokea vibunda.
 
Mbona Kuna eneo limeachwa pembeni kubwa tu atajenga tu
Sasa Mall gani ndugu ulishawai kuona mbele yake unaanza kujenga vibanda vya maduka mahali pa mbele? Au ndiyo tuseme baada ya hapo ataweka tena ukuta kutenganisha? Ukweli usemwe tu ule mchongo tiyari ushakuwa mchongoma.
 
Afumue tu
Hivyo vibanda akajenge buswelu
Anaanzaje sasa!?[emoji23]Na wenye mamlaka washamruhusu na project yake ya wiki mbili inaelekea ukingoni, hivi karibuni anaanza kupangisha[emoji1787][emoji1787]
 
Hivi hilo jengo la sijuwi gorofa 9 (mall) mnalo lilia ,litawapa ugali wa kula na familia zenu?,acheni malalamiko pesa za maboto yaye mwenyewe ndiyo anaamua afanye nini ata angejenga vyoo vya kulipia ni fedha zake.Na hiyo mall si mnataka kwenda kupiga picha tu kwani kuna cha zaidi ya hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…