Kilimo kina changamoto nyingi ambazo saa ingine hasara husika hadi kwa mlaji.
Mie ilishanitokea nimenunua embe au nazi au tikiti maji kufika nyumbani unakuta ndani limeoza halifau kutumia ila kwa nje linaonekana vizuri tuu.
Ubovu huu ujiugundua wakati unanunua bidhaa unaikataa na kuchukua mbadala ambayo iko nzima. Kutokujua kwa Ubovu wa bidhaa huko kunaanzia mbali, unaweza kuta yule muuzaji sokoni nae kununua toka kwa mkulima embe nje zuri ila ukikata ndani funza watupu huwezi kula.
Mkulima nae aidha alipewa mbegu hafifu au mbolea iliisha muda wake haikuwa na nguvu au madawa ya kuzuia wadudu hakuweka au alitapeliwa akauziwa maji badala ya dawa..... nani haswa anatakiwa abebe hio hasara ya embe bovu ndani ila nje zima? Ndomaana saa ingine muuzaji anapandisha bei ya bidhaa kufidia zile ambazo hazitauzika zitakuwa mbovu. Mfano nazi ingeweza kuuzwa Tsh 300 hadi 400 na akapata faida,ila kubeba risk ya zilizooza na hazitauzika wakati yeye keshazilipia toka kwa mkulima kila nazi itauzwa Tsh 1000 ukibembeleza Tsh 800. Hapo akikuta zote nzima basi heri kwake muuzaji.
Kilimo kina changamoto nyingi sana, jaribu wakati mwingine kuchukua bidhaa kutoka kwa wakala mkuu yaweza punguza tatizo.